Pole zetu watanzania wote kwa msiba huu mzito. Nimeona baadhi ya nyuzi zimehusisha nguvu za giza/mashetani kwenye hili!! Nashindwa kuelewa mtu unachambuaje na kufikia kuwa only reason ni mashetani!!
Kuna mambo mengi ambayo yako wazi kabisa kuwa ndio visababishi vikubwa vya ajali. Visababishi vikubwa 3 vya ajali za barabarani popote ni:
1. Binadamu(Dereva wa chombo cha moto, mwendesha baiskeli, mtembea kwa miguu nk).
2. Chombo cha usafiri
3. Barabara
Nadhani kabla hatujaenda huko kwa mashetani na majini, tuangalie kwa kiasi gani nchini kwetu tumedhibiti visababishi 3 vikuu vya ajali za barabarani!
Sio siri kuwa kuna wenzetu wanakuwa na leseni mfukoni kabla hata hajajua jinsi ya kuwasha gari, ila leseni zenyewe ni genuine 100% zimetolewa na mamlaka husika kwa utaratibu usiofahamika. Inakuwaje mtu hajaenda hata driving school ya siku moja apewe leseni? Ina maana huyo hafanyi mtihani wa nadharia wala road testing for competency! Hapa tutegemee nini? Tukubaliane kuwa ni mashetani wanachukua roho za ndugu zetu? Kwenye sehemu za kunywa pombe jioni magari binafsi ni mengi kuliko taxi, na hakuna anaekunywa akaliacha gari lake kwasababu amelewa ili aende nyumbani kwa kutumia taxi! Na akikamatwa na wasimamiaji sheria za barabarani kalewa huku anaendesha mwisho wake siujui! Na hata akikamatwa kijana anaendesha gari bila kuwa na leseni (under age etc) mwisho wake siujui! Madereva wenyewe sisi hatuendi hospitali angalao kujua hali zetu kiafya walao hata mara moja kila mwaka, mtu anatembea na high blood pressure(BP) au kisukari huku hajitambui, au hata macho hayaoni ila kwake sio issue mpaka stroke impige akiwa barabarani speed 100Km/h on busy road, bado mashetani ndio guilty?
Wengi wetu magari tunayoagiza ni mitumba, lakini hata gari lingekuwa jipya bado linahitaji planned preventive maintenance yenye ratiba. Sisi gari hadi liharibike ndio tutakimbizana kwa mafundi. Mara ngapi unakuta gari barabarani tairi limeng'oka kabisa na rim yake kisa ball joints zimeisha, ila kabla ya hapo kila gari likiingia kwenye mashimo si makelele ya suspension hayo but hatujali. Angalao tumekewa wiki ya usalama barabarani kila mwaka ila magari yetu yote yakaguliwe for roadworthness na baada ya kudhibitishwa tupewe sticker kuwa gari letu limekauliwa na liko salama tena kuingia barabarani kwa mwaka mzima uliopo mbeleni. Nani anathibitisha hapa jamvini kuwa gari yake imewahi kukaguliwa na motor vehicle inspector kabla ya "kupewa" sticker ya ukaguzi kuwa "passed"? Na hii haijalishi ni gari la mizigo au abiria japo kwa vyovyote ni hatari kwa watumiaji wenzako wa barabara. Lakini ole wako msimamizi wa sheria za barabarani akusimamishe saa sita ya mchana chalinze ukiwa safarini kwenda mbeya halafu akute gari yako haina sticker ya usalama barabarani, utajuta. Kweli tuko makini?
Serikali inajitahidi kujenga barabara nzuri kwa kiwango cha lami ila barabara hazikawii kuharibika. Zinaharibika kwasababu kuna wenzetu wanaruhusu magari ya mizigo kupitisha uzito uliokatazwa ama mara nyingine viwango hafifu vya ujenzi, Zinapoharibika huchukua muda mrefu kutengea fedha za matengenezo ilihali zinaendelea kutumika. Pamoja na ubovu wa barabara, wingi wa magari unaongezeka kila kukicha na kuongeza density ya magari kwenye miundo mbinu isiyoongezeka na iliyochakaa. Mabango ya alama za barabarani kwenye sehemu za hatari tunayang'oa na kuuza chuma chakavu. Kwenye speed limits kutokana na hazards za barabara hatufuati, sanasana tunatumia smartfones kutuhabarisha zilipo tochi za traffic ndio tupunguze mwendo. Halafu tunaziita kuwa ni ajali? Barabara za mijini hazina hata vituo vya basi, watu wanaruka huku mabasi yakipunguza mwendo tu. Sasa hizo barabara za vumbi ndio usiombee kwa maana hazina hata speed limits. Mwaka jana April nilisafiri kwenda tandahimba kutoka mtwara, dah nilikuwa napigwa overtake za 120Km/H OFF-ROAD!!!! Sijui wana roho gano madereva wa mabasi yale na abiria zao. Na abiria ndio makondoo kabisa, ikishatokea ajali hawaishi kulaumu mwendokasi wa dereva, abiria 55 wanaburuzwa na dereva mmoja dar-mwanza wala hamna anayekemea hadi yawafike!
Visababishi vinginevyo - BODABODA, yaani hawa kama vile wameachwa wafe waishe kumbe akifa mmoja wanatokea wawili mkesho yake, nguvukazi ya taifa inaangamia. Mwaka 2007 nilikuwa Douala, Cameroon. Ule mji ulikuwa hauna daladala; kule ni bodaboda na taxi. Ajali ya bodaboda kule ni nadra sana, kwanini? Kule madereva wa magari na boda wanafanya full driving course wanatofautiana kwenye daraja za leseni wanazopewa. Kwa hiyo ufahamu wa sheria za barabarani kati ya dereva na bodaboda huko Douala hauna tofauti kabisa. Sasa hapa kwetu hali ikoje? Mwendesha baiskeli anafundishwa kuendesha pikipiki kwenye uwanja wa mpira jioni halafu asubuhi yuko kituo cha daladala anasubiri abiria! Matokeo? Yaani hata hajui kwanini anatakiwa aendeshee upande wa kushoto huko barabarani! Kwenye traffic lights mbele ya askari wa usalama barabarani bodaboda huwa hawasubiri kijani, wanakatiza na nyekundu na askari wanawaangalia tu kila mara mpaka imekuwa ni mazoea au haki 'SPESHO' za mabodaboda - tunawafundisha nini? Je kuna shetani hapa? Naona kama mashetani ni sisi wananchi wenyewe, na hasa zaidi wanaosimamia sheria za usalama barabarani. Wao sasa wamegeuza faini kama kukomoa madereva, hata kama huna kosa unabambikwa(imenitokea ila nikagoma kulipa), sijui ni ili unegotiate nao uache "ya kusafisha kiatu" au la!
Kwa kumalizia, majeruhi wengi sana wanapoteza maisha kwa kukosa huduma za kwanza za dharura kabla ya kufikishwa hospitali(Pre-Hospital EMERGENCY MEDICAL SERVICES-EMS). Hata tunyooshe yoote yaliyotajwa hapo juu, kama hatutakuwa na EMS kwenye barabara zetu basi tutapunguza idadi ya ajali tu na sio vifo vinavyozuilika. Ni muhimu kabisa kwa serikali ikishirikiana na wadau wote kuhakikisha EMS inaanza sasa kwenye njia zote kuu kwa kuanzia.
In short mimi nadhani tusahihishe haya yaliyo wazi kabisa tuwe kwenye mstari then tuangalie impact, kama ajali/vifo vitaongezeka ilhali yote haya tumeyasimamia 100% basi nitakupa lift twende sumbawanga tukatafute "Daktari" wa kudhibiti mashetani (with a light touch). Zaidi ya watanzania 11,000 wamepoteza maisha yao kwenye ajali za barabarani kati ya mwaka 2014-2016, TANZANIA BILA AJALI INAWEZEKANA.
Potezea TYPOS