Ajali iliyoua watu 20 Tanga, yadaiwa wakati wa uhai wake, marehemu alisema akifa mwili wake usipelekwe Kilimanjaro

Acheni kumsingizia marehemu wa watu. Kishamaliza safari. Hata kama aliyesema hayo, hakuna mwenye uwezo kama huo hata kama angekuwa hai. Nadhani tuangalia chanzo kingine kama vile mwendo kasi, ubovu wa gari, barabara, matatizo ya dereva kama uwezo wa kuona, kuamua, kufikiri, ulevi, uchovu, magonjwa ya akili na mengine mengi. Kwetu wataalamu wa haya mambo, linapotokea kama hili tunaangalia angles nyingi mwanangu. Mwache marehemu apumzike.
 
Ndugu zetu wa Islam wanaita elim Dunia. Hii ni elimu ya kujuwa Yale hatuyaoni kwa macho. Jr Mshana amekuwa mwalim mzuri sana hapa. Dunia inaenda kwa kasi. Angalia serikali ya sita inachokutana nacho.....🤔
 
Uongo.
 
Aisee
 
Una kiwango gani Cha elimu. Kipi Cha kwanza kuwa Duniani. Dini au dunia
 
serikali inatakiwa kuziangalia hizi kada za udereva vyema atleast dereva awe na form sex kichwani hawa vilaza wa veta from.4 failer watatumakiza
Umeongea utumbo Sana,ungejua madereva wazuri ni wale wasio na Elimu , kwakua wanatambua na kuthamini hiyo ndio kazi yao ,, hao wa chuo au form six hua wanaendesha pasipo kupenda hiyo kazi,,.. afu pia miundo mbinu ya Tanzania ndio kichochea cha ajali nyingi ...
 
Wachaga wengi wenye akili ,wanamjua Mungu na walistarabika huwa hawakimbilii kuzikwa kilimanjaro.nimekaa mbezi ya kimara tumezika wengi pale agape ,msingwa Mazulu na nk washamba ndio hukimbilia kuzikwa kwao
We sema ni wabahili wanaona taabu kutoa pesa kusafirisha mwili
 
Kuna ushauri humu Toka kwa viongozi kuwa kwenye kusafirisha msiba watu wasafiri tofauti tofauti wasipande chombo kimoja..huu ushauri vipi jamani tujadili.
 
Jamani, tusipende kutamka maneno bila kufikiria, na wale wanaoambiwa jambo, wasipuuzie! Jamani, maneno yanaumba! Hilo lililotokea ni nguvu ya neno katika uumbaji!
 
Ila wachaga wa Rombo ni wabishi sanaaa...
Me kuna mmoja niliishi naye yani ni mjuaji mpaka kerooo.
 
Hii inshu imenikumbusha jambo flani lilitokea mwaka 2014. Kuna mshikaji alifariki tulikuwa tunafanya nae kazi kambi moja ya kivuvi. Sasa baada ya kufariki bos hakuwepo ila walikuwepo tu viongozi wa kazi. Tukawa tumeandaa boat dogo tu la kivuvi kwa ajiri ya kusafirisha msiba na injini kubwa ya horsepower 40 kwa ajiri ya kuwahisha. Ukumbuke huku ziwa nyanza injini ya kawaida ya kazi ni horsepower 15. Mtumbwi uliondoka kama kilomita moja tu injini ikagoma. Wakafuatwa pale injini kuletwa kwa fundi haina tatizo ikafungwa tena kwenye boat safari ianze. Lakini haikuvuka pale pa mwanzo ikagoma tena. Ikaonekana hii inadharau haitaki kusafirisha maiti. Tukachukua injini mbili ndogo ndogo tukazifunga na zilikuwa zimetoka ziwani zikiwa hazina tatizo. Kwanza moja iligoma kuwaka palepale ila moja ikawaka wakawa wanaenda huku wanalekebisha ile ya kushoto lakini nazo hazikuzisi lile eneo. Wakawa wamefuatwa pale wakarudishwa. Ikabidi tumpigie boss kumwambia kila kilichotokea huku wakibadirisha tena injini. Cha kushangaza hata zile hazikuwaka kabisa. Kila mtu akaogopa inakuwaje injini tano zote zigome japo kampuni ina injini zaidi ya 14 lakini hakuna aliyediriki kuleta nyingine. Jioni yake boss akaja akakaa na viongozi wa kambi kisha wakamwita mama mzazi wa marehemu wakamwita wakaongea nae sisi hatukujua waliongea nini baada ya hapo wakafunga ile injini kubwa na kuiwasha safari ikaanza ikiwa ni usiku sasa. Tulibaki tunawasiliana nao tu na safari haikuwa na tatizo. Kumbe yule jamaa alikuwa anamdai mmoja wa viongozi pesa ya huko nyuma na alikuwa amempa kumtunzia ila aipoona kafariki ye alimpa tu mama yake malipo ya huo mkataba aliokuwa anao marehemu. Inamaana boss alipokuja aliwaambia viongozi wa kambi walipe kila deni la marehemu ndipo marehemu alikubali kwenda kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…