Ajali iliyoua watu 20 Tanga, yadaiwa wakati wa uhai wake, marehemu alisema akifa mwili wake usipelekwe Kilimanjaro

Ajali iliyoua watu 20 Tanga, yadaiwa wakati wa uhai wake, marehemu alisema akifa mwili wake usipelekwe Kilimanjaro

Wana jukwaa Salaam!

Kwanza natanguliza pole kwa wana ukoo wa Mrema kwa ajali iliyotokea na kuhusisha vifo vya watu zaidi ya 17.

Nimejaribu kujiuliza sana, hasa hii taarifa ya ndugu ambao wanatoa shuhuda kua marehemu alitoa sharti asiende kuzikwa kwao na watakaokaidi ataondoka nao. Mshana jr etc. wenye maarifa zaidi na mambo haya mwageni elimu kuhusu hili. Maana visa vya namna hii viko tele, nyingine nilishasikia kua maiti iligoma kuingia kaburini kwakua haikutaka kuzikwa pale n.k.View attachment 2509626View attachment 2509627
Acheni kumsingizia marehemu wa watu. Kishamaliza safari. Hata kama aliyesema hayo, hakuna mwenye uwezo kama huo hata kama angekuwa hai. Nadhani tuangalia chanzo kingine kama vile mwendo kasi, ubovu wa gari, barabara, matatizo ya dereva kama uwezo wa kuona, kuamua, kufikiri, ulevi, uchovu, magonjwa ya akili na mengine mengi. Kwetu wataalamu wa haya mambo, linapotokea kama hili tunaangalia angles nyingi mwanangu. Mwache marehemu apumzike.
 
Wana jukwaa Salaam!

Kwanza natanguliza pole kwa wana ukoo wa Mrema kwa ajali iliyotokea na kuhusisha vifo vya watu zaidi ya 17.

Nimejaribu kujiuliza sana, hasa hii taarifa ya ndugu ambao wanatoa shuhuda kua marehemu alitoa sharti asiende kuzikwa kwao na watakaokaidi ataondoka nao. Mshana jr etc. wenye maarifa zaidi na mambo haya mwageni elimu kuhusu hili. Maana visa vya namna hii viko tele, nyingine nilishasikia kua maiti iligoma kuingia kaburini kwakua haikutaka kuzikwa pale n.k.View attachment 2509626View attachment 2509627
Ndugu zetu wa Islam wanaita elim Dunia. Hii ni elimu ya kujuwa Yale hatuyaoni kwa macho. Jr Mshana amekuwa mwalim mzuri sana hapa. Dunia inaenda kwa kasi. Angalia serikali ya sita inachokutana nacho.....🤔
 
Yes nachopendea chagas wanadumisha mila wakati makabila mengine yakiona ni ushamba na ushirikina..mila zipo na muhimu. Mila zinasaidia mambo mengi sana na kuondosha mabalaa.
Ndiyo maana wanafanikiwa na ngumu kurogeka ovyoovyo kwenye mapambano ya maisha. Mila muhimu sana.
Uongo.
 
Copy and Paste.


Leo niwashirikishe jambo kuhusu ajali iliyotokea Tanga na kuua watu kumi na saba.

Marehemu aliyekuwa anasafirishwa ni Baba wa miaka 60+, alihamia Dar miaka nane iliyopita akajenga na kufanya biashara zake.

Alipokuwa kijana alioa mwanamke aliyekuwa tayari na mtoto mmoja wa kiume, kwa wakati huo ilikuwa ni aibu sana kuoa mwanamke aliyezaa nyumbani. Sina uhakika kama alipata mtoto mwingine na yule mama ila alimlea kijana aliyemkuta naye kama mwanaye wa kumzaa, akamsomesha hadi akafika chuo kikuu wakiwa Rombo.

Kutokana na upendo kupungua mama hakumheshimu baba tena uzeeni na kijana akaja kujua kumbe yule siyo baba yake wa kumzaa.

Mama akampeleka kijana kwa baba yake akiwa mwaka wa tatu chuo kikuu na kijana akahamia kwa baba yake kiasi kikubwa bila kumuonesha upendo baba mlezi aliyemlea na kumhudumia.

Baada ya kijana kupata kazi alihamia Dar na hakutaka mawasiliano tena na baba yake mlezi, jambo lililomuudhi sana baba yake huyo.

Baada ya mama kuwa haelewani na baba, baba aliamua kuhamia DSM na kuanza maisha upya na pia akamwambia yule kijana kwa sababu hataki kumpa heshima basi afanye maisha yake na kila mtu ashike hamsini zake.

Mzee aliugua na alipokuwa amelazwa Mloganzila kijana akaenda kumuona;
Mzee alikasirika sana na akamwambia alishamueleza kila mtu ajuane na maisha yake mwenyewe.....na pia akamwambia hata akifa asije kumzika maana alikosea na kumsononesha sana.

Kesho yake mzee akafariki; kijana akajiunga na ndugu wengine wa DSM wakapanga na kulazimishia kupeleka msiba na maziko nyumbani Rombo kinyume na matakwa/wosia wa marehemu; wengine walipinga kwa kukubali wito wa marehemu kuzikwa Dar maana hakutaka kuzikwa Rombo.

Safari ililazimishwa, lakini hatima yake ikaishia Korogwe, kwa kila aliyepinga kauli ya marehemu kupoteza uhai pale ajalini. Kijana aliyelelewa na marehemu alikuwa na wanaye wawili wote pia walifariki pale pale.

Sisi tupo level gani ya maamuzi kwenye familia?..... hivyo tusidharau mambo, hasa yale yanayokuwa na sababu na pengine sababu hizo zimefikiwa kwa uchungu mkubwa wa akili na moyo, tena bila madeko....uchungu wenye haki!
Aisee
 
Ninacho amini ninkwamba binadamu hafi akapotea, lakini anabadilika kutoka ubinadamu na kuwa aina nyingine ya kiumbe. Na hii inadhibitishwa na vitabu vyote viwili yaani Bible na Quaran..kwa maana kamba kuna wanao enda jehanam na wale wanao enda peponi. In both cases inaonyesha kuwa roho haifi bali mwili.
Una kiwango gani Cha elimu. Kipi Cha kwanza kuwa Duniani. Dini au dunia
 
serikali inatakiwa kuziangalia hizi kada za udereva vyema atleast dereva awe na form sex kichwani hawa vilaza wa veta from.4 failer watatumakiza
Umeongea utumbo Sana,ungejua madereva wazuri ni wale wasio na Elimu , kwakua wanatambua na kuthamini hiyo ndio kazi yao ,, hao wa chuo au form six hua wanaendesha pasipo kupenda hiyo kazi,,.. afu pia miundo mbinu ya Tanzania ndio kichochea cha ajali nyingi ...
 
Wachaga wengi wenye akili ,wanamjua Mungu na walistarabika huwa hawakimbilii kuzikwa kilimanjaro.nimekaa mbezi ya kimara tumezika wengi pale agape ,msingwa Mazulu na nk washamba ndio hukimbilia kuzikwa kwao
We sema ni wabahili wanaona taabu kutoa pesa kusafirisha mwili
 
Kuna ushauri humu Toka kwa viongozi kuwa kwenye kusafirisha msiba watu wasafiri tofauti tofauti wasipande chombo kimoja..huu ushauri vipi jamani tujadili.
 
Jamani, tusipende kutamka maneno bila kufikiria, na wale wanaoambiwa jambo, wasipuuzie! Jamani, maneno yanaumba! Hilo lililotokea ni nguvu ya neno katika uumbaji!
 
Ila wachaga wa Rombo ni wabishi sanaaa...
Me kuna mmoja niliishi naye yani ni mjuaji mpaka kerooo.
 
Hii inshu imenikumbusha jambo flani lilitokea mwaka 2014. Kuna mshikaji alifariki tulikuwa tunafanya nae kazi kambi moja ya kivuvi. Sasa baada ya kufariki bos hakuwepo ila walikuwepo tu viongozi wa kazi. Tukawa tumeandaa boat dogo tu la kivuvi kwa ajiri ya kusafirisha msiba na injini kubwa ya horsepower 40 kwa ajiri ya kuwahisha. Ukumbuke huku ziwa nyanza injini ya kawaida ya kazi ni horsepower 15. Mtumbwi uliondoka kama kilomita moja tu injini ikagoma. Wakafuatwa pale injini kuletwa kwa fundi haina tatizo ikafungwa tena kwenye boat safari ianze. Lakini haikuvuka pale pa mwanzo ikagoma tena. Ikaonekana hii inadharau haitaki kusafirisha maiti. Tukachukua injini mbili ndogo ndogo tukazifunga na zilikuwa zimetoka ziwani zikiwa hazina tatizo. Kwanza moja iligoma kuwaka palepale ila moja ikawaka wakawa wanaenda huku wanalekebisha ile ya kushoto lakini nazo hazikuzisi lile eneo. Wakawa wamefuatwa pale wakarudishwa. Ikabidi tumpigie boss kumwambia kila kilichotokea huku wakibadirisha tena injini. Cha kushangaza hata zile hazikuwaka kabisa. Kila mtu akaogopa inakuwaje injini tano zote zigome japo kampuni ina injini zaidi ya 14 lakini hakuna aliyediriki kuleta nyingine. Jioni yake boss akaja akakaa na viongozi wa kambi kisha wakamwita mama mzazi wa marehemu wakamwita wakaongea nae sisi hatukujua waliongea nini baada ya hapo wakafunga ile injini kubwa na kuiwasha safari ikaanza ikiwa ni usiku sasa. Tulibaki tunawasiliana nao tu na safari haikuwa na tatizo. Kumbe yule jamaa alikuwa anamdai mmoja wa viongozi pesa ya huko nyuma na alikuwa amempa kumtunzia ila aipoona kafariki ye alimpa tu mama yake malipo ya huo mkataba aliokuwa anao marehemu. Inamaana boss alipokuja aliwaambia viongozi wa kambi walipe kila deni la marehemu ndipo marehemu alikubali kwenda kwao
 
Back
Top Bottom