Copy and Paste.
Leo niwashirikishe jambo kuhusu ajali iliyotokea Tanga na kuua watu kumi na saba.
Marehemu aliyekuwa anasafirishwa ni Baba wa miaka 60+, alihamia Dar miaka nane iliyopita akajenga na kufanya biashara zake.
Alipokuwa kijana alioa mwanamke aliyekuwa tayari na mtoto mmoja wa kiume, kwa wakati huo ilikuwa ni aibu sana kuoa mwanamke aliyezaa nyumbani. Sina uhakika kama alipata mtoto mwingine na yule mama ila alimlea kijana aliyemkuta naye kama mwanaye wa kumzaa, akamsomesha hadi akafika chuo kikuu wakiwa Rombo.
Kutokana na upendo kupungua mama hakumheshimu baba tena uzeeni na kijana akaja kujua kumbe yule siyo baba yake wa kumzaa.
Mama akampeleka kijana kwa baba yake akiwa mwaka wa tatu chuo kikuu na kijana akahamia kwa baba yake kiasi kikubwa bila kumuonesha upendo baba mlezi aliyemlea na kumhudumia.
Baada ya kijana kupata kazi alihamia Dar na hakutaka mawasiliano tena na baba yake mlezi, jambo lililomuudhi sana baba yake huyo.
Baada ya mama kuwa haelewani na baba, baba aliamua kuhamia DSM na kuanza maisha upya na pia akamwambia yule kijana kwa sababu hataki kumpa heshima basi afanye maisha yake na kila mtu ashike hamsini zake.
Mzee aliugua na alipokuwa amelazwa Mloganzila kijana akaenda kumuona;
Mzee alikasirika sana na akamwambia alishamueleza kila mtu ajuane na maisha yake mwenyewe.....na pia akamwambia hata akifa asije kumzika maana alikosea na kumsononesha sana.
Kesho yake mzee akafariki; kijana akajiunga na ndugu wengine wa DSM wakapanga na kulazimishia kupeleka msiba na maziko nyumbani Rombo kinyume na matakwa/wosia wa marehemu; wengine walipinga kwa kukubali wito wa marehemu kuzikwa Dar maana hakutaka kuzikwa Rombo.
Safari ililazimishwa, lakini hatima yake ikaishia Korogwe, kwa kila aliyepinga kauli ya marehemu kupoteza uhai pale ajalini. Kijana aliyelelewa na marehemu alikuwa na wanaye wawili wote pia walifariki pale pale.
Sisi tupo level gani ya maamuzi kwenye familia?..... hivyo tusidharau mambo, hasa yale yanayokuwa na sababu na pengine sababu hizo zimefikiwa kwa uchungu mkubwa wa akili na moyo, tena bila madeko....uchungu wenye haki!