Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

MBONA MNATISHA WATU WAKIONGEA FACTS? NANI ANAOGOPOA KIFO...KAMA WATU 200 WAMEKUFA WITHIN 2 DAYS IJE KUWA ZITTO AU MIMI AU FLANI? HASIKII UOGO WALA UKWELI.
 
Ajali ya Mv Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe Bado mawaziri?

Ni masikitiko makubwa kwamba, Serikali ya wanyonge imeokoa mtu mmoja, wakati wananchi wenyewe wameweza kuokoa watu 40..... hii ni aibu kubwa sana. Watu 225 wamepoteza maisha sababu ya uzembe.

Tuache kujidanganya na mapenzi ya Mungu. Mungu katupa akili, namna ya kuzitumia ni sisi wenyewe. Huwezi kupata Habari ya ajali saa nane mchana halafu ukaitisha Kamati ya Usalama mkoa saa 11 jioni ( yaani mwendo wa Dreamliner Dar-Mwanza mara 4 ). Rais naye hakuitisha Cabinet ya dharura wala Baraza la Ulinzi na Usalama Taifa kuratibu uokoaji. Uokoaji unasitishwa sababu ya GIZA? Tukihoji mnasema tunaleta Siasa? Nonsense!

Kwa nchi zilizoendelea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu walitakiwa wawe wamekwishafutwa kazi au wamejiuzulu wenyewe.

Miaka 57 baada ya uhuru...Jeshi la uokozi linapoishia kuwa jeshi la UOPOZI, ni wakati wa rafiki nyangu Kangi Lugola kupumzika. Waziri Kamwelwe, Jenista na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja. Bahati mbaya sana Rais amechoka na hivyo hajali tena. Wazembe Ndio wameongoza mazishi ya ndugu zetu leo.
Na wewe bado ni mbunge wakati Halmashauri yako mwaka huu ilipata hati chafu??
 
Hakuna hoja fikirishi hapa zaidi ya kutugeuza sisi wajinga, Huyu "Mpelesi" ni Mbunge, Kiongozi kila kitu anachofanya ni kwa Kodi yetu hata hii posti aliyotuma ametumia Kodi zetu, narudia Zitto ni Kiongozi Kama walivyo hao anaowataka wajiuzuru, ni ujinga kutuaminisha eti they are not part of this simply because they are from opposition, ukweli unabaki wote ni viongozi, Kama ni serikali imekwama yeye hawezi kujiondoa, unless otherwise aje hapa atueleze kwanini analipwa mshahara na Serikali!
kwa hiyo mm kama ni mwalimu na ww ni daktari wote tumeajiriwa na serikali. tuseme mm sikufundisha vizur, wanafunz wakifeli mtihani tutalaumiwa wote mimi na wewe kwa kuwa tunatumia kodi za wananchi?
 
Wametuziba midomo kwa nguvu ya pyupyupyu kwenye majukwaa ya kuikosoa serikali, sasa acha watu wapumulie kero zao kwenye mitandao ya kijamii kama hivi
 
Kinachonishangaza wakati wa maadhimisho ya sikukuu za kitaifa askari wetu huwa wanakuwa na maonyesho ya "Show of Force" kiasi sisi wanyonge huwa tunakuwa na imani kuwa janga lolote likitokea "we are safe"!
 
Super mafia Ninja kangi wa uloga hawezi jiuzuru kirahisi rahisi hivi
 
Zito umekwenda shule Na ni mjuzi wa kuchambua mambo kwa mapana na marefu lkn kwenye Jambo serious la nchi kunaleta siasa.
 
ACT wazalendo mmefanya nini kwenye zoezi la uokoaji?
 
Kujifanya mnauwezo wa kufikiri Lakini sijaona mkiogelea ziwani kuokoa ndiyo tuseme nyie ni zero ? Kama huwezi kitu usilaumu mwingine
 
Back
Top Bottom