Ajali ya bodaboda jijini Mwanza

Ajali ya bodaboda jijini Mwanza

Ni mbaya lakini itawafundisha wengi watakaoiona. Hasahasa bodaboda
Nakazia hoja. Hii labda inaweza kuwa ndo kauli au lugha ambayo bodaboda wataielewa. Ajali hazijaanza leo lakini hao bodaboda hawasikii na wala hawajirekebishi na wala hawajifunzi na inaonekana tunampigia mbuzi gitaa - ni majanga tupu - Wamekaza shingo.
Basi inapendeza zaidi hao-hao watumike kama Teaching aid kwa wenzao wachache watakaotusikia. Tumechoka nao - utasaidia wangapi na mpaka lini? Mbona hawatoi ushirikiano nasi i.e. wanaonywa siku zote wawe waangalifu, waache kuendesha rafu na wazingatie sheria za barabarani. Boda akimgonga mtu badala ya kusimama amsaidie majeruhi, yeye anakimbia(anasepa)......
 
Mara nyingi sana ajali wanazopata boda boda hua wana jisababishia wenyewe kwa upumbavu wao lakini hua hawajifunzi acha waendelee kupungua tuu
 
Una roho mbaya!!
Labda inawezekana lakini bado hajafikia kiwango cha roho mbaya walicho nacho hao maBoda boda. Wanaweza kugonga say kwa bahati mbaya lakini wanakimbia, wanakutelekeza wanakuacha ujifie mwenyewe hapo pembeni ya barabara endapo hutapata msaada.
 
Yani nafikiria kichwani sijui wamegongana vipi, mmoja kushoto na mwingine kulia, mmoja kamfuata mwenzie au wote walikuwa wamezidi sana karibu na kati au mmoja alifanya uzembe wa kuangalia nyuma kidogo then wakakutana aah!...TZ kwamba napo Sasa hv tumechoka sana na maisha au vipi.
 
Watu ni wajinga sana Mkuu yani mtu anadrive/ride/tembea kama yupo korido za chumbani kwake
Mimi hii rule wakati nikidrive huwa inaniokoa sana,kuna wakati,najiulizaga hivi nisingezidi kushoto kwangu ingekuaje baada ya kupishana na careless driver

Always nikikaribia kona yoyote ile ambayo mbele sioni lazima nijae kwangu kushoto,halafu unakuta kama Mungu tu ukifika tu,mwehu huyo kaingia hadi kwako sema anashindwa kukugonga kwa kuwa umebana kushoto zaidi
 
Kuzaliwa tz ni michosho sana

Watu hawajui hata kukabiliana na emergency,mwanzo nilidhani ni vijijini huko, sasa hapo misungwi ajali imetokea barabarani magari yamejaa wanazima moto na mchanga na maji kweli?

Fire extinguisher kwenye magari ni kuajili ya kuonyesha traffic officers? Mbona magari yapo nilitegemea Kuona mtu anakuja na fire extinguisher
Hao fire wenyewe wanawaza moto ukiwaka kwao watamuita nani? Endelea kushangaa
 
Mleta mada usiseme bodaboda bali sema maafisa wasafirishaji. Wapo wakulungwa waliwasifia hawajamaa kama ni maafisa nyakati za uchaguzi
 
Boss mbona unawaita waTz wenzako watu wa hovyo ilhali na ww ni mTz? halafu pia mtu unamwita limtu kana kwamba hafai au hatoshelezi viwango vya kuwa ni mtu kamili?
Sioni kama huyo aliyerocord tukio kama amekosea sana kwa sababu inaelekea bodaboda darasa lao ni moja -Shingo ngumu. Leo anapata ajali huyo, kesho anakufa yule n.k.n.k. lakini wap! hawajifunzi wala hawabadiliki - utadhani ni sifa kwao.
Ajali hapati bodaboda tu. Siku zote inapotokea janga lolote common sense ni kutoa msaada kwa waliofikwa na tukio. Sasa kama unaona mtu anateketea kwa moto badala ya kusaidia wewe una record video una sifa ya kuwa mtu au limtu?
 
Vijana hawajapita jkt...vijana wa kitanzania ni wazembe sana
Sidhani kama mtu anahitaji kupitia JKT ili aweze kutoa msaada. Kwanza jamaa anaonekana anaelewa mambo mfano anawaambia wasimwage maji kwakuwa ni moto wa petrol. So huyo angalau ana idea ya fire fighting lakini sasa ndio hana msaada zaidi ya kuchukua video.
 
Mimi hii rule wakati nikidrive huwa inaniokoa sana,kuna wakati,najiulizaga hivi nisingezidi kushoto kwangu ingekuaje baada ya kupishana na careless driver

Always nikikaribia kona yoyote ile ambayo mbele sioni lazima nijae kwangu kushoto,halafu unakuta kama Mungu tu ukifika tu,mwehu huyo kaingia hadi kwako sema anashindwa kukugonga kwa kuwa umebana kushoto zaidi
Hongera sana mkuu, unajal uzima wako na ustawi wa familia. Hawa wehu muda mwingine ni kuwakimbia tu uwaachie barabara ukishindana nao wanakuua.
 
Back
Top Bottom