Ajali ya Happy Nation yaua Hakimu na mume wake Bukoba

Ajali ya Happy Nation yaua Hakimu na mume wake Bukoba

Wapumzike kwa amani. Ila Polisi bwana kwa maelezo yao hapo dereva wa Happy Nation hana kosa. Ndio umuhimu wa kuwa na camera za barabarani huyo mshenzi aliyewasukuma angedakwa kirahisi tu.

Lengo la kumuweka mtu rumande ni pamoja na kulinda maisha na uhai wake ili asidhuriwe na wale walioumizwa na tukio la ajali
 
Wenda hakimu alikuwa anaenda kumuhukumu mtu kifo au kumpeleka gerezani kwa kumbambikiza kesi

Bas mtuhumiwa akamuwai
Hakimu kufa huwa kirahis hvyo mchezo umechezwaa

Au hakima amekuwa akihiahirsha kesi za watu na huku ushaidi umekamilika sas wamemfanyiaa

All in all poleni wafiwa wote
 
Wazazi kuondoka kwa wakati mmoja ni pigo kubwa sana kwa watoto. Na huenda maisha yao ndo yameanza rasmi kwenda mrama...
Bahati nzuri mwenye mamlaka ya kutoa roho ya Mtu ni Mungu pekee na kila jambo hufanyika kwa wakati kwa makusudi ya mbingu pekee, ndiyomaana kifo ni fumbo.

MATHAYO 10:28.
Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.

MUHUBIRI 3:1-15.
 
Barabaran kuna ujinga sana

Dereva hana kosa lakin kakamatwa na atatoa hela nying tu mpaka kumaliza hyo kesi na akitoka anakosa ajira anaanza tena kutafuta

Mimi kuna liboda boda lilishika brek kwa nguvu likateleza likaja upande wangu nikalikwepa ila likajigonga kwenye body,nikasimama kusikilizia,wanazengo walipokuja naambiwa nimpeleke hospital mara polisi nikaambiwa nitengeneze pikpik na kuhudumia mpaka atakapopona likidonda nalo limegoma kupona heri ningekimbia tu siku hyo
Pole mkuu[emoji28]
 
Polisi acheni uonezi Dereva wa basi kosa lake ni nini hadi mnamshikilia?
 
Barabaran kuna ujinga sana

Dereva hana kosa lakin kakamatwa na atatoa hela nying tu mpaka kumaliza hyo kesi na akitoka anakosa ajira anaanza tena kutafuta

Mimi kuna liboda boda lilishika brek kwa nguvu likateleza likaja upande wangu nikalikwepa ila likajigonga kwenye body,nikasimama kusikilizia,wanazengo walipokuja naambiwa nimpeleke hospital mara polisi nikaambiwa nitengeneze pikpik na kuhudumia mpaka atakapopona likidonda nalo limegoma kupona heri ningekimbia tu siku hyo
Nchi yetu ina watu majinga sana.
Ndio maana nikiwaza wakati mwingine naona sawa tu walamba asali wanavyotukomesha...maana kuna mijinga mingi sana nchi hii.
Pole sana mkuu
 
Polisi mkoani Kagera inamshikilia dereva wa Basi la Happy Nation, Shaaban Khatibu 38 mkazi wa Dare es Salaam akidaiwa kusababisha vifo vya watu wawili.

Tukio hilo inadaiwa lilitokea Barabara ya Biharamulo, Kata Ijuganyondo, Manispaa ya Bukoba, Jumanne Desemba 6, mwaka huu majira ya saa 5.30 asubuhi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amewataja marehemu hao kuwa ni Geofrey John (42), mfanyabiashara na Tumaini Jofrey (41), ambaye ni hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kata ya Maruku.

Amesema Geofrey na Tumaini walikuwa wamebebana kwenye pikipiki, yenye namba za usajili T308CLH, ambapo walisukumwa na mwendesha pikipiki aliyekuwa amebeba magunia ya mkaa na kisha kuangukia uvunguni mwa gari la kampuni ya Happy Nation, yenye namba za usajili T70DFV, aina ya Youtong, inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Bukoba.

Amesema polisi inaendelea kumtafuta dereva wa pikipiki iliyokuwa imebeba mkaa na kwamba uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Katika mitandao mbalimbali ya Whatsapp ya mjini Bukoba, kulisambazwa ujumbe wa Tanzia ulioonesha umetoka Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba kwamba na ukieleza kifo cha hakimu huyo pamoja na mumewe kwa ajali ya gari, ingawa polisi haikusema kama ni mke na mume.

‘Tanzia: Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, inasikitika kutangaza kifo cha Tumaini John Kiyeyeu-C/No.11510783 Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kolekero, Bukoba na mme wake kilichotokea mchana huu kwa ajali ya gari na kupelekea wote kupoteza maisha. Tutaendelea kutoa taarifa kuhusiana na taratibu za mazishi,” unasomeka sehemu ya ujumbe huo.

HABARI LEO
Mikoa ya Geita na Kagera hakunaga Serikali barabarani. Mwisho wa kunukuu
 
Barabaran kuna ujinga sana

Dereva hana kosa lakin kakamatwa na atatoa hela nying tu mpaka kumaliza hyo kesi na akitoka anakosa ajira anaanza tena kutafuta

Mimi kuna liboda boda lilishika brek kwa nguvu likateleza likaja upande wangu nikalikwepa ila likajigonga kwenye body,nikasimama kusikilizia,wanazengo walipokuja naambiwa nimpeleke hospital mara polisi nikaambiwa nitengeneze pikpik na kuhudumia mpaka atakapopona likidonda nalo limegoma kupona heri ningekimbia tu siku hyo
Me kila siku huwa nasema, nikisababishiwa ajali ya kugonga, nikawa salama bila kupinduka na chombo kinatembea, kamwe sisimami na siripoti popote.

Walioajiriwa kwa kazi ya kupeleleza watafanya kazi yao kunipeleleza kwa kunitafuta ili tupambane kisheria mahakamani.

Unapofanya kosa kisha "ukajipeleka", ni upumbafu wako huo, unakuwa unawafanyia kazi watu na hakuna bonasi unayoipata kwa kujisalimisha.

Kuna ushenzi sana barabarani nishashuhudia na kufanyiwa mie!

Mtu mwingine akikamata chombo cha moto kuendesha utadhani kakatwa kichwa!
 
Back
Top Bottom