Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hizo 90 za serikali bado zako unazopokea nyuma ya gari....ah ah umetisha mkuu
Kwa wale wote wanaosafiri safari ndefu siku ya leo kutoka mkoa mmoja hadi mwingine kwa njia ya barabara watakuwa wameshuhudia mabadiliko makubwa ya mwendo wa mabasi wanayosafiria hii ni kutokana na kumwagwa kwa askari wa usalama barabarani wa "kutosha" kila kona.
Nadhani operation hii inafuatia ajali zilizoondoka na roho za watanzania mfululizo hivi majuzi.
Nachukua fursa hii kulipongeza jeshi la polisi kuchukua uamuzi huu mzuri japokuwa "its too late" walipaswa kufanya operation hiyo toka miaka 50 iliyopita.
Nashauri operation hii ifanyike katika idara zote zitoazo huduma kwa jamii ili haki itendeke kwa kila mtanzania. Operation hiyo iwaguse mahakimu wanaopindisha sheria, iwaguse madaktari na manesi wanaobagua wagonjwa kwa kutaka rushwa, iwaguse Uhamiaji wanaozungusha raia wema wanapoomba passport, iwaguse mawaziri, makatibu wakuu, makamishna wanaoingia mikataba ya kifisadi na imguse kila azuiae haki ya mtu mwingine kwa maslahi yake binafsi.
Hapo hata mm nakukubaliKhaa!!® Nadhani jambo la maana ni kupunguza msongamano kwa mabasi ya abiria. Njia mbadala kama treni za kasi, ndege na meli xa kasi ziimarishwe na kufanywa rahisi ili kila. Mmoja azitumie. Barabara tuache kwa mabasi machache na magari binafsi. Kiasi kikubwa cha abiria na mizigo isitumie barabara
Mkuu wahusika wenye mabasi waamrishwe kila basi kwa safari moja iwe inamlipia polisi,au polisi aongezewe mshahara kwa hiyo kazi,kutakuwa na umuhimu zaidi,maana hata gari ikiiendeshwa kwa kasi abiria wanaweza kumcontrol polisi,kuliko dereva na konda kujiamuliaUnataka nchi iwe ya mapolisi tupu? Utaajiri Police wangapi wataokuwa wanasafiri kilasiku aise?