Ajali ya mwendokasi tarehe 22/02/2023 tujiulize maswali haya...

Kuhusu uzembe dereva wa gari dogo ndio wa kulaumiwa
Mshana Jr kama umepita pale karibuni hupaswi kumlaumu Dereva wa gari Ndogo.

Pale Junction mwanzo badala ya Mataa kulikuwa na VIOO mfano wa Side Mirror za gari. Ndio tulikuwa tunatumia unapovuka. Kuona gari za mwendokasi kama zinakuja.

Ila karibuni vile vioo ni havipo tena, hivyo inakuwa ni ngumu kuona Gari ya Mwendokasi kama inakuja.

Kuvuka ile Junction ni kama tu KUBET. inahitaji Umakini wa hali ya Juu sana.
 
empty set kabisa, unapalilia tatizo kwa kuwatetea hao wapumbavu ?
mara ngapi hao jamaa wanagonga watu kwenye barabara za kushare kisa tu wanaendesha basi la Mwendokasi ?

huwezi kwepa tatizo kwa kulikimbia, hao jamaa wapunguze spidi pindi wawapo barabara za kushare
la sivyo kila ajali, na ujinga wenu mtazidi kutetea hao wajinga wenzenu kisa yeye ni Mwendokasi
 
mara ngapi hao jamaa wanagonga watu kwenye barabara za kushare kisa tu wanaendesha basi la Mwendokasi ?
Huyo kaletewa Leseni na Mjomba wake akiwa nyumbani halafu anajiona Dereva.

Hajui yale Makutano pale yanazibwa na Kituo cha Mwendokasi. Huwezi kuona gari inayokuja kwa sababu inakuwa imezibwa na Kituo cha Mwendokasi.

Mwendokasi pale wakipita Taratibu sehemu za Makutano, itapunguza sana Ajali.
 
Kumbuka kuna feeder road na main road bebi niambie gari dogo lilikuwa barabara gani? Na ninani kati ya magari yale mawili alipaswa kuchukua tahadhari anayekatiza barabara ama aliyeko barabara kuu?
Rejea pia ripoti rasmi ya polisi
 
Kuvuka ile Junction ni kama tu KUBET. inahitaji Umakini wa hali ya Juu sana[emoji818]
 
Kumbuka kuna feeder road na main road bebi niambie gari dogo lilikuwa barabara gani? Na ninani kati ya magari yale mawili alipaswa kuchukua tahadhari anayekatiza barabara ama aliyeko barabara kuu?
Rejea pia ripoti rasmi ya polisi
Mwendokasi alipaswa(anapaswa) kuchukua tahadhari kwa kupunguza spidi pindi awapo kwenye barabara za mitaani, punguzeni kutetea ujinga
 
Naunga mkono hoja
Pia kuhusu speedd limit ya magari yale ijulikane.

kwa sababu barabara yao ni uninterrupted wawekewe kasi ya kutembelea ili kumuwezesha dereva kukabili dharura za barabarani
Kuanzia junction ya DIT hadi Kivukoni speed limit iwepo
 
Pale nimejadili lile tukio specifically, and not about mwendokasi drivers! Na wala sijawatetea ila nime-react kwa ulichoandika! Wewe umesema huwezi kumlaumu yule dereva kwa sababu hakuna taa za kuongozea magari! Mimi nikakumbia kuwa asilimia kubwa ya makutano ya barabara yanategemea alama na siyo taa! Wapi nilipowatetea madereva wa mwendokasi? Unadhani mimi sijui walivyo wazembe na kujifanya wababe? Jifunze kusoma kwa ufahamu!
 
Mwendokasi alipaswa(anapaswa) kuchukua tahadhari kwa kupunguza spidi pindi awapo kwenye barabara za mitaani, punguzeni kutetea ujinga
Kwakuwa umeanza kuhemka siwezi kuendeleza mjadala nawe ila nakushauri ukasome tena sheria za barabarani. BTW kama sisi tunatetea ujinga vipi kuhusu ripoti ya polisi?
 
vilaza wanaoajiriwa wakiwa na FFFFFFFF au ?
Vipi kuhusu matumizi ya feeder road kati ya aliye main road? Na anayekatiza barabara? Umeona pale Mbezi njia ya kwenda Goba walichofanya? Hili ndio la kujadili
Kuna sheria za barabarani inabidi uzielewe
 
la kujadili ni hao wehu kupunguza spidi wakitoka kwenye njia zao, la mtaendelea kutwanga maji kwenye kinu
 
la kujadili ni hao wehu kupunguza spidi wakitoka kwenye njia zao, la mtaendelea kutwanga maji kwenye kinu
Ripoti ya polisi ina majibu yote
Ndio itatumika mahakamani na ndio itatumika bima na popote itakapohitajika kumbuka ripoti ya polisi huambatana mpaka na michoro
 
Ripoti ya polisi ina majibu yote
Ndio itatumika mahakamani na ndio itatumika bima na popote itakapohitajika kumbuka ripoti ya polisi huambatana mpaka na michoro
Hata maelezo ya polisi kwa watuhumiwa ndio huwa inatumika mahakamani, na kuna malalamiko mengi tu juu yanavyoratibiwa na kuchukuliwa.

Sheria zipo, sheria za barabarani zipo hilo kila mtu analifahamu, je katika mazingira yale ya mjini hayo mabasi yanapaswa kwenda katika speed kali ile kwa kuzingatia mazingira ya huko mjini na harakati za watumiaji wengine wa barabara? Hebu tulichanganue hili kwa mazingira haya.
 
Nakumbuka hii maana mimi nilipanda mwendokasi ya upande mwingine nilikuwa naelekea kariakoo, sasa nilipofika pale Magomeni ndio nikaona hiyo ajari na lile basi la mwendokasi halikusimama pale likaendelea na safari zake
 
Naam, nimewahi vipna vile vioo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…