Ajali ya Precision Air: Ripoti yabaini hakuna Control Tower, Boti za Uokozi zilichelewa, Mhudumu na Abiria ndio waliofungua mlango

Kwa hiyo pilot alipigwa maluweluwe, badala ya kuona maji akaona nchi kavu........abiria wenyewe wanaweza kuona nje, itakuwa rubani bhana ashindwe kujua hapa anatua majini au nchi kavu......
 
Ina maana Rubani hakuwatangazia abiria kuwa emergency landing ili wavae vesti zao.

Inanamaa alishusha landing gear na akatua kwenye shalow waters kitu kilichomsababishia drag na Ndege kuchotwa na kupoteza muelekeo iwapo asingeshusha landing gear Ndege ingeslide hadi Nchi kavu.
 
The END justifies the means.

Watakuja wengine kusema huyo kijana Jina lake halisi Si Majaliwa.

Majaliwa mvuvi ameshamnasua Majaliwa PM Kutoka HILA za kuzamishwa na wabunge wenzie Bungeni.

Akipanga Mungu, mwanadamu hawezi Pangua.

Ameeeeen.
 
Hivi black box kazi yake ni nini? Na hyo ripoti imengalia vitu gan mpak kuja na majibu ya hvyo , duniani kote ripoti za ajali ya ndege primary data ni black box , kwenye hii ya kwetu hata black box haitajwi
Hii ni report ya awali...ile ya black box itakuja baadae na chanzo halisi na mapendekezo...Ukiisoma hii ripoti imesema uchunguzi wa chanzo is ongoing.
 
Mi nahisi hiyo ndege ilikutwa na kitu kinaitwa aerodynamic stall dakika chache kabla ya kutua kutokana na kupungua kwa airspeed kutokana na kuzunguka mara mbili kabla hali ya hewa haijaimarika maana ni rahisi rubani kupunguza umakini wa kubalance airspeed hivyo wings kuacha ku generate lift na hivyo ndege kuanguka (nosedive).

Kama nitakuja kubahatika kuiona ripoti kamili ya uchunguzi nitalinganisha na mtazamo huu.
 
Ndugu nani kakudanganya wahudumu walikufa?wahudumu wote wawili walipona.Tusiokoteze habari vijiweni
 
Hii ni report ya awali...ile ya black box itakuja baadae na chanzo halisi na mapendekezo...Ukiisoma hii ripoti imesema uchunguzi wa chanzo is ongoing.
Ngoja tusubiri hiyo ya black box mkuu
 
Majaliwa bado atakua Shujaa maana ndiyo Mtu wa kwanza kuiona hiyo ajali na kuwataarifu Wavuvi wenzie na kuwai kukimbilia kwenye ajali na kutoa msaada kwa wakati!!
Hivi ndege ilivyokuwa kubwa tutegemee kuwa wasingeiona?

Serikali na wananchi walikosea kupaisha mtu kabla hawajatoa ripoti.
Ona sasa wameumbuka

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Bongo kila mtu ni mjuaji. Ripoti imetoka bado haiaminiki.

In my view, hata kama unaona mabaya always ila ripoti imekuwa fair. Serikali na vyombo vyake wameambiwa udhaifu wao

Na uchunguzi wa chanzo cha ajali bado unaendelea, tupewe nini tena?
 
Hivi ndege ilivyokuwa kubwa tutegemee kuwa wasingeiona?

Serikali na wananchi walikosea kupaisha mtu kabla hawajatoa ripoti.
Ona sasa wameumbuka

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Namshangaa mdau hapo juu, kwa ukubwa wa ndege bado unamuhitaji majaliwa akuoneshe ndege iliyodondoka tena ikiwa bado inaelea?
 
Kwahiyo mnataka kutuambia Majaliwa hakusaidIa ama? Mwacheni nae alicheza pat yake huyo muhudumu yuko wapi?
 
Binafsi nimesoma maswala ya aviation ndege huwez kufungua mlango ukiwa nje.

Afu pia kasia ambalo ni jiti haliwezi kuvunja mlango wa ndege ukafunguka swali ni je kama majaliwa alifungua mlango wa ndege je huyo muhudumu ameiongopea bodi ya uchunguzi kwamba yey ndo alie fungua mlango na kuuzuia usijifunge mpka abilia washuke?

Jaribuni kutunga uongo unao fanana na ukweli
 
Soma ripoti Acha tantalila.
 
Kwa skendo kama hii, ya kizembe na kuwadanganya wananchi kwa kuweka shujaa wa "mchongo", ingekuwa ni nchi za wenzetu Ulaya, kuanzia Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa, Spika wa Bunge na viongozi wengine wengi wangelazimika kujiuzulu nafasi zao.

Lakini kwakuwa tupo Bongo sishangai kuona wakiendelea na kazi zao bila hata mshipa wa aibu.

Swali la kujiuliza, walitudanganya sisi Wananchi kwa manufaa ya nani????
 
kwa hio kitalaam Majaliwa tunamwitaje ?

tatizo Tanzania siasa mpaka kwenye maisha ya watu
 
Aircraft investigation acha ianze kufanya kazi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…