Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

client

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2015
Posts
667
Reaction score
870
Nimepata habari isiyo na shaka kuwa gari aina ya coaster limeua watoto karibu wote waliokuwa wanaelekea mjini Karatu kwa ziara ya kimasomo including(joint examinations), taarifa zinasema wamebaki watoto(3) tu wengine wamefariki,

shule inaitwa Lucky Vincent Nursery & Primary School ipo Arusha ni medium schools,kwa wenye updates tunaomba mtupe
.............
UPDATES:Ajali imetokea mlima marera kijiji cha rhotia,km chache sana kutoka Karatu mjini,mlima huo una mteremko mkali na daraja na pia kulikuwa na ukungu

Picha: Soon nitaziapload ni ajali ya muda huu
Mungu awalaze mahali pema peponi
----------------------

UPDATE: Coaster inasadikiwa kuwa na zaidi ya abiria 30 na wote wanasadikiwa wamefariki,maiti zimepelekwa hospitalini na watu wameondoka eneo la tukio,mvua inanyesha

UPDATE: Picha zinakuja soon ripota yuko eneo la tukio..


.........................
UPDATES:Magari ya polisi yametanda kila kona na maiti zimebebwa na magari ya polisi
Tayari kuhifadhiwa
...................
UPDATES:Ni watoto watatu (3) wanasadikiwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasiwasi vifo vikaongezeka
UPDATES:Lucky vincent nursery school bus
UPDATES:Shughuli za uokozi

UPDATES:Gari lilikuwa na zaidi ya abiria 30 wanafunzi 25,waalimu (4) wote wa kiume na dereva 1
................
UPDATES:Kati ya majeruhi watoto watatu(3) wawili wako mahututi kabisa na mmoja amepasuka kichwa
................
UPDATES:Maajabu ya ajali hakuna damu zozote zilizotapakaa licha ya watu wengi sana kufa!
..................
UPDATES:Majeruhi mmoja kati ya( 3) amefariki kabla ya kufikishwa hospitali,kwa hiyo taarifa zinasema wamebaki majeruhi wawili walioko ICU
...............
UPDATES:Kuna mkanganyiko mwingi kuhusu chanzo cha ajali ila nature ya eneo la ajali ni mteremko mkali na kuna daraja,ni eneo ambalo dereva anatakiwa kuwa makini kabisa,kwa dareva asiyemwangalifu inaweza tokea lolote,hebu angalia hapo gari lilipotumbukia na haikuwa ina over take ,u can diagnose the nature of an accident
UPDATES:Mwonekano wa gari kwa mbele baada ya kupata ajali

UPDATES:RPC Wa arusha amethibitisha jumla ya vifo 31 vya waalimu na wanafunzi
...................
UPDATES:Taarifa kutoka mjini Karatu zinasema kuwa majeruhi hali zao ni mbaya zaidi na wanakimbizwa hispitali ya rufaa ila mtoto mmoja ni mzima
...............

UPDATES:Mtoto pekee alienusurika amesimulia chanzo cha ajali na amesema kuwa gari lilifeli break tokea mwanzo wa kushuka mlima hali iliyopelekea watoto na waalimu kupiga makelele na kilichofuata ni gari kupaa na kupinduka kwani nature yake sio slope kivile kuna miinuko kidogo

My take:Kulingana na maelezo hayo inaonekana gari lilifeli break,kupoteza mwelekeo na kupinduka ingawa bado polisi hawajatoa taarifa za chanzo cha ajali Bali walitaja idadi ya vifo 31 tu
...............
UPDATES:Majina ya waliofariki



MUNGU AWALINDE NA KUWAREHEMU ITS SO SAD


R.I.P all

Client:Jf member
 

Attachments

  • 1.jpg
    41.7 KB · Views: 674
  • 4.jpg
    33.6 KB · Views: 787
  • 2.jpg
    28 KB · Views: 340
Wakuu habari za leo,

Muda huu kuna ajali mbaya imetokea maeneo ya karatu basi la shule limeanguka kabla ya kuingia karatu mjini na kuua watoto wengi ambao idadi yake bado haijafahamika. Wanafunzi hao wanaokadiriwa kuwa wa darasa la 7 inasemekana ni wa shule inayoitwa Lucky Vicent ya Arusha ambao walikua wanaenda karatu kufanya mitihani ya mashindano na shule za karatu. Kwa mujibu wa shuhuda basi hilo lilikua limebeba watoto zaidi ya 40 na wengi wao (zaidi ya nusu) inasemekana wamepoteza maisha akiwemo dereva na walimu.

Ntawapa updates soon nipo jirani na eneo la tukio na mvua inanyesha sana nimeshindwa kutoka kufika eneo la tukio.
Tuendelee kuwaombea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…