Ajali ya Kimara Stop Over kumbe kaka yangu naye alikuwepo!

Pole Sana
Mungu akupe ujasiri
 
Duh, hili swali mkuu, mtu hafati ajali, ajali inamfata.
Ngoja nikusaidie. Ukiuliza how come alikuwa eneo la tukio.
Kuna majibu matatu hapo

alikuwa bodaboda /eneo lake la kazi

Alikuwa mpita njia au

alikuwa abilia kwenye moja ya boda boda

Don't lose sight next time
 
Ile sehemu pale ni ngumu kuamini eti wamekufa watu watatu tu.
 
Pole sana
 
Pole sana kwa msiba.

Next time ukijiskia hali hiyo ya uzito kupitiliza ni muhimu uombe kuvunja hiyo hali, hiyo ingeweza kusaidia Kaka yako.
 
Ngoja nikusaidie. Ukiuliza how come alikuwa eneo la tukio.
Kuna majibu matatu hapo

alikuwa bodaboda eneo lake la kazi

Alikuwa mpita njia au

alikuwa abilia kwenye moja ya boda boda

Don't lose sight next time
Swali alikuwa anafanya nini eneo la tukio ndo lina haya majibu.

Swali la how come alikuwa eneo la tukio ni umeuliza ilikuwaje akawa eneo la tukio na ni swali linalomlenga mhusika ambaye alipaswa kuwa eneo jingine na si hapo.

Anyway, kama ndivyo ulichokuwa unamaanisha sawa nimekuelewa.
 
Pole sana
 
Nimefafanua msingi wa swali langu. Nadhani nimeeleweka
 
Such is life...nilipita hapo hiyo siku, muda mchache kabla ya hiyo ajali. Gari ilikuwa mwendo Kasi Nini? au kama si mwendo Kasi basi dereva alijichanganya mwenyewe.
 
Pole sana!Pia ahsante kwa ujumbe mzuri.
 
Ushauri: Ishini kwa upendo sana guys, kuwa chanzo cha furaha na tabasamu kwa wote unaokutana nao. Usimdharau mtu yeyote, alienacho asie nacho wote wape heshima.

Usijivune.
Usipungukiwe upendo.
Usimsahau Mwenyezi Mungu.

Moyo wangu unauma.
Pole sana Ndugu,
Huu ushauri wako umenigusa sana
 
Pole sana.....

Nakumbuka kuna kipindi usafiri wa "panton" ulikuwa unasumbua sana....watu wakawa wanavuka kutimia mtumbwi kwenda ng'ambo......

Kila nilipotaka kupanda ule mtumbwi moyo wangu unakuwa mzito sana....nikaghairi....

Ilivyoondoka na kati kati mtumbwi ukapinduka na kuuwa watu kadhaa nikishuhudia.......

Kifo hakibishi hodi......

MWANADAMU HATAKIWI KUKIOGOPA KIFO BALI KUJIANDAA NA MAISHA BAADA YA KIFO(KWA WENYE IMANI)
 
Ndiyo hivyo tena utasikia wanasiasa wakishangilia vifo vya wengine.
 
Pole sana kwa msiba.

Next time ukijiskia hali hiyo ya uzito kupitiliza ni muhimu uombe kuvunja hiyo hali, hiyo ingeweza kusaidia Kaka yako.
Mkuu mimi nadhani alijisikia hali hiyo isiyo ya kawaida kwake, baada seconds tu baada ya kakake kukata roho. Hivyo kuikemea ni sawa kwa ndugu zake wengine walio hai. Rest easy Abi's Brother.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…