Ajifungua Akiwa Safarini Kwenye Basi Kampuni ya Katarama

Ajifungua Akiwa Safarini Kwenye Basi Kampuni ya Katarama

Ngoja waanze kumzungusha kwenye media wamhoji mara paap...mgeni rasmi bungeni
Nawaona UWT nao wakinamama
Watamvizia ...kik kik tu

Ova
 
Inaweza kuwa safari yenye huzuni na kukushtua endapo kunatokea taarifa za kuogofya za ajali hama hama tukio lenye kuhuzunisha.

Hapo hapo safari inaweza kuwa na furaha endapo safarini kuna vicheko kwa wasafiri.

Tukio lililotokea majira ya saa 19:34 maeneo ya dumila karibu na mzani ni mshangao.

View attachment 3132869
Censored image ☝🏾

Ni abiria aliyekuwa anatokea Dar Es Salaam aliyefahamika kwa jina moja la Aneth kuelekea Bukoba amejifungua mtoto wa kike akiwa safarini.

Hatimaye Mama na mtoto wamebaki kituo cha Afya hapo Dumila kwa uangalizi wa wataalam wa Afya.

Hongera kwa wamama wote waliotoa msaada na hatimaye mzazi kujifungua salama, asante kwa kampuni ya Katarama kwa ushirikiano mliotoa.

USHAURI; Wenye makampuni ya mabasi naona haja ya kuwapa elimu zaidi wafanyakazi wenu hata hii ya ukunga, maana si mara ya kwanza kwa tukio kama hili.
Hapo sasa kwa sifa za wahaya mtoto ataitwa "transport rutaswema" ao ontheway rweyemamu, utasikia we "njiani"rwegoshora
 
Hongera mzazi, wafanyakazi wa basi na abilia kwa msaada wenu kuokoa maisha ya mama na mtoto. Ni vizuri ila na sisi tuepushe mama mwenye ujauzito wa miezi tisa kusafiri safiri.
 
Kimsingi mama mjamzito anatakiwa asafiri kwa ushauri wa daktari especially Kwa safari ndefu ila huwa inachukuliwa poa especially kwa usafiri ardhini kwa lolote likitokea kuna abiria lakini kuna vituo vya afya huko njiani.

Kwenye ndege safari za ndani 36 weeks (kwa Tz yetu 32 weeks) unatakiwa usafiri kwa ushauri wa daktari.

Nadhani LATRA kuna haja ya kuweka kipengele kwa abiria wenye mahitaji maalumu kutoa taarifa kwa wasafirishaji ili wasafirishaji wawe karibu na abiria husika especially wanapopita kipande ambacho kirefu hakuna huduma za kijamii

All in all, wamama wenye uwezo wa kuzalisha siku hizi tangu wakunga wa jadi walivyopigwa stop ni wachache sana hivyo wamama wajawazito na sie wababa tujitahidi kuwashauri wajawazito kama hakuna umuhimu sana wasifanye safari ya mbali hasa mimba ikianza kusoma 33 weeks, unaweza ukasafiri na bus ukakuta wamama wote hakuna mwenye ujasiri au ame experience namna ya mtu kujifungua alafu goma lipo katikati ya msitu wa Sao Hill au Shelui - Igunga Kijiji cha karibu kipo mbali kidogo na mtu anatakiwa ahudumiwe within 10 minutes
 
Dere anamwaga sana moto anafkia mashimo had ame induce labor
hongera yetu watanzania tumepata Spika
 
Waafrika tulivyo mazombie ata mpa mtoto jita la KATARAMA ,KATWAKSI .KABUS , KADUMILA ,SIAMINI ,BAHATI ,
 
Huyo msafiri hakujua siku zake au amejifungua njiti

Nadharia na uhalisia ni vitu viwili tofauti ndugu yangu, japo vinahusiana.

Maisha Yana mambo mengi sana, inaweza kuwa siku zilikua haijafika, lakini migogoro na mikwaruzano inapelekea maamuzi kama haya ya mtu kusafiri katika hiyo hali.

Enzi za Scandinavia Express likielekea Dodoma, Kuna mtu namfahamu alijifungulia Morogoro. Bus lilimpeleka Kituo Cha afya wakaendelea na safari ya Dodoma. Walivurugana na Mme wake akaina atajifungua Kwa mateso bila mtu wa kumhudumia, nyumba ilishakua ukanda wa Gaza, akaona mambo yasiwe mengi.

Tushukuru kwamba amejifungua salama na wanaendelea vizuri.
 
Back
Top Bottom