Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

1, Na swali ile ajari ya Moto iliyotokea kwenye ile nnchi ya ulaya mawazili walijiuzuru? Au mamlaka husika inayosimamia?
2, Jitaidi utumie ujana wako kama kweli unawapenda Watanzania vijana waweze kupata fursa za ajira au buni kitu cha msingi umekaa attention mda wote kukosoa ni sawa na unajikita kutafuta mabaya ya mwenzio kwa staili hii tutafika? Ndo maana wabongo wamtoendelea
3, waliosababisha ajali ni Mawazili? au mamlaka husika ndo washughulikiwe?Aseee kuwa Makini
Hizo ni siasa tu,hamna kitu
Ndugu yangu miaka 20 sasa (1998-mv bukoba), na zingine nyingi hapa kati tuendelee kupeana tu pole bila kuambiana ukweli?. Lazima tuache ujinga wa kujisifia kuwa tuna uwezo wakati vitu vya msingi kama uhai wa RAIA wetu ni shida!
 
Na vijana wa rika lake waliopo serikalini wanajaza matumbo yao huku wanyonge wakiangamia na kufa maji, Bora yeye angalau anaona mbali kuliko hayo ambayo hata kushughulisha ubongo imekuwa ngumu.. ...Usitishe uokoaji kisa Giza . . .haiingii akilini, vuta picha angekwepo mama ake, au ndugu yake jee angesema tukalale paka kesho kukiwa na mwanga
Ona hizi akili, kwahiyo Kama vijana wenzake wakifanya upuuzi na yeye afanye upuuzi!
 
Pongezi ziwaendee wale wavuvi. Wamefanya kazi kubwa sana. Mitumbwi ya wavuvi ndio ilikuwa mingi eneo la tukio kuliko boti za jeshi letu la NAVY.

Huenda ni kiashiria kwenye mipaka ya maji kiulinzi hatuko vizuri

si wanasemaga kwa ukanda EAC sisi ndo tunaongoza kwa uimara wa majeshi jaman?
 
Kuna mambo yanakasirisha sana Nchi hii..
 
Pongezi ziwaendee wale wavuvi. Wamefanya kazi kubwa sana. Mitumbwi ya wavuvi ndio ilikuwa mingi eneo la tukio kuliko boti za jeshi letu la NAVY.

Huenda ni kiashiria kwenye mipaka ya maji kiulinzi hatuko vizuri
Unafikiri jeshi huwa linaenda tuu kufanya shughuli hizo za uokoaji, kuna taratibu zake kaka
 
Ajali ya Mv Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe Bado mawaziri?

Ni masikitiko makubwa kwamba, Serikali ya wanyonge imeokoa mtu mmoja, wakati wananchi wenyewe wameweza kuokoa watu 40..... hii ni aibu kubwa sana. Watu 225 wamepoteza maisha sababu ya uzembe.

Tuache kujidanganya na mapenzi ya Mungu. Mungu katupa akili, namna ya kuzitumia ni sisi wenyewe. Huwezi kupata Habari ya ajali saa nane mchana halafu ukaitisha Kamati ya Usalama mkoa saa 11 jioni ( yaani mwendo wa Dreamliner Dar-Mwanza mara 4 ). Rais naye hakuitisha Cabinet ya dharura wala Baraza la Ulinzi na Usalama Taifa kuratibu uokoaji. Uokoaji unasitishwa sababu ya GIZA? Tukihoji mnasema tunaleta Siasa? Nonsense!

Kwa nchi zilizoendelea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu walitakiwa wawe wamekwishafutwa kazi au wamejiuzulu wenyewe.

Miaka 57 baada ya uhuru...Jeshi la uokozi linapoishia kuwa jeshi la UOPOZI, ni wakati wa rafiki nyangu Kangi Lugola kupumzika. Waziri Kamwelwe, Jenista na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja. Bahati mbaya sana Rais amechoka na hivyo hajali tena. Wazembe Ndio wameongoza mazishi ya ndugu zetu leo.
Nasikitika sana kiongozi mkubwa kama wewe huna ufahamu jinsi gani Kamati za maafa zinavyofanya kazi au labda unaenjoy kukashifu Serikali na kuichonganisha Serikali na wananchi.

Naomba nikuulize maswali muhimu kwa niaba ya umma wa wapenda ukweli.

1-Unafahamu kamati ya maafa ya mkoa inaundwa na nani ?Mwenyekiti wa kamati hiyo ni nani?wajumbe wake ni kina nani?
Kwangu mimi kama kamati ya maafa ya mkoa ya Mwanza iliitishwa na kuwa active saa 10 basi mwenyekiti wake anastahili heshima kubwa kwa hili.

2-Unafahamu ni wakati gani au kwa tukio gani kamati ya maafa ya wilaya inaitishwa?

3-Unafahamu ni wakati gani kamati ya maafa ya mkoa inaitishwa au kwa lugha ya kitaalamu inakuwa activated?
4-Je ni wakati upi kamati ya maafa ya kitaifa inaitishwa?kwa vigezo vipi?
unawafahamu wajumbe wake?
Furthemore bwana mdogo Zitto
5-Unafahamu ni wakati gani kamati za maafa za kikanda au kimataifa zinaundwa?ni matukio ya aina gani yana-activate kamati tajwa?

Acha kupotosha umma kijana huu sio ushabiki wa liverpool na Southampton haya ni maafa na Taifa lipo msibani...
Eti unasema Serikali imeokoa mtu mmoja tu?...Hii ni insanity....hivi watu walinusurika walitibiwa na yule babu yako unayetishiaga naye watu au ACT Wazalendo?

Zitto do you know ABCs za uokoaji kwenye maji?Je una thamini usalama wa wataalamu wa uokozi au wataalamu wa kukabiliana na majanga?
Kwa nini basi kama uliona mambo hayaendi vizuri hukutoka huko majuu ulipo ili kuja kusaidia uokoaji Gizani?

Hivi Zitto nikuulize je pale Katika jimbo lako au wilaya yako wewe sio mjumbe wa kamati ya maafa ya wilaya au hata mkoa wenu? Je hufahamu au hujawahi kuhusishwa kwenye Maandalizi ya Disaster Management and preparedness.
Hakuna contigency plan ya kupambana na majanga katika wilaya yako?

Kama ipo kwa nini unaisema Serikali ni zembe?

Kama hakuna je tukulaumu kwa kukaa kimya?

Zitto ni kama vile unalazimishia kukamatwa na kuhojiwa ili upate kiki ya aina mpya yaani eti umekamatwa kwa kuhoji...huu ni utoto na sio siasa bali ni ubaradhuli na roho mbaya kwa wafiwa na waathirika wa tukio hili.

Hivi ukihojiwa na sisi wananchi utupe makosa specific kwa kila unayemlaumu utaweza kujibu?

Nakushauri utulie na usisake kiki ya kisiasa ...wananchi wa Ukara ndio wanaojua kilichotokea ...wanaelewa uzembe upo wapi na wanajua nani awajibike ndio maana kwa sasa wapo msibani na wanaomboleza.

You have been shifting your line of attack yaani mara urukie kwa Rais,Mara JWTZ,Mara mawaziri Mwisho utataka hadi kumtusi Mwenyezi Mungu.

Zitto hebu tumia busara kidogo na ujaribu kukumbuka tweet yako mojawapo ya tarehe 1 juni 2014 na ulinganishe walioyasema watanzania siku hiyo kwako na kwa umma. BASICALLY THEY DID NOT SAY WEWE NI MZEMBE!!

Ukiikumbuka siku hii vyema basi utaelewa thamani ya Mtu mmoja kuokolewa na Serikali.
 
Hivi zile radar zetu za kijeshi zina kazi gani? Maana kwa hali hii Kijiji cha mpakan kinaweza kuvamiwa tukachukua hatua kesho
 
Dont attack personality.

Discuss the topic. ZITTO YUPO SAHIHI KABISA. VERY CRITICAL.

Zitto kumwambia Kwanini Yeye hakuwajibika Kwa chama chake kufanya vibaya 2015 Ni issue ya personal ?

Unapata je ujasiri wa kumwambia Mwenzako ajiuzulu Kwa collective responsibility Wakat Wewe Mwenyewe hukufanya hivyo ?
 
Hakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!
Lakini ana hoja ya msingi! Huko Ulaya unapozungumzia wewe ingetokea ajali kama hii alafu watu wamekufa kizembe hivi sidhani kama kungekalika.
Raia wangeandamana kuiwajibisha serikali kwa uzembe uliosababisha haya maafa
 
Nina mashaka na maharamia kutumia ziwa victoria kutuvamia au kuingiza mambo yao kwa udhaifu wa kutokuwa na taa basi wangechukuwa hata za TRONIC
 
kwa hiyo mm kama ni mwalimu na ww ni daktari wote tumeajiriwa na serikali. tuseme mm sikufundisha vizur, wanafunz wakifeli mtihani tutalaumiwa wote mimi na wewe kwa kuwa tunatumia kodi za wananchi?
Mfano wako ni wa kijinga Sana, Zitto Kabwe ni Kiongozi wa Serikali Kama hao anaowataka wajiuzuru, aanze yeye kujiuzuru kwa sababu Kama serikali imefeli kwa Hili na yeye ni sehemu ya serikali, Zitto no Kiongozi kwenye level ya decision makers Hana tofauti na hao anaotaka wajiuzuru!
 
Asante sana mh Ruyagwa kwa mchango wako kwenye sakata hili lililo tuwacha na majonzi
Ajali ya Mv Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe Bado mawaziri?

Ni masikitiko makubwa kwamba, Serikali ya wanyonge imeokoa mtu mmoja, wakati wananchi wenyewe wameweza kuokoa watu 40..... hii ni aibu kubwa sana. Watu 225 wamepoteza maisha sababu ya uzembe.

Tuache kujidanganya na mapenzi ya Mungu. Mungu katupa akili, namna ya kuzitumia ni sisi wenyewe. Huwezi kupata Habari ya ajali saa nane mchana halafu ukaitisha Kamati ya Usalama mkoa saa 11 jioni ( yaani mwendo wa Dreamliner Dar-Mwanza mara 4 ). Rais naye hakuitisha Cabinet ya dharura wala Baraza la Ulinzi na Usalama Taifa kuratibu uokoaji. Uokoaji unasitishwa sababu ya GIZA? Tukihoji mnasema tunaleta Siasa? Nonsense!

Kwa nchi zilizoendelea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu walitakiwa wawe wamekwishafutwa kazi au wamejiuzulu wenyewe.

Miaka 57 baada ya uhuru...Jeshi la uokozi linapoishia kuwa jeshi la UOPOZI, ni wakati wa rafiki nyangu Kangi Lugola kupumzika. Waziri Kamwelwe, Jenista na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja. Bahati mbaya sana Rais amechoka na hivyo hajali tena. Wazembe Ndio wameongoza mazishi ya ndugu zetu leo.
 
Zitto ana hoja ya msingi. sidhani kama hawa mawairi watajiuzulu. naona kangi anahangaika kunyamazisha wanaokosoa juu ya ajali hii.
 
Wewe ulitaka asifie tu?kwanini msiheshimu mawazo yanayokinzana na mawazo yenu?
This is nonsense

Back
Top Bottom