Sasa huyo mwenye lorry ameovertake wapi hapo na amenyoosha body yake.Wamesema ni uzembe wa dereva wa lori-Howo kuovertake sehemu isiyo ruhusiwa kitu ambacho ni kinyume na uhalisia kwa mujibu wa picha za tukio
Hata wewe ungekuwa ni yeye lazima tu ungefanya alichofanyaDah!
Yaani ameandika maelezo ya uongo hadi mimi nisiyejua sheria za barabarani naona ni uongo.
Kwanza nimeshindwa kuelewa alichoandika.
Kuandika kitu kisichoeleweka?Hata ww ungekuwa ni yeye lazima tu ungefanya alichofanya
Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Umefikiri vizuri lakni mbona picha inaonyesha tela la howo lipo straight kwenye line yake.!!Ukute Howo alimaliza kuovateki na kurudi upande wake wa kushoto lakini kutokana na mwendo kasi wa Ashok ya nyuma akashindwa kufunga break akaamua kutanua kulia ili asimgonge Ashok mwenzake ndio akakutana na Howo. Just thinking [emoji848].
Nakubaliana nawe picha hufanya mirror but hizo namba za gari na maandishi ya laber ya gari vingesomeka kinyume cha maumbile kama hivi inavyoonekana.Dereva wa Lori alijaribu kurudi kwenye njia yake baada ya kuona uso kwa uso lakini bahati mbaya horse tu ndio ilifanikiwa, tela ndio ikasababisha ajali
ukitizama kwa makini kwenye lami hiyo picha ya mwisho utaona jinsi tairi za kichwa zilivyoacha alama kwenye lami kutoka upande mmoja kwenda mwingine
Ifahamike pia picha huwa inajigeuza hapo ndio wengi mnajichanganya kupata uelekeo
Sahihi nimemuwekea picha kabisa aseme lingineKama picha 'imejigeuza' hayo maandishi 'POLISI' kwenye magari yao yangedomeka 'SILIPO', usitetee ujinga.
Vv
Kuteteana muhimuKuandika kitu kisichoeleweka?
Yaani hadi picha zinaonyesha[emoji38]
Yan picha igeuzwe ala neno "polisi" na platnumber zisomeke kutokea bila kugeuka? Alaf ebu angalia hilo tela uoni kuwa lipo straight inamaana jamaa wa roli alikuwa upande wake?Dereva wa Lori alijaribu kurudi kwenye njia yake baada ya kuona uso kwa uso lakini bahati mbaya horse tu ndio ilifanikiwa, tela ndio ikasababisha ajali
ukitizama kwa makini kwenye lami hiyo picha ya mwisho utaona jinsi tairi za kichwa zilivyoacha alama kwenye lami kutoka upande mmoja kwenda mwingine
Ifahamike pia picha huwa inajigeuza hapo ndio wengi mnajichanganya kupata uelekeo
hahahaha likaenda kuanza upyaNahisi nimezeeka, huo mtiririko wa maelezo nimetoka kapa yaani sijaelewa kabisa nimeona kama kulikua na gari lilikua kwenye ajali halafu likaja tena kwenye ajali.
Tatitizo letu wabongo, kila mtu anajifanya ni mchambuzi wa kila kitu, siasa, sheria, uandishi wa habari n.k hebu waacheni majeruhi watibiwe wapone tuache ujuaji.Police walikuwa wanashindana hapo huko walikokuwa wanaendaa lori hana makosa hapo hata kidogo
MmmmmmmmmmhNimejaribu kusoma kwa utulivu kisha nikaangalia picha, naona kama yanapingana na uhalisia, anyway Wajuvi nisaidieni, lory HOwo ame-ovrtake kweli hapo??
Afande taarifa ya ajali:
KAB/TR/ar/16/2021(×)ajali ya magari manane kugongana na kusababisha majeruhi na uharibifu wa magari (×) mnamo tar 14/11/2021 majira ya saa 18:30 huko katika kijiji cha Kwedilomba kata ya Kwedibomba tarafa ya mzundu wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga barabara kuu ya Segera-Chalinze gari No.T.131 DVU aina ya HOW yenye tela No.T.329 DMR ikiendeshwa na Saimon S/O kristo @Mwanyila, 36yrs, Mbena, mkazi wa Kibaha Pwani akitokea kabuku kuelekea Chalinze alipokuwa akijalibu kulipita gari la mbele yake mahala pasipo ruhusiwa ndipo ghafla mbele yake kukatokea gari nyingine iliyokuwa ikitokea Chalinze kuelekea kabuku yenye No.Pt.4036 ashok leyland mali ya jeshi la polisi Tanzania likiendeshwa na H.3637 CPL Juma wa chuo cha Polis CCP Kilimanjalo na ndipo dereva wa gari No.Pt.4036 alisimama ghafla ili kuepuka ajali isitokee na ndipo baada ya gari hiyo kusimama ghafla ikatokea gari nyingine kwa nyuma iliyokuwa ikitokea Chalinze kuelekea Kabuku PT.4087 ashok leyland ikiendeshwa na F.7658 CPL John Robert wa makao makuu madogo ya polisi DSM na kugonga kwa nyuma.
Ghafla tena ikaja gari nyingine kwa nyuma No.Pt.4097 ashok leyland ikiendeshwa na F.5889 CPL Kigiri wa Polisi makao makuu madogo ya Polisi DSM na kusimama ghafla PT.4087 ashok leyland na kusababisha gari No. PT.2370 Isuzu bus ikiendeshwa na g.6123 CPL abel wa chuo cha polisi Kidatu na kugonga ubavuni gari no.Pt.4087 ashok leyland pia ikatokea tena gari No.T.573 AYR toyota corolla ikiendeshwa na Amin S/O UR Rasul@Khan, 60yrs, mkazi wa Tanga na kusimama ghafla baada ya kuona ajali na kusababisha gari no.SU 44275 gx v8 mali ya TANESCO DSM ikiendeshwa na Tuma S/O Hassan lean na kuigonga kwa nyuma gari hiyo no.T.573 AYR Toyota corolla pia ikasababisha gari nyingine yenye no T.773 CND Toyota hilux kuigonga kwa nyuma gari hiyo no.Su.44275 GXV8 TANESCO na kusababisha majeruhi kwa watu 16 ambao ni 1.D.8420 s/SGT John Mwakipesile 2.Pf.18891 insp sister 3.G.6123 CPL Abel ambao wote watatu wamepelekwa hospitali ya rufaa Bombo kwa matibabu
Na 4.Pf.17534 insp Rashida 5.Pf.18326 insp Nyalugembe 6.Pf.17896 insp Gonga 7.Pf.18202 insp Said 8.Pf.17166 insp Ally juakal 9.Pf.17899 insp Sanya 10.Pf.18445 insp pangane 11.Pf.17691 insp Peter 12.Pf.18719 insp Ohusso 13.Pf.17321 insp Ilomo 14.Pf.18616 insp Anthony 15.Pf.17674 insp Zongho 16.H.1659 pc gift (×) majeruhi wote wameumia sehemu mbalimbali za mwili na kutibiwa kituo cha afya Kabuku na kuruhusiwa (×) chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari no.T.131 dvu how yenye tela no.T.329 dmr kujalibu kulipita gari iliyokuwa mbele yake pasipo kuchukuwa tahadhali (×) dereva amekamatwa yupo mahabusu kituo cha polisi Kabuku kwa ajili ya mahojiano (×) eneo la tukio limekaguliwa na acp. Sofia jongo rpc Tanga akisaidiwa na ssp leopord .N. Fungu rto tanga , sp. Elias Rwambano ocs Kabuku, a/insp Rajabu kaimu DTO Handeni pamoja na g.3191 cpl Mussa ambaye ndiye amechora na kupima eneo la tukio (×)///////////
Taarifa kwa maandishi inafuata //////////
Toka rto tanga ///////////
Mkuu ndio TZ iyo na polisi ndio hao hapo wanaogopa kuwajibishwa kwaiy lazma wambebeshe gunia la miba dereva wa Lori ila wanaweza wakamwachia baadae.Hapa natafakari hilo lorry lingekua ni mali ya jeshi sijui wangetunga uongo gani?
Maskini Kristo anabebeshwa msalaba na kwenda kusulubiwa kwa kosa asilolitenda.
Kaa kimya bwege wew sio kila comment lazma uijibu fanya yako.Cheki unavojifanya mjuaji utadhani ulikuwepo wakati ajali inatokea...
Nini kibaya hapo nimeongea ina maana kwa elimu ya msingi uliyosoma hata picha pia umeshindwa kuitafsiri??grow up dude...Tatitizo letu wabongo, kila mtu anajifanya ni mchambuzi wa kila kitu, siasa, sheria, uandishi wa habari n.k hebu waacheni majeruhi watibiwe wapone tuache ujuaji.
Kwahiyo RPC na huyo CPL na mchoraji walikuwepo wakati wa tukio au nao walitumia mazingira baada ya ajali kutoa maelezo waliyotoa? Jitahidini kuwa wakweli maisha yenu yatakuwa ya Amani na mapokeo mema kwa Mungu Baba.Acha kujifanya MUCH-KNOW wewe.
Ulikuwepo wakati ajali inatokea.
Hizo ni picha za baada ya ajali kutokea, zisikufunge akili.