Wakuu ...jamani tupeni uptodates au?
hakuna habari za uhakika huko?
"Huko" wapi tena Mkuu? Wewe uko wapi mkubwa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakuu ...jamani tupeni uptodates au?
hakuna habari za uhakika huko?
No no no, dereva tulishamsikia. "Mheshimiwa" amesema nini?
TBC wamesema dakika 30 zilizopita Mkuu ndo katoka hospitali. Sasa ulimsikia on bed side interview hospitali?
Mheshimiwa Mwakyembe ameweza kuongea leo, yeye amesema amemwachia Mungu kwa maana yeye ni Mkristo na kama ilikuwa ni ajali ya kawaida basi anamwachia Mungu na kama kuna mkono wa mtu yaani hiyo ajali ilikuwa planted basi anamshitakia Mungu,
ameweza kudeclair yeye mwenyewe kuwa gari lake liligongwa kwa nyuma ingawa anasema liligongwa kidogo kwenye taa ya nyuma
...likaongeza motion ya gari lake na dereva waka akapanic baada ya kuona hawezi kulimudu ndo akalitoa nje ya road reserve
.. sasa hapa nafurahi mno kusikia yeye mwenyewe amesema hivyo sijui kamanda Nyombi ataendelea kushikilia msimamo wake kuwa tairi imechomoka dah...
una maana gani ya kutumia quote on quote "mheshimiwa"?
Leo Dk Mwakyembe kazungumza. Nimemsikia akisema kuwa walikuwa wakijaribu kumpita dereva wa lile lori lakini wakati dereva wa lori lile hakuwa anataka apitwe na gari ya Mwakyembe! Na walipokuwa wakimpita aliongeza mwendo na kusababisha kugongwa na lori kwa nyuma na hivyo kusukumwa na kupinduka. MAelezo ya Dk Mwakyembe yanashabihiana na maelezo ya Dereva wake ambyo niliyachukia kama ni kujitetea tu kwa uzembe wake.
Ni mapenzi ya Mungu, tumuachie Mungu.
Yeye mwenyewe Mwakyembe ame hinti hinti kuna mkono wa mtu, eti anamwachia Mungu
Tunamwombea apone upesi arudi katika majukumu ya kila siku nafkiri pia watoto na familia yake wapewe uangalizi na faraja katika siku kama hizi' tuwaamini madaktari wetu na tuepuke dhana zisizo na msingi na ambazo hata tukishikia hazitatua! Kama ipo ipo tu ndugu zangu, hakuna tukio au suala pasina sababu, 2jipe moyo na 2ongeze mapambano kama si leo basi kesho, yeye aliweza basi nasi tutaweza kwani wao wana nini? Tusonge!
Yeye mwenyewe Mwakyembe ame hinti hinti kuna mkono wa mtu, eti anamwachia Mungu
Nani sasa unasema aupuke dhana zisizo na msingi? Cheki hii posti.
"Huko" wapi tena Mkuu? Wewe uko wapi mkubwa?
Nani sasa unasema aupuke dhana zisizo na msingi? .
- Ni mapema mno, kunahitajika muda kidogo kupata facts zote ila hatuwezi ku-rule out anything kwa sasa, ingawa ni mapema mno ku-speculate!
FMES!
Kinacho nishangaza mimi ni kuwa wakati ajali inatokea, kulikuwa na basi (Dr. Mwakyembe ameita coaster, nadhani hakuona vizuri) ndani ya hilo basi kulikuwa na askari wa usalama bara barani wawili (Two Traffic Police). Hao askari ndo waliookoa mali na nyaraka za Dkt. Mshangao wangu ni kwanini hawakufanya jitihada za kuzuia lori linalohusika na ajali hata kwa kuwapigia simu askari wenzao? Kama dereva wa lori hatapatikana, nitaunga mkono shaka hii.