Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ooh hii ni sad news.Polisi mkoani Kagera inamshikilia dereva wa Basi la Happy Nation, Shaaban Khatibu 38 mkazi wa Dare es Salaam akidaiwa kusababisha vifo vya watu wawili.
Tukio hilo inadaiwa lilitokea Barabara ya Biharamulo, Kata Ijuganyondo, Manispaa ya Bukoba, Jumanne Desemba 6, mwaka huu majira ya saa 5.30 asubuhi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amewataja marehemu hao kuwa ni Geofrey John (42), mfanyabiashara na Tumaini Jofrey (41), ambaye ni hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kata ya Maruku.
Amesema Geofrey na Tumaini walikuwa wamebebana kwenye pikipiki, yenye namba za usajili T308CLH, ambapo walisukumwa na mwendesha pikipiki aliyekuwa amebeba magunia ya mkaa na kisha kuangukia uvunguni mwa gari la kampuni ya Happy Nation, yenye namba za usajili T70DFV, aina ya Youtong, inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Bukoba.
Amesema polisi inaendelea kumtafuta dereva wa pikipiki iliyokuwa imebeba mkaa na kwamba uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.
Katika mitandao mbalimbali ya Whatsapp ya mjini Bukoba, kulisambazwa ujumbe wa Tanzia ulioonesha umetoka Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba kwamba na ukieleza kifo cha hakimu huyo pamoja na mumewe kwa ajali ya gari, ingawa polisi haikusema kama ni mke na mume.
‘Tanzia: Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, inasikitika kutangaza kifo cha Tumaini John Kiyeyeu-C/No.11510783 Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kolekero, Bukoba na mme wake kilichotokea mchana huu kwa ajali ya gari na kupelekea wote kupoteza maisha. Tutaendelea kutoa taarifa kuhusiana na taratibu za mazishi,” unasomeka sehemu ya ujumbe huo.
HABARI LEO
Sasa kama huyo boda alikuwa anataka apite katikati yetu wakati napishana na gari jingine,alivyokosa nafasi akaamua ashike breki wa nyuma kwa nguvuMtu mwingine akikamata chombo cha moto kuendesha utadhani kakatwa kichwa!
Hiyo tafsiri ya sheria. Usidhani kila mtu ni bwege humu kama wewe.Such a mere reason.
We kwa akili yako unaona hilo ni sahihi?
Na hela ya matumizi wampa?Barabaran kuna ujinga sana
Dereva hana kosa lakin kakamatwa na atatoa hela nying tu mpaka kumaliza hyo kesi na akitoka anakosa ajira anaanza tena kutafuta
Mimi kuna liboda boda lilishika brek kwa nguvu likateleza likaja upande wangu nikalikwepa ila likajigonga kwenye body,nikasimama kusikilizia,wanazengo walipokuja naambiwa nimpeleke hospital mara polisi nikaambiwa nitengeneze pikpik na kuhudumia mpaka atakapopona likidonda nalo limegoma kupona heri ningekimbia tu siku hyo
Mwanzo nilikuwa nampa ila nilivyoona siku zinakuwa nyingi nikasitisha,na anataka akipona kabisa nimlipe,nataka akipona nimkumbushe kuwa "unakumbuka ajari ulisababisha mwenyewe" sahv nishaona ni bora kwenda polisi tu au hata mahakamaniNa hela ya matumizi wampa?
Pole sana mkuu,hio situation ilishanitokea ukiangalia boda alikua na makosa,ila niligoma kutemgeneza pikipikiBarabaran kuna ujinga sana
Dereva hana kosa lakin kakamatwa na atatoa hela nying tu mpaka kumaliza hyo kesi na akitoka anakosa ajira anaanza tena kutafuta
Mimi kuna liboda boda lilishika brek kwa nguvu likateleza likaja upande wangu nikalikwepa ila likajigonga kwenye body,nikasimama kusikilizia,wanazengo walipokuja naambiwa nimpeleke hospital mara polisi nikaambiwa nitengeneze pikpik na kuhudumia mpaka atakapopona likidonda nalo limegoma kupona heri ningekimbia tu siku hyo
Ufutwe tu!..Bodaboda ni mojawapo ya usafiri wa hovyo sana.
Mbona pikipiki ina namba za gari?
Mungu awapumzishe kwa amani
Kwa umri huo kama wana watoto bado watakuwa tegemezi.... Nawaonea huruma sana....
Barabaran kuna ujinga sana
Dereva hana kosa lakin kakamatwa na atatoa hela nying tu mpaka kumaliza hyo kesi na akitoka anakosa ajira anaanza tena kutafuta
Mimi kuna liboda boda lilishika brek kwa nguvu likateleza likaja upande wangu nikalikwepa ila likajigonga kwenye body,nikasimama kusikilizia,wanazengo walipokuja naambiwa nimpeleke hospital mara polisi nikaambiwa nitengeneze pikpik na kuhudumia mpaka atakapopona likidonda nalo limegoma kupona heri ningekimbia tu siku hyo
Acha kujificha kwenye kichaka cha sheria we bwege. Nimekuuliza wewe kama wewe kwa mtazamo wako na si kwa mtazamo wa sheria. Tuna sheria ngapi kandamizi zinapigiwa kelele kila uchwao? Nani hajui tuna sheria nyingi za kibwege zinazohitaji amendments. Usiishi kwa kukariri kwa kilichoandaliwa na kuletwa mbele yako ukakimeza kama kilivyo bila ku digest mambo. Kichwa maji!Hiyo tafsiri ya sheria. Usidhani kila mtu ni bwege humu kama wewe.
Habari Yafo mmekuPole sana kwa familia zao
Aisee hapo kama anakukomoa eti,Mwanzo nilikuwa nampa ila nilivyoona siku zinakuwa nyingi nikasitisha,na anataka akipona kabisa nimlipe,nataka akipona nimkumbushe kuwa "unakumbuka ajari ulisababisha mwenyewe" sahv nishaona ni bora kwenda polisi tu au hata mahakamani
Ni kwel ila mahakimu huwa na dhambi sanaMbona pikipiki ina namba za gari?
Mungu awapumzishe kwa amani
Kwa umri huo kama wana watoto bado watakuwa tegemezi.... Nawaonea huruma sana....