TUNDALI,
Mkuu umeandika mengi lakini bahati mbaya ni kuwa ume bwabwaja zaidi kuliko kuwa na hoja.
Hujaona magari ya serikali au ya mashirika ya umma yakihusika kwenye ajali? Ni magari ya umma yapi yanayofuata alama za barabarani? Yapi yanayojua kuna speed limit barabarani au hata kuwa kuna zebra crossing?
Mkuu kwa kukumbusha tu au kukufahamisha kama ulikuwa hujazaliwa siku za nyuma kulikuwa na mabasi ya serikali yakiwamo Kamata, mabasi ya Railways, Kauma, Kaudo, UDA, CoCabas nk you name them. Yote yalikufa kifo cha mende achilia mbali kuwa yalikuwa hayasumbuliwi na polisi wala mamlaka kama Sumatra kama wanavyofanyiwa hawa ambao wewe una uthubutu wa kuwaona kuwa wana akili zero. Ndugu ni eneo lipi ambalo wewe unalitanabaisha na akili zozote huku makwetu? Kwa nini wachina na makampuni toka nje yanaendelea kuja kutujengea mabarabara? Hatuna wahandisi wetu kufanya haya? Huko midogodini je hatuna ma geologisit?
Sidhani kama kulikuwa na moral authority ya kuwabeza baadhi ya watu katika nchi hii tokea katika hoja nyepesi nyepesi kama zako pasipo na kuangalia boriti kwenye jicho lako kwanza.
Wapo watu katika mamlaka wenye maslahi tofauti ambao wasingependa sekta binafsi ya usafirishaji ku prosper hilo ni wazi. Kama wangekuwa mamlaka zingekuwa na maslahi mapana ya nchi at hand kwa kuanzia wapiga debe wasingekuwapo katika vituo vya mabasi.
Uliwahi kujiuliza nani anawalea wapiga debe kinyume cha matakwa ya abiria wala wenye mabasi?
Nitakuwa sijakutendea haki kama sitakukumbusha kuwa kudai fulani ana ukwasi mkubwa kwa hisia tu bila ya yeye kusema hivyo ni kutojitendea haki wewe mwenyewe. Palikuwa na uzi hapa wa mzee Sumry aliyefikia hatua ya kufunga biashara ya mabasi kurejea shambani tokana na usumbufu na hasara kubwa inayoambatana na biashara hii.
Ni ajabu na kweli mtu unapotokea bila ya facts zozote ku rukia kwenye conclusions kama ulizoweka kwenye bandiko lako na kwa hoja za ki Sizonje kama ulizoweka.