Ajali Korogwe: Madaktari walipigiwa simu saa nne usiku wakafika saa kumi na moja

Bro, wewe si wa kwanza kuishi nje. Sasa sijui wazungumzia nje ipi. Madaktari hawahusiki na tiba ya ajali nje ya hospitali. Huko kuna paramedics, ambao si madaktari. Mna paramedics hapa bongo?
 
Mkoa, Wilaya na Hospital hawana mpango maalum wa kushughulika na dharura/Emergency Operations Plan?
Na kuna wagonjwa walihitaji referral muda ule mtoa referral hayupo ilibidi dc asaini referral na kulihitajika vitu vingi vitatuliwe kiutawala
 
Ww mbona unaongea ujinga, sasa kama huyo Dc sio mtaalam wa afya hiyo referral form kaandika kitu Gani?

Acheni kuingiza siasa kwenye taaluma za watu hilo ni jukumu la zimamoto na vikosi vya ulinzi kazi ya ma Dr ni kuwasubiri hao wagonjwa hospitali wawatie huduma.
 
Issue haikua suala la wao "madaktari" kufika eneo la tukio, la hasha! Issue ilikua mwitikio wa hao "madaktari" kufika hospitalini kwa wakati.

Kwa maelezo ya mkuu wa mkoa, licha ya kwamba mmoja wa hao madaktari kuishi karibu/jiranibna hospitali, kila alipokua akipigiwa simu na mkuu wa wilaya alikua akijibu kuwa anayo taarifa ya ajali hiyo na ameipata mapema.

Mkuu wa mkoa ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa, kuchelewa kufulika kwao hospitali ilipelekea mpaka rufaa kwa wagonjwa kutolewa kwa amri na utashi wa mkuu wa wilaya, kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa kitabibu.

Misingi na sababu za kusimamishwa ipo hapo.
 
Na kuna wagonjwa walihitaji referral muda ule mtoa referral hayupo ilibidi dc asaini referral na kulihitajika vitu vingi vitatuliwe kiutawala
Kwa hiyo DC ndio aliandika referral? Mbona nyie wabongo wapuuzi puuzi tu. Mnadanganyika danganyika tu na wanasiasa. Nani aliandika referral letter ambayo DC aka sign? Au iliandikwa na DC? Unadhani referral letter ni barua ya mapenzi?
 
Popote walipoitwa, Je Mkoa, Wilaya na Hospitali zilikuwa na Emergency Operation Plan na ilifuatwa??
Sijui ni mimi ndio nimeielewa hii habari vibaya au kuna watu wana matatizo ya akili

Nahisi nimemsikia RC anadai Doctors waliitwa Hospital sio eneo la accident
 
Hivi ndugu umelewa? Hujui kama madaktari wana zamu hadi ya usiku, wanapokezana mahospitali
 
Sijui ni mimi ndio nimeielewa hii habari vibaya au kuna watu wana matatizo ya akili

Nahisi nimemsikia RC anadai Doctors waliitwa Hospital sio eneo la accident
Ni kweli ndicho alichomaanisha mkuu wa mkoa, sio jukumu la daktari kufika eneo la ajali, hilo ni jukumu la jeshi la zimamoto na uokoaji, daktari anasubiri hospitali ndipo penye dawa na vifaatiba.
 
Kwa hiyo DC ndio aliandika referral? Mbona nyie wabongo wapuuzi puuzi tu. Mnadanganyika danganyika tu na wanasiasa. Nani aliandika referral letter ambayo DC aka sign? Au iliandikwa na DC? Unadhani referral letter ni barua ya mapenzi?
Ndio ilikuwa hivyo kumbuka DC ni kila kitu kwenye wilaya
 
Kwa hiyo DC ndio aliandika referral? Mbona nyie wabongo wapuuzi puuzi tu. Mnadanganyika danganyika tu na wanasiasa. Nani aliandika referral letter ambayo DC aka sign? Au iliandikwa na DC? Unadhani referral letter ni barua ya mapenzi?
Mkuu, ni kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa mkoa, na akasema kuwa jambo limefanyika na ni kinyume na taratubu za kitabibu, linefanyika kwa utashi wa mkuu wa wilaya kwa kuwa tu mtu wa kulitekeleza hilo kwa utaratibu hakuwepo eneo husika.

Sasa kaandika kwa namna gani au kwa lugha ipi wanajua wao.
 
Suala la utu haliwezi kulazimishwa ni hisani tu, hao madaktari hawapaswi kusimamishwa sasa kama lingekuwa suala la utu tu na sio sehemu ya majukumu yao ya msingi.
Emergency ni suala la utu kila mtu anatakiwa awajibike kwa nafasi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…