Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

mimi naona ni bora wangetumia askari wa barabarani katika safari za mikoani ingepunguza ajali.
 
hizo 90 za serikali bado zako unazopokea nyuma ya gari....ah ah umetisha mkuu

ndio tatizo la mijitu mijinga michache. Ukielezea kitu unachokijua basi unaonekana ww ndiyo unafanya.
Mm sio traffic pumbu ww ila najua kichofanyika
 
polisi wenyewe wanaendesha gari ovyo na wao ndiyo wavunja sheria # 1...!
 
sawa mkuu.Nazani ktk jeshi hilo wapo sana madereva hivyo basi waajiriwe na makampuni hayo ya mabasi tena posho lukuki na mishahara.
 
inamaana wakikubaliana hawa madereva wa sasa watakuwa makonda,maonda watakuwa wapiga debe na waiga debe watakuwa vibaka.
 
Kwa wale wote wanaosafiri safari ndefu siku ya leo kutoka mkoa mmoja hadi mwingine kwa njia ya barabara watakuwa wameshuhudia mabadiliko makubwa ya mwendo wa mabasi wanayosafiria hii ni kutokana na kumwagwa kwa askari wa usalama barabarani wa "kutosha" kila kona.

Nadhani operation hii inafuatia ajali zilizoondoka na roho za watanzania mfululizo hivi majuzi.

Nachukua fursa hii kulipongeza jeshi la polisi kuchukua uamuzi huu mzuri japokuwa "its too late" walipaswa kufanya operation hiyo toka miaka 50 iliyopita.

Nashauri operation hii ifanyike katika idara zote zitoazo huduma kwa jamii ili haki itendeke kwa kila mtanzania. Operation hiyo iwaguse mahakimu wanaopindisha sheria, iwaguse madaktari na manesi wanaobagua wagonjwa kwa kutaka rushwa, iwaguse Uhamiaji wanaozungusha raia wema wanapoomba passport, iwaguse mawaziri, makatibu wakuu, makamishna wanaoingia mikataba ya kifisadi na imguse kila azuiae haki ya mtu mwingine kwa maslahi yake binafsi.
 
Isijekuwa ni nguvu za soda tuu,maana Tanzania tumea Advance kwa Kufanya kitu pale Matukio yanapotokea..
 
Wadau.
Hapo hata madereva wakilipwa mshahara kwa mwezi 5mil marupurupu kila route 1mil haitasaidia kitu!!, kitu kingine kwa sasa dereva wa basi la abilia kama hana cheti (siyo leseni) kutoka Taasisi ya Taifa ya Usafirishaji au NIT awezi pewa basi la abilia kwa mmiliki mwenye nidhamu, ila kuna kampuni zinachukua experience drivers na ambao wengi wao wanafahamika kwa utovu wa nidhamu barabarani kwa askari usalama barabarani.
Jambo lingine na ambalo linaweza kuwa msaada kwa usalama wa abilia na mabasi yenyewe ni kuepuka tabia ya kuwahi kufika sehemu wanapokwenda kuanzia kwa wamiliki kuacha tabia ya kuwapa madereva vichwa na kuwalipia faini pindi wanaposhikwa na kuwekwa ndani kwa kuwahi sehemu eti madai basi hilo injini yake kubwa au ni jipya, hapo pia kuna abilia wanakuwa tayari kulipa faini za njiani ili kuwahi kufika wakijifanya wana hela kwa kuwa ni wafanyabiashara!!
NAKUMBUKA.
Kampuni ya mabasi scandinavia walikuwa kabla ya dereva kupewa basi lazima akae week kadhaa akifanya shanting kupeleka mabasi ggarage na kuyaleta terminal, lakini pia walikuwa na walimu wao hata kabla ya kupewa basi kwenda safari unapewa elimu/nidhamu lakini pia siku ya safari yako ya kwanza unakuwa na mtu anayekuangalia uendeshaji wako na jinsi unavyofanya. (uhusiano wako na abilia)
Hii iliwanya scandinavia kuwa na madereva wanaofahamika kwa abilia na hata abilia wenyewe kufahamiana nao na kuwatafuta kujua wapo wapi ili kuwezq kufanya nao safari.
Mwisho:
Najaribu kuona gharama za vyuo vya udereva wa mabasi kama ingekuwa sawa na vyuo vikuu, ili kupata dereva mwenye wivu na pesa yake alolipia chuo, hii inanipa picha kuwa hata madereva wangekuwa wachache na kuweza kujivuna.
Cha kuchekesha ni hiki kazi hii inaonekana ni ya watu wasio na elimu na walio kosa kazi za maana (ambapo si kweli) japo usishangae hata sasa kuna maderva wasiojua kuandika wala kusoma karne hii!!.
UNATARAJIA NINI HAPO?

Nawasilisha.
 
Tatizo la Tz vibarabara ni vyembamba sana, inakua madereva wanapata wakati mgumu kuongoza magari wanapokua njiani

Jengne la msingi wakati gari inapopata ajali kampuni iwajibike kwa kuwalipa wahanga wote thamani kubwa ambayo kampuni na dreva watakua makini kwa kuogopa na kuepusha harama hizo
 
Khaa!!™® Nadhani jambo la maana ni kupunguza msongamano kwa mabasi ya abiria. Njia mbadala kama treni za kasi, ndege na meli xa kasi ziimarishwe na kufanywa rahisi ili kila. Mmoja azitumie. Barabara tuache kwa mabasi machache na magari binafsi. Kiasi kikubwa cha abiria na mizigo isitumie barabara
Hapo hata mm nakukubali
ila ni vigumu kudhibiti mwendo kasi kwani haya mabasi yanapenda kushindana na kuwawahisha abiria
MY TAKE
FBY 2013
Serikali IJENGE BARABARA 2 (tWO WAY) hii itapunguza kugongana uso kwa uso lakini kuanguaka na kuacha njia bado kutakuwepo
kuliko kujenga Vyuo vya udereva wa magari ya Abiria tu ni gharama

Kuna siku nilitunia gari ndogo nilinusurika kwa fujo za mabasi kwani hawatumii Sheria kabisa katuka kuOvertake au kupishana wao ni mradi wawahi huko waendako
 
Wandugu habari.

Tangu mfuulizo wa tafakari za ajali barabani uwepo.

Madereva wengi wasio na sifa hupewa magari ili wawalipe Mshahara kidogo,mwenye cheti cha NIT Na uzoefu wanachwa,kisa watahitaji hela ndefu,tusikubali wananchi leo mimi, kesho huenda akafa ndugu yako au hata wewe.

Tuhakikishe kwa kila namna madereva wasio na sifa hawapaiti nafasi ya kutuua.
 
Kwani sumatra ndo wanaajiri madreva wa magari ya abiria siku hizi?
 
Wakuu ni wazo tu,

Kwamba ili kupunguza ajali ambazo zimepoteza maisha ya ndugu zetu wengi.

Haya mabasi yaendayo mikoani yawe na polisi hata mmoja kwa kila basi,kwa mfano safari kutoka Dar kwenda Arusha polisi anaweza akashuka Tanga kupokezana na mwingine na akarudi na lingine kuelekea Dar.

Kuwe na utaratibu basi linapoondoka abiria kuhakikisha kuwepo na polisi na kuangalia vitambulisho vyake,haya yote ili kupunguza ajali,atakuwa anajua gari linaendaje.

Haya ni maoni yangu tu mwenye maoni tofauti atoe ili kupunguza ajali za barabarani.
 
Unataka nchi iwe ya mapolisi tupu? Utaajiri Police wangapi wataokuwa wanasafiri kilasiku aise?
 
Unataka nchi iwe ya mapolisi tupu? Utaajiri Police wangapi wataokuwa wanasafiri kilasiku aise?
Mkuu wahusika wenye mabasi waamrishwe kila basi kwa safari moja iwe inamlipia polisi,au polisi aongezewe mshahara kwa hiyo kazi,kutakuwa na umuhimu zaidi,maana hata gari ikiiendeshwa kwa kasi abiria wanaweza kumcontrol polisi,kuliko dereva na konda kujiamulia
 
Back
Top Bottom