Air Tanzania yapigwa Marufuku kufanya safari zake Katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya kwasababu za Kiusalama

Air Tanzania yapigwa Marufuku kufanya safari zake Katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya kwasababu za Kiusalama

ni ujinga kupingana na ukweli kwa sababu kupinga hakufanya uongo kuwa kweli. Ndiyo maana kuna mashirika ya kusimamia usafiri wa anga. Timiza masharti iweze kuingia kama huwezi kaa huko.
Umejua ni masharti gani ATCL haija-comply? Au wewe ukisikia beberu amesema basi ni 100% wako sawa hujui kuwa hapa duniani kuna figisu nyingi sana. Bwana mdogo kuwa uyaone!!
 
Mnapewa funzo bado hamuelewi na wala hamjifunzi kitu ndani yake?

Fanya uswahili nyumbani kwako, usiupeleke kwingineko.
Kama huna viwango na hufuati taratibu zilizopo, unataka watu washushe viwango kwa ajili yako?

Hovyo Kabisa.

Kuna mengi ya kuwalalamikia wakoloni hao; lakini kuna upuuzi usio vumilika kwenye nchi za hovyo kama hii yetu sasa hivi.
 
Naona hapo kuna kiwingu cha kisiasa tu. Ndege zote za ATCL zinazosafiri masafa marefu ni mpya sana kuliko baadhi ya ndege za mashirika ya Ulaya, na zimetengezwa na makampuni yanayoaminika sana Ulaya,yaani Boeing na Airbus. Kwa tuhuma hizo za kutokuwa ndege salama inabidi ATCL wawashitaki watengezajiowa ndege hizo (Boeing na Airbus) kama waliwauzia ndege zisizokuwa salama huko Ulaya; yaani mzigo huo wawatwishe washirika wao.
 
Ujinga ni mzigo!

Kusoma hujui au lugha ni tatizo wewe kunguni wa mama Abdul?

Umeambiwa wamezuiwa bada ya kushindwa kufika viwango vya kimataifa vya usalama wa anga sasa vyombo vinayodhibiti ubora wa viwango hivyo ulaya huko vinamilikiwa na upinzani?
 
Hii ya Kagame ni mfano tu ila kutua Heathrow sio utani
Sisi hata kuwa na ubia na wengine hatuwezi
Angalia Kenya Airways hata ticket zao ziko juu kutoka London to Nairobi
Kuna Ethiopian pia inatua Heathrow pia na hawajaanza leo napanda sana kipitia Addis to Dar
Hata sisi tunaweza ila ujanja ujanja mwingi tu
Air Tanzania imeshatua sana tu hapo Heathrow siku za nyuma.
 
Inatakiwa sasa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Eng. Peter Ulanga ajitokeze haraka kuelezea kadhia hii ya hatari kwa usalama wa abiria watakaotumia ndege katika anga la nyumbani, pia kwenda Dubai, India na China usalama upo vipi.
 
Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza kuzuia ndege za shirika la ndege la Air Tanzania kuingia katika anga la nchi wanachama wake, jumla ya nchi 28, kwa madai kuwa shirika hilo halijakidhi vigezo vya kimataifa vya usalama wa anga.
 
ATCL zinazosafiri masafa marefu ni mpya sana kuliko baadhi ya ndege za mashirika ya Ulaya

Air Tanzania wasifanye mzaha maana pamoja na mamia ya abiria kutumia ndege za ATC pia Rais hutumia huduma hizo katika ziara kibao, mfano juzi juzi Kwenda Rio de Janeiro Brazil, China n.k

President of Tanzania, Samia Suluhu Hassan - G20 Rio De Janeiro Brazil

View: https://m.youtube.com/watch?v=mDBuSC9It0g
 
Kwani ina route za huko au ni ile ya akina Mengele?😂
Zipo route za kwenda huko hasa kwa viongozi wetu wakuu. Na ikimbukwe moja ya mikakati ya Tanzania ni kuhakikisha shirika hili linabeba watalii moja kwa moja toka nchi za ulaya na kwingineko duniani na kuwatua nchi kwetu kutembelea vivutio mbalimbali. Wazungu hawakubali kupigwa pesa yao mara mbili.

Kama kuna mambo ya kurekebisha ili kukidhi viwango vya Ulaya ni sawa yafanywe.
 
Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza kuzuia ndege za shirika la ndege la Air Tanzania kuingia katika anga la nchi wanachama wake, jumla ya nchi 28, kwa madai kuwa shirika hilo halijakidhi vigezo vya kimataifa vya usalama wa anga.

“Umoja wa Ulaya leo umesasisha orodha ya mashirika ya ndege yanayozuiwa kuingia au kuwekewa vikwazo vya kiutendaji ndani ya umoja huo,” inasema taarifa ambayo The Chanzo imeipata. “Air Tanzania sasa imeongezwa kwenye orodha hiyo.”

Sababu kuu ya kuijumuisha Air Tanzania, kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni changamoto za kiusalama zilizobainishwa na Wakala wa Usalama wa Anga wa Umoja wa Ulaya (EASA). Kwa hatua hiyo, Air Tanzania imejiunga na mashirika mengine 129 yaliyopigwa marufuku, ikiwa ni pamoja na Air Zimbabwe (Zimbabwe), Avior Airlines (Venezuela), Blue Wing Airlines (Suriname), Iran Aseman Airlines (Iran), Fly Baghdad (Iraq), na Iraqi Airways (Iraq).

Kamishna wa Usafiri Endelevu na Utalii wa Umoja wa Ulaya, Apostolos Tzitzikostas, amesema EU iko tayari kushirikiana na Air Tanzania ili kusaidia shirika hilo kufikia viwango husika vya usalama. “Uamuzi wa kuijumuisha Air Tanzania kwenye Orodha ya Usalama wa Anga ya EU unatokana na dhamira yetu ya kuhakikisha viwango vya juu vya usalama kwa abiria barani Ulaya na duniani kote,” amesema Tzitzikostas.

“Tunatoa wito kwa Air Tanzania kuchukua hatua za haraka kurekebisha changamoto hizi. EU iko tayari kushirikiana na mamlaka za Tanzania kuboresha usalama wa ndege za Air Tanzania na kuhakikisha zinafikia viwango vya kimataifa,” ameongeza.

Tangu mwaka 2016, Tanzania imekuwa ikiboresha shirika lake la Air Tanzania kwa kununua ndege mpya, zikiwemo Boeing 787-8 Dreamliner mbili, Dash 8 Q400 tano, Airbus A220-300 nne, Boeing 767-300F ya mizigo moja, na Boeing 737 MAX 9 tatu. Air Tanzania imekuwa ikifanya safari katika maeneo 14 ya ndani ya nchi, nane ya kikanda, na matatu ya kimataifa—China, India, na Dubai.

Hata hivyo, tangazo hili la Umoja wa Ulaya linaweza kuwa changamoto mpya kwa shirika hilo, ambalo sasa linatarajiwa kuchukua hatua madhubuti kushughulikia masuala ya usalama wa anga.
View attachment 3176052
View attachment 3176054
*********

Commission updates EU Air Safety List and adds Air Tanzania to the airlines banned within the European Union

Top
The European Commission today updated the EU Air Safety List, the list of airlines that are subject to an operating ban or operational restrictions within the European Union, because they do not meet international safety standards. Ensuring the highest level of air safety for Europeans and all other travelling passengers is at the very heart of the Commission's aviation safety policy.

Following today's update, Air Tanzania has been included on the List. The basis for this decision is safety concerns identified by the European Union Aviation Safety Agency (EASA). These also led to the decision not to grant Air Tanzania a Third Country Operator (TCO) authorisation.

Commissioner Tzitzikostas also welcomed EASA's positive decision on 29 November 2024 to lift the Third Country Operator (TCO) suspensions imposed on Pakistan International Airlines (PIA). Since the TCO Authorisation was suspended in 2020, PIA and the Pakistan Civil Aviation Authority (PCAA) have made substantial progress in improving safety performance and oversight capabilities. PIA is now allowed to resume operations to the EU. Furthermore, Airblue Limited, another Pakistani airline has also received EASA's TCO Authorisation.

Following today's update, a total of 129 airlines are banned from EU skies:

100 airlines certified in 15 States, due to inadequate safety oversight by the aviation authorities from these States;
22 airlines certified in Russia, as well as 7 individual airlines from other States, based on serious safety deficiencies identified: Air Tanzania (Tanzania), Air Zimbabwe (Zimbabwe), Avior Airlines (Venezuela), Blue Wing Airlines (Suriname), Iran Aseman Airlines (Iran), Fly Baghdad (Iraq) and Iraqi Airways (Iraq).
Two additional airlines are subject to operational restrictions and can only fly to the EU with specific aircraft types: Iran Air (Iran) and Air Koryo (North Korea).

Background

Today's update to the EU Air Safety List is based on the unanimous opinion of Member State aviation safety experts, who met in Brussels on 19 to 21 November 2024 under the auspices of the EU Air Safety Committee. This Committee is chaired by the European Commission with support from EASA. The European Parliament's Transport Committee also supports the update. Decisions under the EU Air Safety List are based on international safety standards, and notably the standards decreed by the International Civil Aviation Organization (ICAO).

EU COMMISSION
Kwanza hatuna route za huko
 
Kwa udogo wa ubongo wako ulitakiwa kuhurumiwa lakini wengi watakucheka. Air Tanzania inaweza kuwa tishio kwa nani? Hii ambayo nina uhakika miaka 10 ijayo haitakuwepo au itakuwa imekabidhiwa kwa mwarabu?
Eti nina uhakika,kwani uhakika wako wewe unatusaidia nini sisi,wewe ni Mungu,ulijua leo TZ ingekuwa na treni ya SGR au ulijua kuwa hilo shirika lako la ATCL lingeweza kumilike ndege zake lenyewe tena mpya zaidi ya 7,acha kuishi maisha ya kusadikika ya kufikiri kuwa mtu mweusi hawezi fanya miujiza...
 
Air Tanzania imeshatua sana tu hapo Heathrow siku za nyuma.
Hiyo ilikuwa miaka ya 70 na 80 nakumbuka sana
Enzi hizo tulikuwa na uzalendo haswa boss
Hata Somali Airlines ilikuwa inakuja Tz na kulikuwa na ndege nyingi zinatua Dar na kuondokea Dar kuja nje
Nimepandia huko Air France, Lufthansa, SwissAir hizo nimepanda na kuja nazo nje miaka ya nyuma sana ikiwamo na ndege zetu pia
Je tumepatwa na nini leo?
 
Back
Top Bottom