Ajali mbaya Dar yachukua uhai wa Kelvin Kavishe (Kaloosh)

Hivi ni rich kids au utajiri wa washua wao coz wale wanaosaka wenyewe hawakatiki namna hyo, RIP dogo
Ni za kwao tu, hata ww unatafuta kwa ajili ya wanao.
Sema sasa sifa ndio zinawamaliza na kale kamsemo kao "Nakula bata"
 
Huyu demu kumbe nae ni mshamba eeh? mtu mwenye majonzi anapata wapi nguvu ya kushika simu na kujipiga selfie na kujipost instagram na kuandika caption? nimemtoa akili kweli huyu mpuuzi.
 
kiruuuu
 
Lile eneo kutoka Stanbic mpaka njia ya kuingia Leaders litakuwa na tatizo, ajali nyingi za pale ni za usiku na lazima mtu afe
Ahaaa we jamaa kiboko lazima uunganishe na yale mambo anyway eneo lingine ni ile barabara yakuelekea maisha club ya zamani
 
Oook......RIP kijana.........lakini nataka nijue......alikuwa milionea.....?........
Yaani shosta una maswali!😉 Hakuwa milionea; Ni kijana wa mjini ambae alikuwa karibu sana na ma-so called Bongo Celebrities; hapa naongelea "Lulu", Jack Wolper, Jux...to name a few! . Kijana mdogo sana, Apumzike kwa Amani
 
R.I.P kijana inasikitisha sana kifo cha ghafla.
naomba kuuliza tu alikuwa ni nani hapa mujini? bilionea au milionea?

kila wakati tunapoamka/kulala tusisahau kuomba sala ya Kifo Chema
 
Jamani mwendokasi haui mtu kinachoua mtu ni kitu kingine kabisa
R.I.P
 
Inaonekana marehemu (apumzike kwa amani) alikuwa ana uwezo wa kuingia bar akanunua bia za laki tatu ndo akawa celeb wa eneo lake la kujidai.

Nchi kubwa hii jamani. Kuna watu tunaishi huku Kilindoni, Mafia.
Ha ha haaa hata hapo Kilindoni kuna wengine ni maceleb wa Mapozi na wengine kwa Thadei!!
 
Mbona huyo manusura, anapiga selfie na ndugu zake halafu wanacheka! Au wamemtoa kafara...!
 
R.I.P kijana inasikitisha sana kifo cha ghafla.
naomba kuuliza tu alikuwa ni nani hapa mujini? bilionea au milionea?

kila wakati tunapoamka/kulala tusisahau kuomba sala ya Kifo Chema
kashesho huyu kafa wala hajui hata uchungu wa mauti na kukata roho hakuuhisi
 

Ubalozi wa Kenya upo Maeneo ya wapi? mshana jr
 
Yaani shosta una maswali!😉 Hakuwa milionea; Ni kijana wa mjini ambae alikuwa karibu sana na ma-so called Bongo Celebrities; hapa naongelea "Lulu", Jack Wolper, Jux...to name a few! . Kijana mdogo sana, Apumzike kwa Amani

Ooh, very fresh meat......RIP
 
Apumzike kwa amani kijana maarufu. Nawashauri vijana wengine maarufu au bata boys watoe ajira kwa ma babu dere, kwani wengi wao hapa town ni waendesha magari tu sio madereva.Mtu anaendesha gari uku ana selfika ili awahi kupost insta.
 
Nani aliyetoa taarifa kwamba marehemu alikuwa anaendesha gari akiwa amelewa?
Tatizo la watu wengi wanpenda sana kuhukumu wenzao kwa makosa ambayo hata wao wanafanya
Alikuwa na demu wake saa kumi usiku wakitoka rhapsody..walikuwa na wenzao wameongozana na ndio hao walompeleka hospital akiwa maiti na wote walikua chakali .. ...sema jingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…