Ajali ya Happy Nation yaua Hakimu na mume wake Bukoba

Ajali ya Happy Nation yaua Hakimu na mume wake Bukoba

Polisi mkoani Kagera inamshikilia dereva wa Basi la Happy Nation, Shaaban Khatibu 38 mkazi wa Dare es Salaam akidaiwa kusababisha vifo vya watu wawili.

Tukio hilo inadaiwa lilitokea Barabara ya Biharamulo, Kata Ijuganyondo, Manispaa ya Bukoba, Jumanne Desemba 6, mwaka huu majira ya saa 5.30 asubuhi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amewataja marehemu hao kuwa ni Geofrey John (42), mfanyabiashara na Tumaini Jofrey (41), ambaye ni hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kata ya Maruku.

Amesema Geofrey na Tumaini walikuwa wamebebana kwenye pikipiki, yenye namba za usajili T308CLH, ambapo walisukumwa na mwendesha pikipiki aliyekuwa amebeba magunia ya mkaa na kisha kuangukia uvunguni mwa gari la kampuni ya Happy Nation, yenye namba za usajili T70DFV, aina ya Youtong, inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Bukoba.

Amesema polisi inaendelea kumtafuta dereva wa pikipiki iliyokuwa imebeba mkaa na kwamba uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.

Katika mitandao mbalimbali ya Whatsapp ya mjini Bukoba, kulisambazwa ujumbe wa Tanzia ulioonesha umetoka Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba kwamba na ukieleza kifo cha hakimu huyo pamoja na mumewe kwa ajali ya gari, ingawa polisi haikusema kama ni mke na mume.

‘Tanzia: Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, inasikitika kutangaza kifo cha Tumaini John Kiyeyeu-C/No.11510783 Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kolekero, Bukoba na mme wake kilichotokea mchana huu kwa ajali ya gari na kupelekea wote kupoteza maisha. Tutaendelea kutoa taarifa kuhusiana na taratibu za mazishi,” unasomeka sehemu ya ujumbe huo.

HABARI LEO
Kwa hiyo dereva wa bus amesababishaje vifo hapo?
 
Aisee hapo kama anakukomoa eti,



Ni muda gani sasa?
Miezi miwili sasa

Kuna muda huwa nakosa muda kuna boda wa huko huko alipo huyo mgonjwa huwa namtumia kumpeleka hospitali
Huyo dogo kuna siku alinipigia simu nakuniambia kuwa hawa watu wamepanga kukukomoa kwanini usiwazimie simu au kukataa kupokea simu zao na ukawapotezea mazima
 
Aisee hapo kama anakukomoa eti,



Ni muda gani sasa?
Miezi miwili sasa

Kuna muda huwa nakosa muda kuna boda wa huko huko alipo huyo mgonjwa huwa namtumia kumpeleka hospitali
Huyo dogo kuna siku alinipigia simu nakuniambia kuwa hawa watu wamepanga kukukomoa kwanini usiwazimie simu au kukataa kupokea simu zao na ukawapotezea mazima
 
Maisha mengine haya main road na pikipiki? Kuna vitu mimi siwezi kujaribu. Hawa wababeba mkaa na bodaboda wanatakiwa kufukuzwa kbs. Morogoro road wamejaa na trafiki wanaangalia tu.
 
Wenda hakimu alikuwa anaenda kumuhukumu mtu kifo au kumpeleka gerezani kwa kumbambikiza kesi

Bas mtuhumiwa akamuwai
Hakimu kufa huwa kirahis hvyo mchezo umechezwaa


Au hakima amekuwa akihiahirsha kesi za watu na huku ushaidi umekamilika sas wamemfanyiaa

All in all poleni wafiwa wote
mahakama ya mwanzo huhusika na makosa madogo madogo mtaani
wala hahusiki na kuhuku kifo wala mamiaka meeengi
Tusiwahukumu jamani hii ni ajali...tuwaombee kwa Mungu awasamehe makosa yao
 
Back
Top Bottom