Ajali ya Kimara Stop Over kumbe kaka yangu naye alikuwepo!

📌📌
 
Kuna watu wengi wanadhaniwa "Wameenda Dar hawataki hata kurudi wala kusalimia", kumbe inawezakana walishazikwa siku nyingi. Poleni
 
Idadi halisi ikiwekwa hapa mtakamatwa...elewa hivyo...poleni mkuu.
 
Amin
 
Pole mpendwa kifo ni kigumu
Ipo siku haya yote yatakoma kama tukiamini.
 
Pole sana mwanangu Abby
 
Mkuu mimi nadhani alijisikia hali hiyo isiyo ya kawaida kwake, baada seconds tu baada ya kakake kukata roho. Hivyo kuikemea ni sawa kwa ndugu zake wengine walio hai. Rest easy Abi's Brother.
Ni sawa na nilimwelewa mkuu, nachomaanisha hapa ni kuwa kama jambo baya kabisa liko karibu kutokea taarifa itakuja kwako mapema zaidi kabla ya tukio.

Kwa mfano unaweza ukataka kusafiri lakini unajiskia vibaya, mkuu hiyo ni taarifa unapewa.

Akikaa vizuri akakumbuka atakumbuka eidha ni uzito, waswas, ama huzuni alikuwa nayo hata kabla ya kaka yake kupata ajali, ndicho nazungumzia.

Inamaana Mleta mada ana kitu cha tofauti katika ulimwengu wa kiroho.

Kwa hivyo anapaswa kujiweka karibu na Mungu zaidi ili kitu hicho kijidhihirishe zaidi, kwa sababu sio kila mtu yuko hivyo mkuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…