Ajali: Tuambiane ukweli dhahama hili lituepuke

Chanzo kikubwa cha ajari nyingi ni miundo mbinu mibovu,barabara ni za lami lakini mashimo kama yote,ukisema elimu unamaanisha madereva wa mabus hwajapitia NIT !? Sio kweli angalia maderava wanaoendesha viongozi wote ni walewale lakini wanaongoza kwa matukio
 
Mkuu tuition wala haisaidii. Imekuwa miaka mingi mno. Bora graduates wakamate usukani wenyewe kabisa.
Dar lux alichukua hao akasahau maswala ya elimu na vyeti haviusiani akachukua vijana wabichi kabisa wanamwaga Moto bila tahadhari haivuki week mbili isipogongwa itagongwa
 
Ukweli n mchungu lakini tufike mahali tuuseme hata kama unauma.

Mengi yamesemwa kuhusu ajali miaka nenda rudi, lakini ajali ziko pale pale.

Bahati mbaya mzizi wa tatizo umekuwa hausemwi kwa kujua au kutokujua.

"Tatizo letu kuu kimsingi ni ujinga ndugu zangu."

1. Kulikoni dereva kuendesha gari akiwa haoni waziwazi anakokwenda?

2. Kulikoni dereva kuendesha gari bila kujali hali ya miundo mbinu alipo?

Pana haja ya kurekebisha viwango vya elimu angalau kwa kuanzia, madereva wa mabasi na malori.

Kwanini kutokuwatumia wahitimu wa vyuo vikuu kuendesha mabasi?

Kwanini kama ilivyo kwingine kama kiwango cha juu cha mwendo ni 80km/h, isiiwe hivyo kwa vyombo vyote vya moto barabarani?

Kwa kuzingatia haya tu, ajali zitakwisha.

Serikali inao wajibu.
shida sheria hazifuatwi na faini haziumizi ... serikali iweke kamera barabara zote za mkoani kupiga picha watu wa mwendo kasi. faini za laki 2 kwa kuongeza speed inatosha kumuadhibu dereva akirudia mara 5 anakuwa anafaini mil 1 then leseni inapumzishwa kwa miezi 3 unafikiri mtu anayefanya kazi kutumia gari atajaribu kuvunja sheria maana atalala njaa
 
Ajari zitakwishaje wakati wengine wanafanya kazi kwa kutumia mazingaombwe?amesoma kwa kutumia mazingaombwe? Gari Ina mazingaombwe?anaendesha biashara kwa kutoa sadaka kwa miungu?

Africa haiwezi kuendelea kwa kutumia mazingaombwe!!
Mpaka kwa akina mama Lishe ni mazingaombwe tu ! 🙄🇹🇿 Tumeshapotea njia !!
 
shida sheria hazifuatwi na faini haziumizi ... serikali iweke kamera barabara zote za mkoani kupiga picha watu wa mwendo kasi. faini za laki 2 kwa kuongeza speed inatosha kumuadhibu dereva akirudia mara 5 anakuwa anafaini mil 1 then leseni inapumzishwa kwa miezi 3 unafikiri mtu anayefanya kazi kutumia gari atajaribu kuvunja sheria maana atalala njaa
Kabisa !
 
Chanzo kikubwa cha ajari nyingi ni miundo mbinu mibovu,barabara ni za lami lakini mashimo kama yote,ukisema elimu unamaanisha madereva wa mabus hwajapitia NIT !? Sio kweli angalia maderava wanaoendesha viongozi wote ni walewale lakini wanaongoza kwa matukio
Kwa majaribio iwekwe sheria madereva wa mabasi wasiajiriwe wenye umri chini ya miaka 45 ! Ni kuanzia 45 na kuendelea uone kama kuna basi litagongana na gari jingine uso kwa uso !!
 
Mbinu zilezile zisizo zenye matokeo duni na bado hazifuatwi, Wasimamizi wa usafiri wanadai wamefunga vi zibiti mwendo kwenye magari lakin kila siku tunaziona hizo ligi za magar ya abiria Maana yake nin!

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
 
Elimu ni ufunguo wa maisha. Wasomi wajinga wapo lakini ni wachahe Kwa asilimia ukilinganisha na mburula wajinga.

Fikiria:

1. Kulikoni dereva kuendesha gari akiwa haoni waziwazi anakokwenda?

2. Kulikoni dereva kuendesha gari bila kujali hali ya miundo mbinu alipo?

Inawezekana je? Tena Labda dereva huyo kabeba watu 50?
Kwahiyo wahitimu wa vyuo vikuu wao ndio wana akili kuliko wengine? Umeaanza vizuri ila hivyo vigezo vya elimu hapana. Kwani hao wasomi hawapati ajali na private car zao? Mimi nafikiri, it's all about maturity tu.

Kuna tabia fulani imejengeka kuanzia stand hadi kwy hayo mabus watu wanakuwa na haraka bila sababu za msingi. Fikiria bus linapotoka stand mwendo kama mnapaa lkn mkiwa huko porini hizo speed hola. Mkiingia kwy mji mabio yanaanza tena hadi unashangaa. Nafikiri ni mentality tu khs hiyo huduma. Na sio mabus tu, angalia bajaji na daladala hasa vihaice vurugu ni nyingi lakini matrafiki wao wako busy na private cars tu kuulizia triangle. Inabidi kupitia mfumo mzima na sio kuibuka tu inapotokea ajali ndio viongozi wanabweka kama mbwa koko.
 
Mbinu zilezile zisizo zenye matokeo duni na bado hazifuatwi, Wasimamizi wa usafiri wanadai wamefunga vi zibiti mwendo kwenye magari lakin kila siku tunaziona hizo ligi za magar ya abiria Maana yake nin!

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
Hawako siriaz na uhai wa watanzania !!
 
Tatizo la ajali za Tanzania ni barabara kuwa ndogo,halafu magari ni mengi.Kinachotakiwa kifanyike ni kupanua barabara zote kuu,Dar to Tunduma, Dar to Mwanza, Dar to Arusha, Dar to Mtwara.Hizo njia kuu zikishatanuliwa, tutakuwa tumeokoa vifo vya ajali kwa asilimia 90
Hapo umenena mkuu! Tatizo la ajali sehemu kubwa linaratibiwa na barabara zenyewe! Kwanza nyingi ni chini ya kiwango ingawa kuna majinga yanatamba nazo! highway toka lin ikawekwa bams? Madereva kufuata sheria lkn na serikal kutimiza wajib wao! Barabara na magar sio vyanzo rasmi vya mapato kwa polis wetu! Imefikia hatua polis trafik anasubiri mtu avunje sheria ili akachukue fedha au apige faini! Kuna ajali nying mno zinasababishwa na hawa ndugu zetu polisi lkn mzigo anabebeshwa dereva
 
Ukija kwenye timu ya wakaguzi wa magar upande wa polisi! Kwanza hawana ujuzi wowote wa mv mechanics! Taaluma ya magari ni pana mno sio ya mtu wa umri wa mtu mzima mwenye majukumu ya familia kwenda veta au nit kwa mwezi mmoja halaf unampa majukumu ya kukagua gari!
 
Ukweli ni mchungu lakini tufike mahali tuuseme hata kama unauma.

Mengi yamesemwa kuhusu ajali miaka nenda rudi, lakini ajali ziko pale pale.

Bahati mbaya mzizi wa tatizo umekuwa hausemwi kwa kujua au kutokujua.

"Tatizo letu kuu kimsingi ni ujinga ndugu zangu."

1. Kulikoni dereva kuendesha gari akiwa haoni waziwazi anakokwenda?

2. Kulikoni dereva kuendesha gari bila kujali hali ya miundo mbinu alipo?

Pana haja ya kurekebisha viwango vya elimu angalau kwa kuanzia, madereva wa mabasi na malori.

Kwanini kutokuwatumia wahitimu wa vyuo vikuu kuendesha mabasi?

Kwanini kama ilivyo kwingine kama kiwango cha juu cha mwendo ni 80km/h, isiiwe hivyo kwa vyombo vyote vya moto barabarani?

Kwa kuzingatia haya tu, ajali zitakwisha.

Serikali inao wajibu.
hata barabara zetu ni tatizo kubwa, ni nyembamba mno. Barabara nyingi zina upana wa mita tano basi na lori vikikutana lazima wakwepane hadi wafika eneo la waenda kwa miguu, na huko kama kuna mtu anatembea au kuendesha baiskeli/pikipiki....unamuachia Mungu tu.
 
Wakati Magufuli anawaambia matrafic wawabane madereva wazembe mkasema ni mshamba!

Mama yenu kupitia kinana akaondoa matrafic barabarani mkashangilia eti anafuta legacy!

Kunyweni damu za wanaofariki sasa!

Mavi matupu nchi hii
Sifa ya mjinga ni kutokua na kumbukumbu
 
Elimu ni ufunguo wa maisha. Wasomi wajinga wapo lakini ni wachahe Kwa asilimia ukilinganisha na mburula wajinga.

Fikiria:

1. Kulikoni dereva kuendesha gari akiwa haoni waziwazi anakokwenda?

2. Kulikoni dereva kuendesha gari bila kujali hali ya miundo mbinu alipo?

Inawezekana je? Tena Labda dereva huyo kabeba watu 50?
Haya matatizo mawili mzizi mkuu ni tabia na mazoea ya wahusika.

Kuwa na elimu pekee Kwa madereva sio suluhisho tosha. Magari ya serikali Yana madereva wasomi Ila wakiwa barabarani akili zinafyatuka. Nadhani udereva mzuri ni ustaarabu WA mtu binafsi makuzi yake, na Ile Haiba ya kutii Sheria bila shurti.

Mamlaka inabidi iongeze umakini katika utoaji wa leseni, iwe Kama wenzetu nchi za ulimwengu wa Kwanza kule mpaka upate leseni ya udereva ujue umepiga mafunzo mengi barabaran yaani ni mtiti kwelikweli .
 
Mawili hayo ni matokeo ya ujinga siyo kingine. Dawa ya ujinga ni elimu ya kutosha.

Magari ya serikali hayaendeshwi na wasomi aina ya tunao warejea hapa.
 
Ukija kwenye timu ya wakaguzi wa magar upande wa polisi! Kwanza hawana ujuzi wowote wa mv mechanics! Taaluma ya magari ni pana mno sio ya mtu wa umri wa mtu mzima mwenye majukumu ya familia kwenda veta au nit kwa mwezi mmoja halaf unampa majukumu ya kukagua gari!

Huku ndiyo kuchanganyikiwa halisi. Hili la ukaguzi waachane nalo wanajidhalilisha tu.
 
Back
Top Bottom