Ajali Korogwe: Madaktari walipigiwa simu saa nne usiku wakafika saa kumi na moja

Ajali Korogwe: Madaktari walipigiwa simu saa nne usiku wakafika saa kumi na moja

yaani kusema ukweli, kwa wale waliowahi kuishi nje kidogo, madaktari wa kibongo wanaboa sana. wana kiburi, wapenda rushwa na vinajifanya vitaalaamuuuu wakati kutibu haviwezi. kuna wakati huwa naviangalia naviacha tu. kwamba tusiwaseme ati wanatutibu wakati tunawaona wazi kabisa wanazingua tukiwalinganisha na madoctor wenzao? walevi, malaya na kiufupi hakuna kitu yaani. watz wengi wanapona kwa kudra za Mungu tu ila majority ni incompetent, hawana ari ya kutibu wanafanya tu kwa mshahara. (though sio wote, wapo wale wazoefu wanajitahidi ila majority ni vuruvuru tu). binafsi nikikuta asehemu doctor au polisi anafumuliwa na wenye madaraka, hata huwa siumizi moyo kufikiria. wengi wanastahili.
Bro, wewe si wa kwanza kuishi nje. Sasa sijui wazungumzia nje ipi. Madaktari hawahusiki na tiba ya ajali nje ya hospitali. Huko kuna paramedics, ambao si madaktari. Mna paramedics hapa bongo?
 
Mkoa, Wilaya na Hospital hawana mpango maalum wa kushughulika na dharura/Emergency Operations Plan?
Na kuna wagonjwa walihitaji referral muda ule mtoa referral hayupo ilibidi dc asaini referral na kulihitajika vitu vingi vitatuliwe kiutawala
 
Bavicha mbona mna ututusa mwingi

Umeambiwa madaktari hawakuwepo hospital ingawa walipigiwa Simu kwamba kuna wahanga wa ajali wanaletwa

Hai madaktari Wanaishi Kwenye kota za hospital hapo hapo

Ilibidi DC ambaye siyo Daktari kitaaluma atoe referral kwa wale wenye hali Mbaya

Acheni ujinga!
Ww mbona unaongea ujinga, sasa kama huyo Dc sio mtaalam wa afya hiyo referral form kaandika kitu Gani?

Acheni kuingiza siasa kwenye taaluma za watu hilo ni jukumu la zimamoto na vikosi vya ulinzi kazi ya ma Dr ni kuwasubiri hao wagonjwa hospitali wawatie huduma.
 
Hivi kwani Zimamoto kama jeshi la uokoaji kazi yao ni ipi.?..Nafikiri sasa Tuamke Tuanzishe vitengo kama Paramedic kwenye Jeshi letu ili tuepuke kusingizia watu mambo yasiyowahusu.Kwa maana sioni haja ya Kumlaumu DMO kutofika eneo la tukio kwani Miongozo yake haimruhusu kutuma kikosi cha mdaktari kutibia nje ya Hospitali.. hii sasa inayofanywa ni siasa baada ya kuona Mapungufu na wananchi kulalamika
Issue haikua suala la wao "madaktari" kufika eneo la tukio, la hasha! Issue ilikua mwitikio wa hao "madaktari" kufika hospitalini kwa wakati.

Kwa maelezo ya mkuu wa mkoa, licha ya kwamba mmoja wa hao madaktari kuishi karibu/jiranibna hospitali, kila alipokua akipigiwa simu na mkuu wa wilaya alikua akijibu kuwa anayo taarifa ya ajali hiyo na ameipata mapema.

Mkuu wa mkoa ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa, kuchelewa kufulika kwao hospitali ilipelekea mpaka rufaa kwa wagonjwa kutolewa kwa amri na utashi wa mkuu wa wilaya, kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa kitabibu.

Misingi na sababu za kusimamishwa ipo hapo.
 
Na kuna wagonjwa walihitaji referral muda ule mtoa referral hayupo ilibidi dc asaini referral na kulihitajika vitu vingi vitatuliwe kiutawala
Kwa hiyo DC ndio aliandika referral? Mbona nyie wabongo wapuuzi puuzi tu. Mnadanganyika danganyika tu na wanasiasa. Nani aliandika referral letter ambayo DC aka sign? Au iliandikwa na DC? Unadhani referral letter ni barua ya mapenzi?
 
Popote walipoitwa, Je Mkoa, Wilaya na Hospitali zilikuwa na Emergency Operation Plan na ilifuatwa??
Sijui ni mimi ndio nimeielewa hii habari vibaya au kuna watu wana matatizo ya akili

Nahisi nimemsikia RC anadai Doctors waliitwa Hospital sio eneo la accident
 
Ni upuuzi tu !! Kwani masaa ya kazi hayajulikani? Hata uwapigie simu siyo lazima waje muda huo, kwani hawana shughuli nyingine waliyokuwa wanafanya? Eti asingekuwa Magufuli wasingefanya hivyo? UJINGA MTUPU.

Mbona yeye mwenyewe KAFA akiwa Rais? Kwa nini watu hawakumuogopa kuwa atakufa.
Hivi ndugu umelewa? Hujui kama madaktari wana zamu hadi ya usiku, wanapokezana mahospitali
 
Sijui ni mimi ndio nimeielewa hii habari vibaya au kuna watu wana matatizo ya akili

Nahisi nimemsikia RC anadai Doctors waliitwa Hospital sio eneo la accident
Ni kweli ndicho alichomaanisha mkuu wa mkoa, sio jukumu la daktari kufika eneo la ajali, hilo ni jukumu la jeshi la zimamoto na uokoaji, daktari anasubiri hospitali ndipo penye dawa na vifaatiba.
 
Kwa hiyo DC ndio aliandika referral? Mbona nyie wabongo wapuuzi puuzi tu. Mnadanganyika danganyika tu na wanasiasa. Nani aliandika referral letter ambayo DC aka sign? Au iliandikwa na DC? Unadhani referral letter ni barua ya mapenzi?
Ndio ilikuwa hivyo kumbuka DC ni kila kitu kwenye wilaya
 
Kwa hiyo DC ndio aliandika referral? Mbona nyie wabongo wapuuzi puuzi tu. Mnadanganyika danganyika tu na wanasiasa. Nani aliandika referral letter ambayo DC aka sign? Au iliandikwa na DC? Unadhani referral letter ni barua ya mapenzi?
Mkuu, ni kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa mkoa, na akasema kuwa jambo limefanyika na ni kinyume na taratubu za kitabibu, linefanyika kwa utashi wa mkuu wa wilaya kwa kuwa tu mtu wa kulitekeleza hilo kwa utaratibu hakuwepo eneo husika.

Sasa kaandika kwa namna gani au kwa lugha ipi wanajua wao.
 
Suala la utu haliwezi kulazimishwa ni hisani tu, hao madaktari hawapaswi kusimamishwa sasa kama lingekuwa suala la utu tu na sio sehemu ya majukumu yao ya msingi.
Emergency ni suala la utu kila mtu anatakiwa awajibike kwa nafasi yake
 
Back
Top Bottom