Kwa wale wote wanaosafiri safari ndefu siku ya leo kutoka mkoa mmoja hadi mwingine kwa njia ya barabara watakuwa wameshuhudia mabadiliko makubwa ya mwendo wa mabasi wanayosafiria hii ni kutokana na kumwagwa kwa askari wa usalama barabarani wa "kutosha" kila kona.
Nadhani operation hii inafuatia ajali zilizoondoka na roho za watanzania mfululizo hivi majuzi.
Nachukua fursa hii kulipongeza jeshi la polisi kuchukua uamuzi huu mzuri japokuwa "its too late" walipaswa kufanya operation hiyo toka miaka 50 iliyopita.
Nashauri operation hii ifanyike katika idara zote zitoazo huduma kwa jamii ili haki itendeke kwa kila mtanzania. Operation hiyo iwaguse mahakimu wanaopindisha sheria, iwaguse madaktari na manesi wanaobagua wagonjwa kwa kutaka rushwa, iwaguse Uhamiaji wanaozungusha raia wema wanapoomba passport, iwaguse mawaziri, makatibu wakuu, makamishna wanaoingia mikataba ya kifisadi na imguse kila azuiae haki ya mtu mwingine kwa maslahi yake binafsi.