Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

RPC Charles Mkumbo wa Mkoa wa Arusha kutoa taarifa za awali kwani ni mpaka ufike mwenyewe eneo la tukio unapo mjibu mtangazaji wa ITV kuwa huwezi kutoa majibu ya kubuni kwani Karatu hakuna msaidizi wako ambaye ni OCD au msaidizi wa OCD ambaye lazima akupe taarifa iliyokufa utoke Arusha kuelekea Karatu!!!

Ma RPC mbadilike ktk kutoa taarifa kwa umma hasa za awali then kuna taarifa za tukio zima baada ya kufika eneo la tukio.

Sasa ikitokea ajali mbaya Ngorongoro 400kms kutoka Arusha hizo taarifa mpaka Ngorongoro baada ya saa 12 ndiyo utoe taarifa za awali wakati unawaza kupata taarifa kutoka kwa OCD.

Ajali ni mbaya na inaonekana Driver ni mgeni na njia na hakuchukua tahadhali pale Rhotia eneo la tukio kuna mteremko mkali na korongo!!

MUNGU awape nguvu majeruhi wapone haraka na kuwapa moyo wa uvumilivu wazazi ktk kipindi hiki kigumu cha majonzi

R.I.P Watoto wote waliofariki
RPC yupo sahihi,kauli ikikosewa huleta shida,basi wangemuhoji huyo OCD mkuu.
 
TAMKO LA UMOJA AS WA WATOTO
"SISI NI MWENYEZIMUNGU NA KWAKE NI MAREJEO YETU"
BARAZA UONGOZI NA MSHIKAMANO WA WATOTO DUNIANI LINAWATOA HOFU WATOTO WOTE ULIMWENGUNI KWAMBA VIFO VYA WATOTO NA WALIMU HUKO ARUSHA VIMETOKANA NA AJALI MBAYA YA GARI NA SI VINGINEVYO.TUKIWA TUNASUBURI TAMKO RASMI LA POLISI .

BARAZA LIMESIMAMISHA SHUGHULI ZA UMOJA KWA SIKU SABA NA VENDERA YETU HAITAPEPEA KWA MUDA HUI.
UMOJA WA WATOTO UNAWAOMBA WATOTO KUENDA SHULE KAMA KAWAIDA NA MITIHANI YA KITAIFA IENDELEE KAMA KAWAIDA DUNIANI KOTE."MUNGU ATUPE SUBURA NA UVUMILIVU KWA KUONDOKEWA NA WANACHAMA WENZETU AMBAO NI WAPENDWA WETU"

BARAZA LINATOA POLE KWA SHULE HUSIKA,WAZAZI,NDUGU NA JAMAA WA MAREHEMU" MOLA AZILAZE MAHALI PEMA NAFSI ZA MAREHEMU.
CHIFU CHAKACHENE ISMAIL ALLY IBRSHIM
FOUNDER AND GEAD OF WORLD CHILDREN UNION
 
badilisha mind set yako,hilo tatizo ulilonalo ni sababu hauamini kuwa kuna anaye monitor maisha ya binadamu wote,haya maisha yetu MUNGU kayapanga,usidhani unaweza kuepusha kitu MUNGU alichopanga kwa akili yako.

mwanao angeweza kuwemo humo wakafa wote akapona yeye.Waache wanao wawe huru acha imani potofu,utakufa kwa presha.

hakuna unachoweza kukiepusha wewe MUNGU anachopanga,wala sisemi uwe careless.

MUNGU anaweza akakupa mtihani sehemu usioitegemea.
Nakubaliana na wewe mkuu ila ni roho tu ya uchungu wa mzazi,na pia migodini viwandani na hata kwenye gesi kuna safety analysis kabla ya kuanza kazi yoyote,pia accidents zinazoweza kutokea,na jinsi ya kujikinga au tahadhari za kuchukua.sisi Mara nyingi katka maisha tuliyozowea hatufanyi Hays yote mwisho kabisa hata near miss inatakiwa kuwa reported maana near miss ya Leo inaweza kuwa incident au accident kesho kuna ajali naimani zilishatokea eneo hilo zamani zikapimwa na makosa kutupiwa madereva kma Leo,lakini serikali ibebe lawama za kutoweka zile bar za kwenye kingo za barabara,najua haxitaweza kuzuia ajali lakini gari hazitadumbukia labda.
 
b3aad0707bd68839502ed059ff00de80.jpg

Picha ya watoto waliofariki leo, ilipigwa wakati wanasubiria magari ili waondoke. Tunaweza kuitumia kama profile picha zetu kwa mda huu wa maombolezo.
RIP OUR SONS AND DAUGHTERS
Ukiangalia hii picha kwa makini.....utagundua jambo....wamekaa kiuzuni
Huyu alikuwa kwenye bus la nyuma sio lililopata ajali.gari lililopata ajali majeruhi wako mahututi
Nilitaka kushangaa....amekuwa discharged haraka hivyo bila a thorough medical checkup....na counselling
 
Wanangu mpumzike kwa amani,MUNGU AWAPE PUMZIKO LA AMANI,POLENI SANA WAZAZI WENZANGU NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA.
 
Ombi wasanii wetu kuonyesha mmeguswa na msiba huu watungieni watoto wetu (marehemu)japo wimbo mmoja wakuwafariji wazazi wa marehemu na watanzania kwa ujumla. Ni msiba mkubwa mnoo.arushanzima ni simanzi
 
RPC yupo sahihi,kauli ikikosewa huleta shida,basi wangemuhoji huyo OCD mkuu.
OCD hana mamlaka ya kuzungumzia jambo kama hilo....ni RPC pekee...kama hayupo kuna utaratibu....wa kufata sio kila mtu anaongea tu.....labda kama amepewa ruksa
 
OCD hana mamlaka ya kuzungumzia jambo kama hilo....ni RPC pekee...kama hayupo kuna utaratibu....wa kufata sio kila mtu anaongea tu.....labda kama amepewa ruksa
Kwa hyo RPC alikuwa aongee kabla hajafika eneo LA tukio?
 
b3aad0707bd68839502ed059ff00de80.jpg

Picha ya watoto waliofariki leo, ilipigwa wakati wanasubiria magari ili waondoke. Tunaweza kuitumia kama profile picha zetu kwa mda huu wa maombolezo.
RIP OUR SONS AND DAUGHTERS
[emoji24] [emoji24] [emoji24]
 
Pole sana wafiwa. Mungu awape wepesi katika kipindi hiki kigumu.

However, CCM na serikali yao walaumiwe sana kwa kukusanya kodi nyingi sana na kuzitumia kununua ndege badala ya kuimarisha barabara za wananchi. Kama barabara hii ingekuwa imara ajali hii iliyopoteza roho za wapendwa wetu isingetokea.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Nimepata habari isiyo na shaka kuwa gari aina ya coaster limeua watoto karibu wote waliokuwa wanaelekea mjini Karatu kwa ziara ya kimasomo including(joint examinations), taarifa zinasema wamebaki watoto(3) tu wengine wamefariki,

shule inaitwa Lucky Vincent Nursery & Primary School ipo Arusha ni medium schools,kwa wenye updates tunaomba mtupe
.............
UPDATES:Ajali imetokea mlima marera kijiji cha rhotia,km chache sana kutoka Karatu mjini,mlima huo una mteremko mkali na daraja na pia kulikuwa na ukungu

Picha: Soon nitaziapload ni ajali ya muda huu
Mungu awalaze mahali pema peponi
----------------------

UPDATE: Coaster inasadikiwa kuwa na zaidi ya abiria 30 na wote wanasadikiwa wamefariki,maiti zimepelekwa hospitalini na watu wameondoka eneo la tukio,mvua inanyesha

UPDATE: Picha zinakuja soon ripota yuko eneo la tukio..

19a4fcd1c935e4c031670cd880a46bc5.jpg

.........................
UPDATES:Magari ya polisi yametanda kila kona na maiti zimebebwa na magari ya polisi
Tayari kuhifadhiwa
...................
UPDATES:Ni watoto watatu (3) wanasadikiwa wako hai ila wako mahututi kabisa na kuna wasiwasi vifo vikaongezeka
UPDATES:Lucky vincent nursery school bus
62d62ef75dec257e496254f5cfb2808e.jpg

UPDATES:Shughuli za uokozi
a198eaa3cab45eec73b51943888b0a63.jpg

UPDATES:Gari lilikuwa na zaidi ya abiria 30 wanafunzi 25,waalimu (4) wote wa kiume na dereva 1
................
UPDATES:Kati ya majeruhi watoto watatu(3) wawili wako mahututi kabisa na mmoja amepasuka kichwa
................
UPDATES:Maajabu ya ajali hakuna damu zozote zilizotapakaa licha ya watu wengi sana kufa!
..................
UPDATES:Majeruhi mmoja kati ya( 3) amefariki kabla ya kufikishwa hospitali,kwa hiyo taarifa zinasema wamebaki majeruhi wawili walioko ICU
...............
UPDATES:Kuna mkanganyiko mwingi kuhusu chanzo cha ajali ila nature ya eneo la ajali ni mteremko mkali na kuna daraja,ni eneo ambalo dereva anatakiwa kuwa makini kabisa,kwa dareva asiyemwangalifu inaweza tokea lolote,hebu angalia hapo gari lilipotumbukia na haikuwa ina over take ,u can diagnose the nature of an accident
efc42e9814d84a123b6aa5a8a92fed7c.jpg

UPDATES:Mwonekano wa gari kwa mbele baada ya kupata ajali
1b9b2ef92a5648b20c71d3e04a5e5f65.jpg

UPDATES:RPC Wa arusha amethibitisha jumla ya vifo 31 vya waalimu na wanafunzi
...................
UPDATES:Taarifa kutoka mjini Karatu zinasema kuwa majeruhi hali zao ni mbaya zaidi na wanakimbizwa hispitali ya rufaa ila mtoto mmoja ni mzima
6d688744c79e95ed10fb0d0ea09e695e.jpg

...............

UPDATES:Mtoto pekee alienusurika amesimulia chanzo cha ajali na amesema kuwa gari lilifeli break tokea mwanzo wa kushuka mlima hali iliyopelekea watoto na waalimu kupiga makelele na kilichofuata ni gari kupaa na kupinduka kwani nature yake sio slope kivile kuna miinuko kidogo

My take:Kulingana na maelezo hayo inaonekana gari lilifeli break,kupoteza mwelekeo na kupinduka ingawa bado polisi hawajatoa taarifa za chanzo cha ajali Bali walitaja idadi ya vifo 31 tu
...............
UPDATES:Majina ya waliofariki
470862a5c10126e56155ee706126acdd.jpg

fbf2939173eaa07ff41af774c40b5eed.jpg


MUNGU AWALINDE NA KUWAREHEMU ITS SO SAD
d60caf7575f56820b6c8c35459ed5a35.jpg


R.I.P all

Client:Jf member
Mungu awalaze mahali pema pepon[emoji24] [emoji24]
 
Back
Top Bottom