Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania


umenena vema mkuu
 
sijui kama wamekusikia maana wenyewe mawazo yao yapo kwenye uchaguzi tu hata hivo watakwambia kuwa gharama saana wakati huo huo mtu ana mabilioni kaficha uswisi
 
Nakumbuka Bwana Yesu msalabani akisema, "ee Baba uwasemehe kwa kuwa hawajui watendalo."Mimi nasema ee Baba uwasemehe kwa kuwa hawajui chanzo cha ajali."Let me say this,as long as we pretend we know the cause of accidents,they will continue to kill our brothers and sisters.Ajali zinazotokea are spiritial,and unless we are spiritial we will never,I repeat never, be able to contain them.You can suggest a million solutions as a means of tackling the problem,but if sense does not prevail and the nation continues to be satanic,accidents will infact increase,
 
Ajali nyingi ni Bangi na ulevi tu, hata tukiendesha ndege angani kwa uendeshaji huu tunaouona barabarani NA HASA MADREVA WA MABASI YA MIKOANI, AJALI HAZITAISHA. Napendekeza serikali ianze kuwa na MAANDALIZI MAALUMU TANGU MWANZO KWA MADREVA WA MABASI (SPECIAL TRAINING) na kila mmiliki wa basi aajili kutoka hii pool.
 

Chadema hawataki hilo
 
Naumia sana kuona kilasiku Alish_Ajali anavyoua tz.Tujiulize tu,kwanini sana kipindi hiki cha uchaguzi?kama wanasiasa wanapishana kwa sangoma tutegemee nini?Hakuna kitu gari kugongana uso kwa uso,haya ni mazingaombwe tu.Mnadhani madereva wanatamani kufa?Tanzania tumrudie Mungu.Wapo wengi wanadiriki kusema hakuna Mungu,watania wenzangu tutubu.Nchi inaongozwa na Nguvu zingine jamani.
 
Nawakilisha ni mawazo yangu
Me kama mwananchi wa kawaida kabisa napenda nitoe mapendekezo nini cha kufanya dhidi ya hizi ajali barabarani zinazozidi kuua mamia na kuwatia uvilema maelfu ya watanzania

1.Serikali inapaswa kusitisha utoaji wa leseni hasa vyombo vya moto vinavyobeba abilia na malori makubwa

2.Kupitia na kuhakiki madereva wote wa malori na mabusi

3.Kuamuru madereva wote warudi kusoma na kupata vyeti na hati mpya za defensive driving

4.Kufuta license za mabasi yote hasa yenye namba kuanzia A pamoja na B kubeba abiria na hata malori ya mizigo pia

5.Serikali kupitia Tanroad kuziba mashino yote yakiyopo hasa hizi main road kuepusha ajari zisizo za lazima

6.Serikali kupitia Jeshi la Polisi kuanza kuwateua hasa trained trafic polisi kusimamia na kutekeleza usalama bara barabi wengine ni hovyo kabisa hawafai (Siku hizi tochi nyingi ajali kibaoooo)

7.Kuandaa sheria mahususi hasa kwa wale wanaoleta ajari kwa makusudi

8.Kiandaliwe chombo maalamu/Taasisi itakayohusika na kusimamia utekelezaji wa hizo sheria

9.Ukarabati wa Reli za kati hasa za mizigo ili kuwe na maandalizi ya kuyapiga marufuku malori yote nchini yawepo lkn kwa vibali maalum sio kama njugu tu


Wenu mwana JF
 
Nakubaliana na hoja.

Hivi serikali imeshindwa kabisa kutoa tamko lolote kuhusiana na wimbi la ajali?

Unataka kuniambia mpaka kufikia hivi sasa serikali imeshindwa kabisa kufanya mikakati yoyote kuhusiana na ajali?

Kama ni muda sio kweli, wimbi la ajali halikuanza jana wala juzi.

Serikali tunaomba mtusikilize kilio chetu karibu kila siku inayoenda tunapoteza ndugu, jamaa, marafiki, tuwapendao na orodha bado ndefu inaendelea ....
 
Mimi pendekezo langu ni moja tu, imetosha kuelekeza nguvu kwnye vifaa (magari). Nadhan ni muafaka kuelekeza nguvu kwa wanaoendesha hivy vifaa sasa. Process ya kuwapata madereva wa mabasi ni lazima iwe thorough...
 
haitasaidia kitu njia rahisi ni kudhibiti mwendo wa mabasi kwa kuyapangia muda maalum wa kufika katika vituo husika
 
haitasaidia kitu njia rahisi ni kudhibiti mwendo wa mabasi kwa kuyapangia muda maalum wa kufika katika vituo husika
Bado haitosaidia mwanzoni walisema safari za usiku zinasababisha ajali wakaziondoa, wakaja na vifaa vya kudhibiti mwendo navyo sijui viliishia wapi!

Kwahiyo hata ukiwapangia muda watakuwa wanakamua kama kawaida wakiona wanakaribia vituoni watakuwa tayari wapoteze muda(kuvuta muda) kuegesha mabasi yao ili wakishawasili vituoni wawe wameenda sawa na muda
 
Ninavyoona kila siku kutakuwa na ajali mpya zenye kuuwa na kuacha vilema watu inasikitisha sana
 
cement

Kwa kuwa humiliki gari ungekuwa na moja ya basi au roli lenye kuanzia A usingethubutu kusema wazuie yasibebee abiria na mizigo. halafu yakishazuiliwa yakafanye kazi gani?
 
Last edited by a moderator:
cement

10. mizimu ya ccm iombwe kafara ziwe za mbuzi na ng'ombe na si binadamu.
 
Last edited by a moderator:
Halafu ukichunguza sana ni haya mabasi ya kichina ndo shida mi nahisi kuna tatizo
 
kwa kuwa humiliki gari ungekuwa na moja ya basi au roli lenye kuanzia A usingethubutu kusema wazuie yasibebee abiria na mizigo. halafu yakishazuiliwa yakafanye kazi gani????

Kaka wanatuchosha sana hawa watu ndugu yangu
 
Idadi ya magari imezidi uwezo wa barabara hivyo kuanzia sasa wapige marufuku kuongeza mabasi au malory na tuondoe magari mabovu njiani.
 
cement

Point namba 1 naikataa kabisa, ni sawa na kuturudisha enzi za ujima, serikali inapaswa kisajiri basi na magari ya mizigo mapya ili kurahisisha usafiri.

Point 2, naikubari hasa malori kampuni zibanwe kuajiri madereva wenye uweledi maana siku hizi kuna madereva wengi wa malori watoto wadogo sana, anakaa kishoto trip mbili congo ya tatu yeye ndie dereva hapa waajiri wanfuata cheep labour maana wanawalipa kidogo wao wanalizika kuendesha Scania 40 ft.

Point 3., siikibali maana mafumzo waliopata hawali somo hilo lilikuemo, sasa kama hatuamini elimu waliopata nashauri walimu wao kwanza ndio wakasome upya kisha ndio wafuate madereva.

Point 4 siikubali kabisa maana namba ya gari hai determine ubora wa gari inaweza kua namba D na gari likawa ovyo kabisa A ikawa bora kabisa mfano chukua basi ya dar express Benz yenye namba A Linganisha na Yutong yoyote ya namba B Au C ya mwanzo. Au naweza tu nikaimpot basi bovu tu toka kenya nikapata na D napata leseni.

Mimi nashauri serikali inunue mtambo ya kukagua ubora wa magari no questions. Pia watu tunaisahau sana tbs kwenye hilo sakata inahusika sana maana Vipiri vingi vinavyouzwa Tz ni feki tbs wamelala tu.

Point 5 niongezee, watanue barabara hasa climbing lanes maeneo ya milima, au kona kali.

Point 7 naongezea kama tunahitaji mabasi yatembee mwisho speed 80 basi serikali itunge sheria ambayo itaruhusu kusajiri mabasi yenye speed mwisho 80,hivyo watengenezaji watatengeneza mabasi ambayo speed max ni 80 na siyo shortcut ya kufunga speed gavana.

Point nyingine nazikubali at least 99%
.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…