Ajenda za CHADEMA zilizojadiliwa Ikulu

Ajenda za CHADEMA zilizojadiliwa Ikulu

Chadema bure kabisa

Mnataka Rais aingilie Mahakama kuwakandamiza Covid 19?
Unajua lilivyokuwa presented kwenye huo mkutano? Kwanini ung'ake kwa hasira kwa jambo ambalo hukusikiliza mwanzo mwisho?

Bwashe mbona unajifanya unajuasheria sana? Au wewe ni kati ya wale waliopata ""A ya constitutional law""? Na wanaandika mambo ya kisheria pale tu wanapolenga CDM? Hovyo kabisa
 
CHADEMA wanapambana na watu wasiowajua kwenye anguko lao kukosa wabunge waliochaguliwa na wananchi bungeni na ni anguko kubwa sana kisiasa na kikubwa ni kukosa ushawishi wa kisiasa kwa wananchi ambao ndio wapiga kura wao sasa wao badala ya kuja kwa wananchi na kujenga imani nao kwa siku za mbeleni wao wamekomaa na serkali hayo maridhiano wanayotaka na wengine wanavyojua ni tofauti wenzao wanawaza kuleta maelewano mazuri kwenye siasa wao wanawaza kupewa nafasi za kiuongozi na kupewa hela kama fidia hiyo haipo,mpaka sasa mi sioni sababu kwanini nimchague kiongozi kutoka CHADEMA sioni sababu hivyo tusishangae 2025 hali ikawa tete na kuna dalili waliokuwa wabunge wa CHADEMA wasiingie tena bungeni kwa nafasi ya ubunge na tukawasahau kabisa na pia hicho chama kunakoelekea kitakuwa kama TLP au NCCR ambavyo mvuto wake kwa wananchi ni wakawaida kiasi kufikia kuwa na mbunge mmoja tu au asiwepo kabisa.
 
Kwenye suala la akina Halima, mnamuomba Rais avunje Sheria aingilie muhimili wa mahakama? Sasa zamu yenu kuomba maelekezo kutoka juu kwenye maamuzi ya mahakama zetu?
Katiba imevunjwa hata kabla ya suala lenyewe kupelekwa mahakamani!
 
Hakuna kuingilia mahakama, ila haki itendeke mahakamani. Samia asiweke mkono wake pale wa kuleta delaying tactics, only that!
Kama kweli mnaheshimu mamlaka ya mahakama na mnaataka Jambo hili limalizikie huko, kulikua na sababu gani ya kuliweka kuwa sehemu ya agenda za kikao chenu na Mh Rais?
 
Mbona hukusema aliposema wenzie Mbowe walishafungwa wakati kesi ikiwa mahakama
Chadema Kama chama kinachotetea haki, hakipaswi kuwa sehemu ya vyama vinavyoamini katika nguvu ya Maelekezo kutoka juu Kama msingi mkuu wa kupata haki.
 
Maazimio yako wapi?

Yaani mwisho wa kikao wakatoka na kitu gani cha kufanyia kazi kwa pamoja?

Au ndiyo yaleyale ya "Rais amesikia na atayafanyia kazi yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho..?"

Kama ni hivi, basi hivi vinavyoendelea huko haviwezi kuitwa vikao vya majadiliano na maridhiano..!

Majadiliano & maridhiano maana yake, kila mtu anaweka mezani makwazo (grievances) zake, yanajadiliwa kwa pamoja, mnakubaliana tuache lipi na tuende mbele na lipi kwa pamoja..

Na mwisho kila upande unaondoka na kuanza kutekeleza makubaliano...

Je, hiki ndicho kinacho/kitakachofanyika kupitia vikao vyao hivi?

Hicho kikao Lissu alihitajika sana
 
Hicho kikao Lissu alihitajika sana
Ni kweli..

Lakini tukumbuke issue ya usalama wake bado haijawa resolved na Rais alishashindwa kutoa kauli yoyote sawasawa na alivyoombwa na victim..

Hopefully, issue yake ni moja ya components za mjadala huo. Tunaamini sooner or later, issue yake itakuwa resolved..
 
1. Upatikanaji wa katiba mpya.
2. Tume huru ya uchaguzi,
3. Zuio la mikutano ya hadhara.
4. Makovu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
5. Suala la wabunge 19 wa viti maalum.
6. Suala la ruzuku,
7. Usawa wa vyama vya siasa,
8. Watu waliochukuliwa hatua za kisheria kwa sababu za kisiasa.
9. Wakimbizi wa kisiasa waliokimbilia nje ya nchi.

Lengo kubwa la majadiliano hayo ni kuimarisha demokrasia na hali ya kisiasa nchini.

CHADEMA kiliwakilishwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohammed, John Mnyika (Katibu Mkuu), na Katibu Mkuu wa BAWACHA, Catherine Ruge.

Ujumbe wa CCM ulimjumuisha Mwenyekiti wa CCM, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka.
Hoja nzito sn
 
Hivi swala la wabunge 19 linawaumiza Nini wao? Kama wako Bungeni na kazi yao ya kuwafuta uanachama wamesha wafuta basi swala la kwao limeisha, juhudi za hawa 19 kuendelea na kazi ili wapate mishahara walee familia zao linawahusu nini?
 
1. Upatikanaji wa katiba mpya.
2. Tume huru ya uchaguzi,
3. Zuio la mikutano ya hadhara.
4. Makovu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
5. Suala la wabunge 19 wa viti maalum.
6. Suala la ruzuku,
7. Usawa wa vyama vya siasa,
8. Watu waliochukuliwa hatua za kisheria kwa sababu za kisiasa.
9. Wakimbizi wa kisiasa waliokimbilia nje ya nchi.

Lengo kubwa la majadiliano hayo ni kuimarisha demokrasia na hali ya kisiasa nchini.

CHADEMA kiliwakilishwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohammed, John Mnyika (Katibu Mkuu), na Katibu Mkuu wa BAWACHA, Catherine Ruge.

Ujumbe wa CCM ulimjumuisha Mwenyekiti wa CCM, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka.
Hoja za msingi zote,tunasubiri kwa hamu matokeo ya mjadala.
Heko CDM,CCM,Watanzania kwa kukubaliana kutokubaliana.Tunajenga nyumba moja,ya nini kugombnia fito?
Matatizo yote yanayotupata ni laana tunayopokea kwa kupuuza hoja ya Katiba tangia 1991/92.
Tanzania iliyokuwa kinara wa demokrasia Afrika na duniani inakuwa ya mwisho kwenye jambo la Katiba bora?Hii aibu ni kwa ajili ya CCM kuhofia kuondolewa madarakani?
CCM ni Bora kuliko Tanzania?
 
Kwenye suala la akina Halima, mnamuomba Rais avunje Sheria aingilie muhimili wa mahakama? Sasa zamu yenu kuomba maelekezo kutoka juu kwenye maamuzi ya mahakama zetu?
Mahakama na utii wa sheria ni vitu viwili tofauti.Mdee na wenzake siyo wanachama wa CDM,kisheria siyo wabunge mpaka mahakama itakapowarudishia uanachama wao.
 
Chadema bure kabisa

Mnataka Rais aingilie Mahakama kuwakandamiza Covid 19?
Rais ndio mkuu wa mihimili yote wacha ushamba kwani mbowe katolewa na nani c huyo huyo rais samia na hao wote waliowekwa ndani na kesi zao zikawa hazimaliziki wakati wa magufuli na mahakama zilikuwepo lakini zilikuwa hazifanyi kazi kutokana na amri kutoka kwa magufuli.
 
1. Upatikanaji wa katiba mpya.
2. Tume huru ya uchaguzi,
3. Zuio la mikutano ya hadhara.
4. Makovu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
5. Suala la wabunge 19 wa viti maalum.
6. Suala la ruzuku,
7. Usawa wa vyama vya siasa,
8. Watu waliochukuliwa hatua za kisheria kwa sababu za kisiasa.
9. Wakimbizi wa kisiasa waliokimbilia nje ya nchi.

Lengo kubwa la majadiliano hayo ni kuimarisha demokrasia na hali ya kisiasa nchini.

CHADEMA kiliwakilishwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohammed, John Mnyika (Katibu Mkuu), na Katibu Mkuu wa BAWACHA, Catherine Ruge.

Ujumbe wa CCM ulimjumuisha Mwenyekiti wa CCM, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka.

Conclusion:
Agenda zote ni blah blaha
 
CHADEMA kinasema kimewaweka kiporo Madiwani 85 pamoja na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenan kwa kosa la kutokukubaliana na msimamo wa chama hicho, uliolaani na kujiondoa kwenye matokeo yote ya Uchaguzi Uliopita.

lakini wanamtambua Rais Samia. 😁
 
Back
Top Bottom