Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

No no no, dereva tulishamsikia. "Mheshimiwa" amesema nini?

TBC wamesema dakika 30 zilizopita Mkuu ndo katoka hospitali. Sasa ulimsikia on bed side interview hospitali?

una maana gani ya kutumia quote on quote "mheshimiwa"?
 
Mh! Tz tusipoangalia sasa tunaelekea pabaya. Siku zinavyoenda ndo mambo yanazidi kufanyika wazi bila haya! Sijui wanafikiri si wote vipofu na wajinga, tuna akili za kuanalyze tunavyoviona. Tukiendelea hivi, patakuwa hapatoshi jamani, who knows who will be targeted next?!

Mungu ibariki Tz, hasa nyakati kama hizi!!
 
Mheshimiwa Mwakyembe ameweza kuongea leo, yeye amesema amemwachia Mungu kwa maana yeye ni Mkristo na kama ilikuwa ni ajali ya kawaida basi anamwachia Mungu na kama kuna mkono wa mtu yaani hiyo ajali ilikuwa planted basi anamshitakia Mungu,

...haya sasa, mheshimiwa mzima anaanza kutuletea paukwa pakawa! akisema hivyo kina Mudhihir Mudhihir na Kapuya nao waliopata ajali watasemaje?

ameweza kudeclair yeye mwenyewe kuwa gari lake liligongwa kwa nyuma ingawa anasema liligongwa kidogo kwenye taa ya nyuma

...alijuaje kwenye taa ya nyuma iwapo alipoteza fahamu kwa mshituko? ...kahadithiwa?

...likaongeza motion ya gari lake na dereva waka akapanic baada ya kuona hawezi kulimudu ndo akalitoa nje ya road reserve

...Kwenye picha, taa ya kulia inaonekana nzima. Ndio kusema kama lori lilikuwa linawafuata kwa kasi na kuwagonga lingewagonga taa ya kulia, sio kushoto.

Aseme tu baada ya ku overtake dereva wake alipunguza mwendo ghafla kuogopea hako kashimo lndio maana wakagongwa kushoto!...
Simlaumu dereva, anatetea unga wake.

.. sasa hapa nafurahi mno kusikia yeye mwenyewe amesema hivyo sijui kamanda Nyombi ataendelea kushikilia msimamo wake kuwa tairi imechomoka dah...

...kama limechomoka ajabu ni nini kwenye impact kama hiyo?
 
una maana gani ya kutumia quote on quote "mheshimiwa"?

Kwanza kula tano!

Maana kama watu wangekuwa makini hivyo, kuulizana kwa nini hapo umeweka nukuu, tungekuwa mbali sana.

Nimeweka nukuu kwa sababu kuna mchangiaji kasema dereva na mheshimiwa wameelezea ajali.

Sasa sikukata ku assume kwamba ana maanisha Mwakyembe, na mimi nikamrudishia na Mheshimiwa hiyo hiyo:

Sasa kama "mheshimiwa" ni Mwakyembe, atakuwa kaongelea ajali saa ngapi manake ndo kwanza anaripotiwa na TBC kwamba ndo anatoka hospitali? Mleta habari "Vijisenti" hajarudi tena!
 
Leo Dk Mwakyembe kazungumza. Nimemsikia akisema kuwa walikuwa wakijaribu kumpita dereva wa lile lori lakini wakati dereva wa lori lile hakuwa anataka apitwe na gari ya Mwakyembe! Na walipokuwa wakimpita aliongeza mwendo na kusababisha kugongwa na lori kwa nyuma na hivyo kusukumwa na kupinduka. MAelezo ya Dk Mwakyembe yanashabihiana na maelezo ya Dereva wake ambyo niliyachukia kama ni kujitetea tu kwa uzembe wake.

Nadhani wale waliokuwa wakipinga sana maelezo ya dereva sasa na wajitokeze kumuomba samahani. Maana kwa kweli walimshambulia sana mtu wa watu afadhali Dk. kathibitisha mwenyewe. Tuwe makini wakati tunatoa comments zetu!
 
Nasikia Mwakyembe kisha zungumza.. habari zake zinafanana na dereva, lile shimo halikuwa sababu isipokuwa waligongwa kwa nyuma na lori dereva wake akapoteza control..
 
Tunamwombea apone upesi arudi katika majukumu ya kila siku nafkiri pia watoto na familia yake wapewe uangalizi na faraja katika siku kama hizi' tuwaamini madaktari wetu na tuepuke dhana zisizo na msingi na ambazo hata tukishikia hazitatua! Kama ipo ipo tu ndugu zangu, hakuna tukio au suala pasina sababu, 2jipe moyo na 2ongeze mapambano kama si leo basi kesho, yeye aliweza basi nasi tutaweza kwani wao wana nini? Tusonge!
 
Ni mapenzi ya Mungu, tumuachie Mungu.

Mkuu ni kawaida yetu sisi binadamu tukifanya jambo au tukifikwa na jambo ambalo tumesababisha sisi wenyewe tunawasingizia Mungu na shetani. Haya ni clearly mapenzi ya mtu, najua sasa atakuwa anasikitika sana. Mapambano siku zote yanakuwa magumu, kuna wanaofika nchi ya ahadi na aambao hawafiki nchi ya ahadi.

Tanzania ya sasa ni ya 2000 na sio ya 1947. Lakini tatizo ni kuwa sisi watanzania wa leo bado tunabehave kama wale wa 47. Hatuwezi hata kuwapigania wanaotupigania, badala yake tunaendelea kuwatukuza mafisadi. inasikitisha.
 
Dereva ana umri gani miaka 30 au 36 maana kuna hadithi mbili hapa ..
 


Tunamwombea apone upesi arudi katika majukumu ya kila siku nafkiri pia watoto na familia yake wapewe uangalizi na faraja katika siku kama hizi' tuwaamini madaktari wetu na
tuepuke dhana zisizo na msingi na ambazo hata tukishikia hazitatua! Kama ipo ipo tu ndugu zangu, hakuna tukio au suala pasina sababu, 2jipe moyo na 2ongeze mapambano kama si leo basi kesho, yeye aliweza basi nasi tutaweza kwani wao wana nini? Tusonge!
Yeye mwenyewe Mwakyembe ame hinti hinti kuna mkono wa mtu, eti anamwachia Mungu

Nani sasa unasema aupuke dhana zisizo na msingi? Cheki hii posti.
 
Yeye mwenyewe Mwakyembe ame hinti hinti kuna mkono wa mtu, eti anamwachia Mungu

Nani sasa unasema aupuke dhana zisizo na msingi? Cheki hii posti.


kwani muhashimiwa anaamini yale mambo yetu ya kiswahili???? maana ni ngumu kuhisi fauol play hasa ukizingatia hali ya barabara zetu na tabia mbaya za madereva wa magari makubwa[na kwamba walimfanyia uhuni kwa kuwa yeye ni mwakyembe au kwa kuwa gari lake ni dogo?]....zaidi ya hapo theory pekee inayoweza kuprove "mkono wa mtu" ni manyanga manyanga!

kama tukiamua kubase kwa Mungu ...tutasema ni bahati mbaya tu kidunia na kwa Mungu ameamua kumdhihirishia mwakyembe kuwa bado kazi yake inahitajika aongeze mwendo wa kuwatumikia waananchi kwani amemkumbusha kuwa muda unakwenda na kifo kipo.......
 
- Ni mapema mno, kunahitajika muda kidogo kupata facts zote ila hatuwezi ku-rule out anything kwa sasa, ingawa ni mapema mno ku-speculate!

FMES!

 
- Ni mapema mno, kunahitajika muda kidogo kupata facts zote ila hatuwezi ku-rule out anything kwa sasa, ingawa ni mapema mno ku-speculate!

FMES!

Majasusi waliofuzu kuuwa kwa ajali it's the last resort [tena zamani ] and risky kwani mara nyingi target wanakuwa na uwezekano wa kupona.

Eyewitness wanaweza kutokea, na pia inampa target muda wa kuwasiliana kuomba msaada pale anapohisi gari inamfuatilia na haitaki kupita au kupitwa... na hawawezi kutumia lori ambalo halina maneuvering flexibility ku-escape baada ya tukio... na zaidi ya yote ku-eliminate kwa kutumia gari kuna risky pia kwa agent kuwa involved kwenye accident [refer kifo cha Sokoine gari ya Dube iliyosababisha ajali ilishindwa kuondoka, iliumia, target mwenyewe (kama kweli) hakuweza kufa na inahisiwa alijaribu kukimbia akawa hit from the back (chest)]....

So who wants to risk?... Refer uuaji wa the most feared UGANDA RESEARCH BUREAU..... Mara zote ajali walizokuwa waki plant targets walipona ..na iliwalazimu kuyapindua magari na kuyachoma moto... kiasi hata mtoto mdogo akiangalia alijuwa ni USR involved!!! ...angalia kifo cha Princess Diana cha ajali hadi leo kimeacha doa kwa M15.. [wengi wanadhani mapaparazi waliwakimbiza wakijuwa along the way wangeweza kupata ajali, na pia inaaminika kuwa ambulance ya kwanza kufika ilichelewesha kutoa huduma ya kwanza iliyohitajika kwani walikuwa hawajakata roho]. Inakuwa rahisi sana watu kugundua.


Ingekuwa ajali ya Mwakyembe ni ujasusi lazima kungekuwa na gari la surveillance nyuma ambao jukumu lao lingekuwa kujifanya wanatoa msaada baada ya ajali na jukumu lao ni kumalizia kazi kama wangekuta bado asingepona.!

Nafikiri tuache speculations kwani hali ya barabara zetu inajulikana tena ni bahati sana kwa barabara za highland ...huwa kuna maporomoko marefu sana ambako gari ikiingia hata kuinasua ni kazi na msaada wa majeruhi labda mlete helicopter...
 
No wonder tunawauwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi kama uwezo wetu wa kufikiri ndiyo huu.

Nawaombea kwa mwenyezi Mungu awasamehe wale wote wenye mawazo potofu.
 
Kinacho nishangaza mimi ni kuwa wakati ajali inatokea, kulikuwa na basi (Dr. Mwakyembe ameita coaster, nadhani hakuona vizuri) ndani ya hilo basi kulikuwa na askari wa usalama bara barani wawili (Two Traffic Police). Hao askari ndo waliookoa mali na nyaraka za Dkt. Mshangao wangu ni kwanini hawakufanya jitihada za kuzuia lori linalohusika na ajali hata kwa kuwapigia simu askari wenzao? Kama dereva wa lori hatapatikana, nitaunga mkono shaka hii.

JF HOME OF GREAT THINKERS.

Wewe unafikiri hao matrafiki wanatumia nguvu za Mungu au GIZA? yaani sipati picha hapa unamaanisha nini wangewezaje kuzuia ajali isitokee kutoka kwenye gari tofauti?

Hivi kwenye speed ya 120km/hr unashindwa kukwepa LORI? du madereva tusaidie isijekuwa huyu dreva aliover take bila ya kuwa makini alafu mnataka kusingizia yaani kila tukio mnataka kulihusisha na mafisadi? KESHO MVUA ZITAKOSA NJI NZIMA NA MTASEMA KUNA MKONO WA MTU

WAKE UP PLEASE!!!!!
 
Yote tumuachie Mungu maana ndie anapanga yote. Na huyo driver hatapatikana kama yule aliyomuua Hon. Mbatia. Kama ni kweli kulikua na askari polisi kwenye coaster them ni maajabu kwamba hawakufuatilia lile lorry.
Naamini Mungu wetu sote ni mkubwa na ndiye alipanga Mh. na driver wapone waeleze ajali ilivyokua
 
Watanzania tuache tabia ya kusingizia maderefa wa magari makubwa, kila siku wao ndio wanasingiziwa kuwa ndio vyanzo vya ajali barabarani.

Sasa mwakyembe anasema kuna mkono wa mtu kivipi??
 
Back
Top Bottom