Pole SanaSiku tatu hizi hajarudi anapoishi,wamemtafuta simu hapatikani,kazini kwake nao hawampati
Mwisho akakutwa mortuary hafai
Aliopolewa akiwa tayari kaenda
Unajua nlivopata taarifa ya Ile ajali mida ya asubuhi nlishinda siku yote najiskia hatia.mpaka najiuliza kwanini sipati jibu.najiskia vibaya tu na uzito ndani yangu
Tumekua wote,tumecheza wote,tumekula wote,moments nyingi tumeshea tukiwa karibu
Tabasamu lake,ni mtu asiejua kukasirika labda awe pissed off Kwa sana
Mizaha na utani wake.30 good years tupo wote.now mwendo kaumaliza
Mtu mnaongea mnacheka mda wote, anakwambia baadae basi kumbe ndo kwaheri.
Hakujua Nini kitatokea usiku Ule,hakuna aliejua
Ile barabara na kituo ndio njia ya uelekeo kazini.
Akajikuta mmoja wa wahanga bila kutarajia
Sitamuona tena
Waliosema hakuna ajuae kesho yake hawakukosea
Ushauri:ishini Kwa upendo sana guys,kuwa chanzo Cha furaha na tabasamu Kwa wote unaokutana nao,
Usimdharau mtu yeyote
Alienacho asie nacho wote wape heshima.
Usijivune
Usipungukiwe upendo na usimsahau Mwenyezi Mungu.
Moyo wangu unauma
Mungu akupe ujasiri