Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Majuzi imetokea ajali ya kutisha ya basi la Mwendokasi liliyokuwa inatokea Kivukoni.
Miaka 3 iliyopita ilitokea ajali maeneo ya Utumishi jirani na kivukoni ambapo mtembea kwa miguu alikuwa anavuka kwenye zebra aligongwa na basi la mwendokasi na kufariki hapo hapo. Aliyefariki ni jirani yangu ameacha mjane na watoto.
Mwezi Desemba 2022 nilishuhudia ajali ya basi la Mwendokasi likimgonga mtembea kwa miguu mbele ya Mahakama ya Rufaa Kivukoni. Dereva akakimbia.
Ninaamini wengi wetu humu tumeshihudia ajali kadhaa za mabasi haya ya Mwendokasi ambapo madhara ya binadamu yamekuwa yakiripotiwa.
Katika kauli ya Kamanda wa Kanda Maalum Dar akielezea tukio la ajali ya juzi hapa. Alisema basi la Mwendokasi likiwa kwenye njia yake, gari binafsi ikaingilia na kusababisha ajali ile.
Tuangalie matokeo, yaani impact iliyotokana na ajali hii. Basi limeharibika sana na hata upande uliogongwa kumetokea uharibifu mkubwa. Kwa vyovyote vile basi lilikuwa katika speed kali.
Tujiulize hapa;
Mabasi ya Mwendokasi yanaruhusiwa kutembea mijini kwa speedlimit ya KPH ngapi? Pale Kisutu, dereva wa chombo anapita makutano ya Jamhuri na Morogoro kwa speed kubwa na akashindwa kufunga breki na kuparamia maduka.
Afande Muliro, anajihakikishiaje usahihi wa kasi ya basi kushindwa kushika breki hadi linaenda kuparamia watembea wa miguu.
Swali lingine ni hili, mgonjwa unknown, yaani asiyetambulika pale MOI wanatudanganya ili iweje?
Mkiangalia picha za basi baada ya ajali (nitaziweka baadaye) kuna virago vya kulalia vya ombaomba wasio na makazi. Hao nao taarifa zao zipoje? Kwa sababu ni mtu mmoja pekee aliyeonekana anakimbia. Naye alikuwa amekaa kwente kiti.
Tanzania ni yetu sote, tunahitaji kupata majibu ya mikakati ya kupunguza ajali za Mwendokasi.