Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

soma vizuri thread,
kinachozunguzwa ni jinsi ya kupata takwimu za mwendo wa gari(basi),suala la takwimu hizo zitafanyiwa kazi vipi,"is another square"

Mkuu na sisi tunaofanya jogging unaweza itumia kufuatilia mwendo? Kama inawezekana unaitumiaje?
 
''Kutokana na ajali za barabarani ambazo watalawa kama vile wameshindwa kusimamia au kuchukua hatua za dharura kunusuru maisha ya watu ambayo yanapotea kila siku; Ningekuwa kiongozi ningesema haya yafuatayo:

''Sitaki kusikia ajali zinatokea, hivyo basi kamanda wa usalaama barabani wa eneo usika (eneo la ajali), mkuu wa wilaya wa eneo n.k , barua zao ziko tayari kufukuzwa kazi kama hayo yatatokea katika eneo lao ikiambatana na kutunga sheria ya kufungwa kwa miaka 3 jela kushindwa kuweka mikakati ya kuzuia ajali''

MATOKEO:Wakuu hao wataweka mitakati ya kudhibiti ajari, hutasikia ajari za hovyo ovyo.

2.Kama wauzaji wa madawa ya kuleya wamewekewa sheria kali,kwa nini madereva na wamiliki wa kampuni ya usafirishaji yasiwekewe sheria kali.

Mfano🙁a)ikithibitika ni uzembe wa dereva;Dereva akisababisha ajari atalipa fidia ya sh TZS 10 billion Na kifungo cha maisha jela
(b) Wamiliki wa mabasi hayo pia watalipa fidia ya TZS 10 billion na kufungiwa kufanya shughuli za usafirishaji kwa miaka isiopungua 5

3.Serikali kufuta vyuo vya mitaani ambavyo havina sifa za kufundisha udereva.

Je kama haya yakisimamiwa kutakuwa na ajari barabari

WADAU TUJADILI
Hili ndilo tatizo letu na umeandika sawa kabisa na maamuzi mengi ambayo hufanyika nchini. Kwanza hakuna mtu anayejua hizi ajali zinasababishwa na nini? tunakisia tu kuwa sababu ni madereva wabaya lakini hakuna uchunguzi ulofanyika kwa kila ajali.

Nimesoma habari nyingi sikuona mahojiano ya dereva ama abiria juu ya chanzo ama sababu na imekuwa kama vile kitu sintojua sababu. Yawezekana kabisa kuwa magari yenyewe yamechakaa na hayafanyiwi ukarabati kabla ya safari, hivyo kukatika kwa chombo chochote ikawa sababu. Inawezekana sababu ni barabara zetu. Highway haiwezi kuwa ni barabara inayopitwa na watu wa baiskeli, wakatisha kwa miguu, ng'ombe, mbuzi wanyama pori na kadhalika.

Barabara yoyote yenye lane moja mara zote speed limit ni kilomita 50, sasa iweje sisi barabara hiyo watu waendeshe kwa speed ya 80 au 100 na iwe kiwango kinachokubalika? barabara zetu hasa Highway lazima ziongezwe ukubwa wa lane zake na zipite mbali na makazi ya watu, wanyama na kadhalika.
 
hii hatua ni ndogo sana lakini ni nzuri pia kama ikifanyiwa kazi kwani hata kama itapunguza vifo vya watu wawili tanzania nzima bado inafaa sana.
ukichunguza kwa makini hata kwa kuangalia taarifa ya habari basi kila ajali inayotokea wakati abiria wanaulizwa utasikia ni mwendo kasi,swali je ni kwa nini mwendo kasi?mwendo kasi huo unasababishwa na nini?
tukirejea malalamiko ya madereva wa mabasi ya mkoa utaambiwa mambo mengi sana.
mfano ni kitambo sasa madereva wanalalamika kuto kuajiriwa badala yake wao ni vibarua tu.wizara husika iko kimya kama haiwasikii hivi
ukijiuliza kwa nini madereva wakimbize magari hapa ndipo utapata sababu nyingi sana kama zifuatazo.
1-barabara zimejaa matuta kibao yani utafikiri sio barabara za masafa marefu(mfamo barabara ya dar-arusha) dereva inabidi atembee polepole huko kwenye hayo matuta na ukiongeza na mashimo yaliopo kwenye baadhi ya maeneo unakuta eneo la kutumia nusu saa katumia masaa mawili halafu bado unamshauri akikuta eneo liko sawia asikimbize gari huo mda aliopoteza huko kwenye matuta na mashimo ataufidia saa ngapi?
2-utitiri wa matrafki wenye vitochi nao unachangia sana ajali kutokea,yani unakuta trafki katega mahali na kitochi chake sasa derevaakifika pale anapunguza mwendo ili kumzuga akisha mpita gari inakua ndege.lakini kabla hajafika mbali anakutana na trafki mwingine tena kwa hiyo inabidi azuge tena na mwendo wa kuzuga unaendelea mpaka afike anakokwenda.
3-uelewa mdogo wa abiria na watanzania wengi kwa ujumla juu ya sheria za barabarani.unakuta gari limeharbika sehemu ya hatari kabisa mfano kwenye kona,watu wanaweka majani na kugeuza eneo hilo ndio gereji tena hata kwa zaidi ya masaa matano bila kuliondoa hapo.sasa hata kama ni basi linatoka kwa mwendo wa kawaida bado hatari ya ajali itakuepo tu.
kwa watanzania kutokua na uelewa juu ya sheria za barabarani ni tatizo kubwa sana we angalia mtu akigongwa inakuaje,yani hatakama huyo aliegongwa ndio mwenye matatizo bado usalama wa dereva utakua mdogo kwani kama atasimama hapo ni lazima apigwe tu
hayo hapo juu ni machache sana ila yapo mengi sana kama madereva watasikilizwa naamini ajali zitaisha kabisa.
 
Nakubaliana na namba 3

Halafu ongeza sasa kuboresha miundombinu. It is time barabara zote kuu zipanuliwe...sijui kitaalamu wanaiitaje ile gari zinazoenda opposite directions zisitumie barabara moja!
 
Mkuu na sisi tunaofanya jogging unaweza itumia kufuatilia mwendo? Kama inawezekana unaitumiaje?

miye naitumia sana kwenye "route march" zangu ni za uhakika!
Ni rahisi tu ukiwa na smartphone ukadownload hiyo application kwenye Google play,halafu inakupa maelekezo
mwisho wa mwezi/mwaka itakupa jumla ya kilometres ulixokimbia kcls(ugali) ulotumika
 
Tufanye sasa tayari sheria ulizoziainisha zimepitishwa halafu mimi ndo kamanda usalama barabarani mathalani Dodoma.

1.Ikibainika dereva wa basi alikuwa speed inayozidi 40km/hr abiria mtaumia aisee mtakula bakora za kutosha na dereva ananyang'anywa leseni.Dar-Mza siku mbili.

2.Dereva akibainika amelewa,anaswekwa lupango miaka mitano(hakuna msamaha wa rais) na kufanyishwa kazi ngumu.

3.Ikitokea ajali na watu wakapoteza maisha,mmiliki wa hicho chombo atapaswa kuwalipa fidia(actually kifuta machozi) 80mil kila marehemu na 200mil kwa majeruhi wenye ulemavu wa kudumu kama kisababishi cha ajali ni ubovu wa chombo au uzembe.

4.Kama chanzo cha ajali ni ubovu wa chombo basi dereva,makenika,mmiliki watakuwa answerable NB hizi kesi haziendi mahakamani ni kitengo kinakuwepo maalumu kwa ajili ya ajali.

5.Mabasi yote na malori ya usafirishaji hayataruhusiwa kuwa barabarani yakitembea 300,000km

6.Madereva wa malori na mabasi wawe na elimu ya kidato cha sita na kuendelea na lazima awe na uzoefu wa 10yrs bila ajali ndo akabidhiwe gari kwengine.

7.Bodaboda akipata ajali kama abiria hajafa basi anapewa yeye hiyo pikipiki na unamlipa fidia na bakora unakula.

8.Basi likifika stendi kabla ya mda uliopangwa abiria mnatoa maelezo na bakora juu.

Nitaendelea.......

umetisha mkuu
 
Jawabu ni Smart phone

Huawei Ascend Y530,download application iitwayo "My tracks"- controller akae siti yoyote ya BASI,safari ianze.
Speed,umbali, vyoote vitaonyeshwa na muda uliotumika kituo hadi kituo!

Mahitaji:-
1)smartphone kama iliyotajwa hapo juu au iliyo bora zaidi.

2)mtu(operator) wa simu hiyo
3)power bank(chargers)

4)My track(application) haihitaji mtandao wa simu ila smartphone iwe na line ya sim(sim card)

Utaratibu

Smartphone ikaguliwe na RTO au wakala wake!
Dereva asini kuwa smartphone yenye IMME 12345678... Ndiyo itakayo record mwendo wa basi lake kwa siku hiyo!

Kama una mawazo bora zaidi changia

wazo zuri
 
hii hatua ni ndogo sana lakini ni nzuri pia kama ikifanyiwa kazi kwani hata kama itapunguza vifo vya watu wawili tanzania nzima bado inafaa sana.
ukichunguza kwa makini hata kwa kuangalia taarifa ya habari basi kila ajali inayotokea wakati abiria wanaulizwa utasikia ni mwendo kasi,swali je ni kwa nini mwendo kasi?mwendo kasi huo unasababishwa na nini?
tukirejea malalamiko ya madereva wa mabasi ya mkoa utaambiwa mambo mengi sana.
mfano ni kitambo sasa madereva wanalalamika kuto kuajiriwa badala yake wao ni vibarua tu.wizara husika iko kimya kama haiwasikii hivi
ukijiuliza kwa nini madereva wakimbize magari hapa ndipo utapata sababu nyingi sana kama zifuatazo.
1-barabara zimejaa matuta kibao yani utafikiri sio barabara za masafa marefu(mfamo barabara ya dar-arusha) dereva inabidi atembee polepole huko kwenye hayo matuta na ukiongeza na mashimo yaliopo kwenye baadhi ya maeneo unakuta eneo la kutumia nusu saa katumia masaa mawili halafu bado unamshauri akikuta eneo liko sawia asikimbize gari huo mda aliopoteza huko kwenye matuta na mashimo ataufidia saa ngapi?
2-utitiri wa matrafki wenye vitochi nao unachangia sana ajali kutokea,yani unakuta trafki katega mahali na kitochi chake sasa derevaakifika pale anapunguza mwendo ili kumzuga akisha mpita gari inakua ndege.lakini kabla hajafika mbali anakutana na trafki mwingine tena kwa hiyo inabidi azuge tena na mwendo wa kuzuga unaendelea mpaka afike anakokwenda.
3-uelewa mdogo wa abiria na watanzania wengi kwa ujumla juu ya sheria za barabarani.unakuta gari limeharbika sehemu ya hatari kabisa mfano kwenye kona,watu wanaweka majani na kugeuza eneo hilo ndio gereji tena hata kwa zaidi ya masaa matano bila kuliondoa hapo.sasa hata kama ni basi linatoka kwa mwendo wa kawaida bado hatari ya ajali itakuepo tu.
kwa watanzania kutokua na uelewa juu ya sheria za barabarani ni tatizo kubwa sana we angalia mtu akigongwa inakuaje,yani hatakama huyo aliegongwa ndio mwenye matatizo bado usalama wa dereva utakua mdogo kwani kama atasimama hapo ni lazima apigwe tu
hayo hapo juu ni machache sana ila yapo mengi sana kama madereva watasikilizwa naamini ajali zitaisha kabisa.

Mawazo yako yana balance!
Na uelewa wako kuhusu waTz na Barbara ni kweli !
Lakini ukiwa na speed tracking system hatutahitaji vitochi!
Record zote zinatunzwa kwenye computer mbalimbali!
Na record za tracking system sio rahisi kuziediti
 
Kwanza ajali hizi za mabasi zinatokea kwasababu ya mgogoro uliopo kati ya wamiliki wa mabasi na madereva.

Madereva wanaiona kazi ni ngumu na muda wakuifanya ni mfupi yaani kusafiri umbali mrefu kwa siku moja(Masaa 12 Dar-Mwanza) mf. Huo.

Pia wanalipwa pesa kidogo. madai hayooo!

Lakini uhusianao uliopo kati ya wamiliki mabasi na vigogo wa serikalini ambao ni viziwi kuwasikia RAIA wa kawaida nao ni tatizo. Wamiliki wa mabasi wapo serikalini sio wale vivuli tunao wasikia wakiongea ongea tu.

Kuna jamaa mmoja yuko Zambia leo anasema huko wanaonekana wanamatatizo na sio waaminifu lakini LA zaidi ni uzembe wa serikali kutokuona tatizo.

Uchawi jambo lingine so. It is beyond my capacity maana wengi wanadai ni KAFARA za uchaguzi!
 
huawei haiwezi kuzuia kontena kudodokea juu ya basi, au kuna app ya container skipping??
 
Mbona matrafiki wote watakukimbia: wataomba uhamisho haraka sana coz nao ni wazembe.

Bakora ni zile kama za Mwalimu ama! Maana enzi za mwalimu hakuna mchezo....
Wangekura bakora tu!
 
Umemaanisha serikali hii hii ya kifisadi ya ccm chini ya mr dhaifu aka vasco dagama kikwete? Wako busy na urais na kupiga dili za kuliibia taifa ili wapate pesa za kununulia kura
 
Hao ndio madereva walio tetewa wasisome!
 
ulilolizungumza ni.kweli ila sekta ya usafirishaji ninaimani.imebeba ajira kubwa sana kwa wananchi wengi wengne ndo hao wakina boda boda nk. ila chamsingi ni kuwapa tu elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya vyombo vya usafirishaji pamoja na matumizi ya barabara.....the maaskari wapunguze kupokea hongo
 
Kwani ni Ajali zote huwa zinasababishwa na mwendokasi?? Vipi kuhusu umakini wa dereva barabarani??

Ku-overtake kwenye kona au mlima, ku-overtake magari zaidi ya mawili kwa mpigo tena yote yakiwa kwenye mwendokasi, service za mabasi yenyewe lakini pia wakati mwingine ni uzembe tu wa madereva wengine kwa mfano ile ajali iliyosababishwa na Passo hivi majuzi..

Unaweza kuovertake magari yaliyo kwenye mwendo kasi mkubwa bila ya wewe kuwa kwenye mwendo kasi mkubwa?
 
huawei haiwezi kuzuia kontena kudodokea juu ya basi, au kuna app ya container skipping??

soma mada (kupata takwi
my za Basi na mwendo wake) .
suala LA kontena kuanguka umelitoa wapi?
kwani matairi hapasuki?
mada haisema hata speed ipi ndo muafaka.

tujaribu kutumia jf kwa kujielimisha na kuelimishana sio @ jambo mpaka ulitafutie harufu mbaya.

hapa inakiwa jambo moja liondolewe ha lafu jingine litaonekana.
kama vile:-
matairi mabovu
barabara mbovu
viroba vya pombe
kazi kubwa kwa dereva(Massa 15 bila kupumzika)
kukimbilia abiria

kubeba mzigo kupita kiasi
nk nk nk
 
Jawabu ni Smart phone

Kwanza naunga mkono hoja kwamba ajali nyinga sana hapa nchini zinasababishwa na mwendo kasi uliozidi. Hili halina ubishi hata kidogo. Lakini niulize: Hivi unafikiria polisi wanashindwa kuzuia mwendo kasi uliozidi kwa sababu hawana ushahidi kuwa magari yanakimbia sana? Bila hata kutumia hiyo application unayosema ziko njia luluki za kujua kama basi inakimbia. Na zaidi niseme polisi wanajua kabisa magari yanayokimbia. Kitu kinachofanya haya mabo yasiishe ni rushwa! Nakuhakikishia kama kusingekuwa na rushwa iliyokithiri madereva wote wangeshika adabu na wangekuwa na mwendo unaokubalika. Ni kama wanaosema adhabu ya kifo itumike kwa mafisadi! Mimi huwa nasema kuwa tatizo si adhabu bali wanakamatika? Pamoja na changamoto hii lkn wazo lako bado ni zuri sana sana = ku-monitor speed ya mabasi!

Halfu njia ulipendekeza ya kutegemea applicatin ya simu sio realiable! Kuna navigation system nyingi tu tena za uhakika zinaweza kutumiwa na polisi kujua mwendo wa mabasi. Ukiwa sehemu kama Ulaya na unasubiri basi kuna sehemu zenye screen yenye ramani inakuonyesha basi linavyotembea, liko wapi na muda litakaofika na mwendo wake. Hivi ni vitu affodable kabisa kununulika. Mwisho niseme sikupinga wazo wako ila nimeonyesha changamoto zake nyingi na mwisho nikiri una wazo zuri lakini naomba tutumie navigation systems zilizo reliable na sio application za simu.
 
Smartphone ikaguliwe na RTO au wakala wake!
Dereva asini kuwa smartphone yenye IMME 12345678... Ndiyo itakayo record mwendo wa basi lake kwa siku hiyo!

Kama una mawazo bora zaidi changia

Vivax usife moyo kuanzisha mada zenye tija.

Kukosoa ni kazi nyepesi sana. Mnapokosoa, fikirieni pia kupendekeza suluhu mbadala ya hoja au pendekezo lililoko kwenye mada. Wachache wameonesha mfano hapa.

Mimi nitaongezea kwa kushauri kila gari lifungwe dashboard camera. Kama ambavyo ni lazima gari kuwa na insurance, iwe lazima kufunga dashcam. Iwepo adhabu kwa watakaokiuka utaratibu huu.
 
Back
Top Bottom