Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

dawa ya hizi ajali ni moja tu,tutembee kwa miguu...
 
Sijali matumizi yako mabovu ya R ila naomba kujua uhusiano ya wote uliowataja na ajali za barabarani!
Na nataka kujua kifungu cha sheria ulichorefer ili faini ya dereva aliyehusika kwenye ajali iwe bilioni 10 na ningependa kujua namna ya utekelezaji wa malipo husika ikiwa mtuhumiwa atakuwa amefariki kwenye ajali!

soma vizuri ;;soma namba 2
 
Jawabu ni Smart phone

Huawei Ascend Y530,download application iitwayo "My tracks"- controller akae siti yoyote ya BASI,safari ianze.
Speed,umbali, vyoote vitaonyeshwa na muda uliotumika kituo hadi kituo!

Mahitaji:-
1)smartphone kama iliyotajwa hapo juu au iliyo bora zaidi.

2)mtu(operator) wa simu hiyo
3)power bank(chargers)

4)My track(application) haihitaji mtandao wa simu ila smartphone iwe na line ya sim(sim card)


Utaratibu

Smartphone ikaguliwe na RTO au wakala wake!
Dereva asini kuwa smartphone yenye IMME 12345678... Ndiyo itakayo record mwendo wa basi lake kwa siku hiyo!

Kama una mawazo bora zaidi changia
 
Kwani ni Ajali zote huwa zinasababishwa na mwendokasi?? Vipi kuhusu umakini wa dereva barabarani??

Ku-overtake kwenye kona au mlima, ku-overtake magari zaidi ya mawili kwa mpigo tena yote yakiwa kwenye mwendokasi, service za mabasi yenyewe lakini pia wakati mwingine ni uzembe tu wa madereva wengine kwa mfano ile ajali iliyosababishwa na Passo hivi majuzi..
 
we ropoka tu ,hivi unadhani hizi barabara zina ubora kiasi gani?
 
Mm naona ajari ikitokea dereva na kondakta wauwawe. Atleast wauwawe wachache, kuliko mamia ndani ya mwezi.

Hii njia ilisaidia sana zamani kwa upande wa ajari na wizi ila baada ya siasa na haki za binadamu kuzidi mambo yamekuwa mabaya zaidi!
 
Umekerupuka, only in Tanzania kila mtu ni mtaalamu, sasa mmiliki wa gari anahusikaje na ajari....ajari ya majinja iliyo sababishwa na shimo barabarani anafungwa nani na fain analipa nani? Ajali ikisababishwa na tair kupasuka au matatizo ya kiufundi kama brek, tair road end n.k nani atafungwa, au kulipa hiyo fine?
 
Issue hapa sio barabara mkuu soma vizuri hoja za mleta mada
tunaliangalia suala kimapana zaidi outside the box ,inawezekana ajali hizi hata traffic wala hao munaowataja hawahusiki,kama una uzoefu wa kuendesha magari mikoani utakubaliana na mimi
 
hahahaha mkuu la ajari zinazosababishwa navufinyu wa miundo mbinu je??
hapo nani atatakiwa kulimwa faini??

mfano ile ajari ya basi na semi iliyosababishwa na kuwepo na tuta barabarani hapo ni nani tumfunge??

mkuu ukiangalia asilimia 90 ya ajari zetu nyingi husababishwa na ubovu wa miundo mbinu mfano ufinyu wa barabara.je hapo nani wakulaumiwa??
 
Kwani ni Ajali zote huwa zinasababishwa na mwendokasi?? Vipi kuhusu umakini wa dereva barabarani??

Ku-overtake kwenye kona au mlima, ku-overtake magari zaidi ya mawili kwa mpigo tena yote yakiwa kwenye mwendokasi, service za mabasi yenyewe lakini pia wakati mwingine ni uzembe tu wa madereva wengine kwa mfano ile ajali iliyosababishwa na Passo hivi majuzi..

mimi nimezungumzia mwendo kasi na jinsi ya kuuthibitisha, yapo mengi,endelea kuchangia
 
Back
Top Bottom