Ajali ya ndege Bukoba ni matokeo ya uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.Tuwajibishane ili tusirudie makosa

Ajali ya ndege Bukoba ni matokeo ya uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.Tuwajibishane ili tusirudie makosa

Bora useme Serikali na Bunge lake kujiuzuru,badala ya kutafuta kujiuzuru kwa waziri mkuu!

Ilhali ukijua wazi kwamba Mtunga sera Ni serikali na mleta Bajeti ni wizara ya fedha na wapitisha bajeti ni Wabunge wa CCM!

Majaliwa Mungu aendelee kumjaalia!
Hii ishu si ya kumuwajibisha mtu mmoja hii ni ishu ya uzembe wa watu wengi sana.
Kumuwajibisha waziri mkuu peke yake hali ya kuwa watendaji husika waliozembea kwenye kazi yao kuendelea kuwepo kwenye kazi zao haitasaidia kitu bado wataendelea kufanya kazi kwa mazoea.
Ingekuwa tupo kwenye nchi iliyo serious ilitakiwa kuanzia Meneja wa uwanja wa ndege mpaka watendaji wote wanaohusika na mambo ya usalama pamoja na flight controllers wasimamishwe kazi ili wengine watakaobaki wawe makini na kazi yao.
Ila kwa vile nchi yetu haiko serious bado wanapiga blah blah na kuweka tume na vikao vya kutafuna posho.
 
Afadhali mleta uzi amekuja kiweredi!
Ila watanzania kuna mifumo yetu ya ufikiri haifanyi kazi vizuri. Tunahitaji overhaul!
HAIWEZEKANI KATIKA AJARI HII TUKAJIKITA KWA SUALA LA MAJALIWA NA MLANGO NA KUACHA MAMBO YA MSINGI ILI ISIJIRUDIE TENA! na KUWAJIBISHANA!

Maanake ni kwamba tumejiweka kundi la SIMPLE MINDS DISCUSS PEOPLE! Hapa kuna ISSUES!
Kwa aliyeko bukoba nyamkazi mwaloni kupata picha vizuri kabla, wakati na baada ya ajari haiitaji nguvu sana. Kuna eye witness muhim sana anaitwa Egid,(yuko kati ya waliopewa mil 10 kama kikundi) ndo alimwita hata huyo majaliwa wawahi na mtumbwi mana aliona kila kitu. Ndiye alimbeba maja alipopigwa na kamba akazimia ili apelekwe hosp.

Maja tukio kidogo liondoke nae pia, anastahili pongez pamoja na wenzie bila kujari utofauti wa stori.
Mpaka sasa tunalotaka kujua hatujapewa:

1. Eye witness anasema kulikuwepo mvua lakini visibility hadi musira ilikuwepo.
2. Ndege ilianguka tairi hazijatoka na ikiwa imezimwa kabsa.
3. Ndege ilizunguka mara kadhaa had misenyi kwa sabab ya tairi kugoma kutoka au hali ya hewa!
4. Mchango wa vitengo vyote vya uokozi.
5. Mchango wa wafanyakazi airport wakat ndege ikiangaika na kuzunguka zunguka.
6. Ndege ilianguka nje ya mwelekeo wa uwanja kama vile rubani ameshapanga ajari itokee majini.

Maisha hayana rehearsal, tupende reality.
DO NOT POLITISIZE YOUR LIFE,
LIVE RESPONSIBLY!
 
Mkuu barafu hongera kwa kurejea jamvini tena, imekuwa ni kipindi kirefu cha almost miaka 2 au zaidi tangu upumzike kuandika humu!

Nakubaliana na wewe pamoja na Wachangiaji wengine walioonesha kuwa athari za ajali ile imesababishwa kwa sehemu Kubwa na Uzembe.

Kuna mambo mawili nayaona, Moja ni ufinyu wa Bajeti wa hivyo vyombo vya Uokozi hivyo kukosa zana na vitendea kazi vya Uokozi. Kama Nchi, tumekuwa hatutoi vipaumbele kwenye jeshi la Zimamoto.

Kama mmekuwa wafatiliaji Wazuri, naombeni mpitie Bajeti hii tunayoitumia ya 2022/2023, mtakuja kuona Bajeti Kubwa imekwenda kwenye Mishahara, kununua Silaha, Uniform, Magari n.k

Sababu ya pili, ni Utaalamu. Wengi wa watumishi wa Jeshi la Uokozi wapo na Weledi kwenye upande wa Moto.

Wito kwa Mamlaka ni kufanya mageuzi Juu ya Jeshi hili, kama mmepita pita Wilayani huko, unakuta Kuna Askari Mmoja tu wa Jeshi la Uokozi na Zimamoto ambaye hana hata Fire Extinguisher kwenye Ofisi yake.

Kuna Wilaya sitaitaja Jina, kutokana na shughuli za kiuchumi ambazo ni Uchimbaji wa madini ambao unaendana na Vilipuzi hasa kwa Wachimbaji wadogo wa maeneo yale, nimeshuhudia zaidi ya Ajali 3 za Moto Ndani ya Mwaka Mmoja na hakuna hata hatua zinachukuliwa na Mamlaka walau kuwa na hata Gari la Zimamoto!
 
Tanzania Civil Aviation Authority(TCAA) ndio regulator wa ubora wa viwanja vya ndege Tanzania,wakati Tanzania Airports Authority(TAA) ndio operators wa Viwanja vya ndege Tanzania isipokuwa vya Zanzibar na KIA ambacho kipo mbioni kurudishwa TAA
So ni taasisi gani inayooperate kiwanja cha KIA na Zanzibar airport?
 
Jipigepige kifuani huku ukijisemesha Mimi ni mchawi kasoro vitendea kazi ndio sina.

Hapa JF ni barafu ndio amekuwa ngumu wa kuchambuwa industry ya Aviation unless kama ndio leo umeanza kuna Uzi wake.

Fistula inatibika wahi matibabu.
Wewe matakle kweli, kuchambua huko kunahusiana vipi na ujinga ulionao? Anawaongopea wajinga kama nyie toka lini mlango wa dharura wa precision ukawa na ngazi?
 
Ukishafunguwa mlango unafikaje nchi kavu?
Unajaribu kusogeza goli. Mtaalam alisema hauwezi kufungua mlango bila msaada wa mtu aliyekuwa nje. Ni dhahiri kuwa hakuwa sahihi na mlango unafunguliwa kutoka ndani tu. Taratibu zikifuatwa, abiria wanatakiwa kuvaa life vest kabla hawatoka nje.

Life vest hizo zinawawezesha kuelea mpaka hapo watakapo okolewa na kupelekwa nchi kavu. Ndege nyingi zinakuwa pia na life rafts ambazo zinaweza kutumiwa kuwahifadhi watu mpaka watakapookolewa kama ajali imetokea mbali na nchi kavu au kama nchi kavu kuko karibu kuwapeleka nchi kavu.

Amandla...
 
Afadhar mleta uzi amekuja kiweredi!
Ila watanzania kuna mifumo yetu ya ufikiri haifanyi kazi vizuri. Tunahitaji overhaul!
HAIWEZEKANI KATIKA AJARI HII TUKAJIKITA KWA SUALA LA MAJALIWA NA MLANGO NA KUACHA MAMBO YA MSINGI ILI ISIJIRUDIE TENA! na KUWAJIBISHANA...
Mkuu hata bila code ..shikamoo
 
Heshima kwako kaka, nilikusubiri sana ili nikusome na kujifunza, hivyo nashukuru sana.

Umeshusha Madini mengi sana ila kwa makusudi umeamua kumfagilia na kumpamba huyo dogo Majaliwa kwa sababu unazozijua mwenyewe.

Dogo Majaliwa alieleza kuwa akitumia kasia lake na kuugonga mlango wa ndege mpaka kuuvunja japo wewe umetueleza njia tofauti ya matumizi ya kasia katika mlango wa ndege ili kutimiza agenda yako.

Hakuna asiyekubali msaada mkubwa uliofanywa na wavuvi (Majaliwa akiwa mmoja wao), kinachopingwa ni kutangaza Majaliwa ndiye shujaa na ukichukuza kuna wavuvi wengi waliofanya kazi ya uokoaji mpaka kumuokoa Majaliwa mwenyewe.

Ila nikushukuru kwa kuja humu Jf sababu wengine walishasema #Barafu ni miongoni mwa Marubani waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Nikutakie maisha marefu
 
Heshima kwako kaka, nilikusubiri sana ili nikusome na kujifunza, hivyo nashukuru sana.

Umeshusha Madini mengi sana ila kwa makusudi umeamua kumfagilia na kumpamba huyo dogo Majaliwa kwa sababu unazozijua mwenyewe.

Dogo Majaliwa alieleza kuwa akitumia kasia lake na kuugonga mlango wa ndege mpaka kuuvunja japo wewe umetueleza njia tofauti ya matumizi ya kasia katika mlango wa ndege ili kutimiza agenda yako.

Hakuna asiyekubali msaada mkubwa uliofanywa na wavuvi (Majaliwa akiwa mmoja wao), kinachopingwa ni kutangaza Majaliwa ndiye shujaa na ukichukuza kuna wavuvi wengi waliofanya kazi ya uokoaji mpaka kumuokoa Majaliwa mwenyewe.

Ila nikushukuru kwa kuja humu Jf sababu wengine walishasema #Barafu ni miongoni mwa Marubani waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Nikutakie maisha marefu
Kuuvunja mlango?!

Acha urongo wewe
 
Back
Top Bottom