Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

Ajali ya MV Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe bado Mawaziri?

Hapa kuna hoja fikirishi na za kufanyiwa kazi, this is constructive criticism atakayekasirika atakuwa ana upungufu mkubwa sana wa akili
Hakuna hoja fikirishi hapa zaidi ya kutugeuza sisi wajinga, Huyu "Mpelesi" ni Mbunge, Kiongozi kila kitu anachofanya ni kwa Kodi yetu hata hii posti aliyotuma ametumia Kodi zetu, narudia Zitto ni Kiongozi Kama walivyo hao anaowataka wajiuzuru, ni ujinga kutuaminisha eti they are not part of this simply because they are from opposition, ukweli unabaki wote ni viongozi, Kama ni serikali imekwama yeye hawezi kujiondoa, unless otherwise aje hapa atueleze kwanini analipwa mshahara na Serikali!
 
Ajali ya Mv Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe Bado mawaziri?

Ni masikitiko makubwa kwamba, Serikali ya wanyonge imeokoa mtu mmoja, wakati wananchi wenyewe wameweza kuokoa watu 40..... hii ni aibu kubwa sana. Watu 225 wamepoteza maisha sababu ya uzembe. Tuache kujidanganya na mapenzi ya Mungu. Mungu katupa akili, namna ya kuzitumia ni sisi wenyewe. Huwezi kupata Habari ya ajali saa nane mchana halafu ukaitisha Kamati ya Usalama mkoa saa 11 jioni ( yaani mwendo wa Dreamliner Dar-Mwanza mara 4 ). Rais naye hakuitisha Cabinet ya dharura wala Baraza la Ulinzi na Usalama Taifa kuratibu uokoaji. Uokoaji unasitishwa sababu ya GIZA? Tukihoji mnasema tunaleta Siasa? Nonsense!

Kwa nchi zilizoendelea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu walitakiwa wawe wamekwishafutwa kazi au wamejiuzulu wenyewe.....Miaka 57 baada ya uhuru...Jeshi la uokozi linapoishia kuwa jeshi la UOPOZI, ni wakati wa rafiki nyangu Kangi Lugola kupumzika. Waziri Kamwelwe, Jenista na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja. Bahati mbaya sana Rais amechoka na hivyo hajali tena. Wazembe Ndio wameongoza mazishi ya ndugu zetu leo.
 
Hakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!
Sijui kwa nini mkuu wa nchi ameamua kutoa political stunts?

Kama angepeleka vifaa vya uokozi mapema kusingekuwa na 'KIKI ZA KISIASA'

Kama angetoa amri kwa waliosema wanasitisha tukio la uokoaji kutokana na GIZA kusingekuwa na 'KIKI ZA KISIASA'
 
1, Na swali ile ajari ya Moto iliyotokea kwenye ile nnchi ya ulaya mawazili walijiuzuru? Au mamlaka husika inayosimamia?
2, Jitaidi utumie ujana wako kama kweli unawapenda Watanzania vijana waweze kupata fursa za ajira au buni kitu cha msingi umekaa attention mda wote kukosoa ni sawa na unajikita kutafuta mabaya ya mwenzio kwa staili hii tutafika? Ndo maana wabongo wamtoendelea
3, waliosababisha ajali ni Mawazili? au mamlaka husika ndo washughulikiwe?Aseee kuwa Makini
Hizo ni siasa tu,hamna kitu
 
Masaa 24 ya kuomba radhi. Hakuomba. Mengine msubiri uwezo wake mola
Shida ya sisi waafrika ni uzuzu, kila kitu kutaka kusimamiwa, hilo suala la kivuko wala huhitaji uwajibikani sijui wa waziri sijui nani! Watendaji wa hicho kivuko tu ilitakiwa kujua kwamba kivuko kimejaza nje ya uwezo wake na wala haikutakiwa uwepo wa wazir wala nini.
 
"taratibu zitto, si vizuri kuikosoa serikali yangu. unajua mm ni kama baba yako wa kukuzaa"
 
Maneno ya Zito ni mazito na yanayofikirisha kwa wenye akili. Kama Taifa ni lazima tukubali upungufu mkubwa juu ya utayari na uwezo wetu katika kushughulikia majanga.

Kwa vyovyote, matendo yetu yameongeza idadi ya vifo badala ya kupunguza.

Tunaweza kupuuza maneno ya Zito kwa ubishi tu lakini kuna hoja ya msingi.
 
Rais naye hakuitisha Cabinet ya dharura wala Baraza la Ulinzi na Usalama Taifa kuratibu uokoaji. Uokoaji unasitishwa sababu ya GIZA? Tukihoji mnasema tunaleta Siasa? Nonsense!.
Hili linaleta ukakasi sana. Pombe atakuwa anajua kabisa kuna uzembe na ujinga mkubwa sana ulifanyika hapa. Kuna siku atakuja kutoka hadharani na kulisema hili, ikiwapo kutumbua baadhi ya watu. Hivi hawa walishindwa hata kwenda kuwaomba ACACIA zile taa zao zenye mwanga wa kutosha? Hivi jeshi la majini linalojifanya kufanya patrol ziwani kumbe nalo halina taa? Hatari kubwa
 
Hakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!
Kuna jambo la msingi zaidi ya usalama wa Watanzania!?
Kuonyesha wapi na kipi kimekosewa ni kuprovoke!?
 
Naona zitto unataka wakulissu.
Maana mwenzako alikua na kiherehere Kama chako.
Ngoja tutazame mwisho wako utakuaje maana hutulii
We jua tu anakupigania wewe, watoto wako na wajukuu zako.Hao unaowatetea hawana habari nawe zaidi ya kukutumia tu kama ile tissue ya msalani.
 
Ndio maana wanataka kuzima huu mjadala wa kuihusisha serikali na uzembe wa ajali hii

Badala ya kujibu hoja kama hizi ili wananchi tuwaelewe wanataka kutumia udikteta kuzima uhuru wa wananchi kuhoji serikali yao

Hii kweli ni serikali ya Wanyonge maana Waziri Kigwangallah yeye alipopata ajali alipelekewa ndege ili kumuwahisha hospital, lakini wanyonge walishindwa hata kuokolewa sababu ya giza limeingia

Hadi 2020 hakuna wasiofikiwa na huu mnyororo wa dhuluma, Lissu aliwaambiwa Watanzania kuwa utawala huu wa ajabu sana
 
Na kachoka kweli kweli, nakumbuka aliwahi kusema ana stress.
 
Back
Top Bottom