TANZIA Ajali Mbeya: Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamefariki dunia

pole kwa ndg jamaa na marafiki.
 
Na kale kamteremko ka Inyala kamenyooka kweli kweli kutoka pale kwenye Rail.
 
Kwanini serikali ya CCM haitaki kutanua barabara maeneo hatarishi mkoani Mbeya?

Ajali isipotokea Inyala, inatokea Mlima Nyoka, isipotokea hapo inatokea mteremko wa Mbalizi, lakini serikali inachukulia poa tu miaka nenda rudi.
Mkuu nilikuwa najiuliza kwanii serikali iko kimya juu ya maeneo hatarishi!

Kila siku ajali zinatokea maeneo yale yale, Je kamatai ya Taifa ya usalama barabarani hawaoni hili.

Kitu kingine ambacho ni mzizi hasa kwa Dar es Salaam, Je wameshindwa kubuni njia ya kupunguza ajali hasa maeneo ya mataa yanapokuwa yamezima mfano.
Barabara ya morogoro road maeneo ya taa za Bucha, Baruti Suka ni maeneo ambayo hazipitu siku mbili bila mtu kugongwa au magari kugongana!

Tunahitaji kuja na suluhisho la kudumu kwa maeneo haya, watu tunateketea kila uchwao.

Vyuo kama DIT, St joseph, CoET, MUST, Arusha Tech, VETA mko wapi kuja na suluhisho la taa zinazo dumu!
 
1 na 2 ni kwa kiasi kidogo sanaaa, 3 ndo baba lao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…