Ajifungua Akiwa Safarini Kwenye Basi Kampuni ya Katarama

Una mimba ya karibia kujifungua unaanza safari ya basi dar bukoba😬😬😬😬😬😬😬. Tuna vichaa wengi sana mtaani.
 
Huwa sielewi kwann mtu anasafiri akiwa na mimba ya miezi tisa, mwaka 2015 dada yangu alisafiri na ndege toka mkoani akiwa na mimba ya miezi tisa alivyoulizwa airport akasema Ina miezi sita Sasa na mwili wake unajua ni kweli, basi Ile anatua tu pale airport uchungu balaa, akakimbizwa haraka hospitali Ile kufika hata daktari hajamuona akajifungua, alijifungulia pale rugambwa hospital Iko sijui ukonga pale, mjini asingeweza kufika..!
 
Hakutakiwa kusafiri huyo asirudie tena kusafiri iwe kwa ndege au gari kama anakaribia kujifungua
 
Na kwa nini asafiri huku siku za kujifungua zikiwa zimefika? Inabidi achapwe viboko.
 
Watu Bado wanaishi kizamani kwa kujisemea "mimba yangu ya kwanza ilikuwa hivi" au "mama alikuwa hivi" hivyo nikiondoka naweza kufika. Alafu hofu tu zilizopitwa na wakati mtu anaenda kujifungulia nyumbani maana unakuta na mwanaume wake ameunga mkono hoja ya mkewe kwenda home. Wakati siku hizi mtu akionyesha dalili tu unakimbiza hospital unasikilizia tu atajifungua lini.

Walihisi wataokoa gharama ndo wameingia gharama sasa maana nauli imekwenda na wanapata gharama za kumsikilizia mzazi kwa siku moja ama mbili aweze kutoka, na tushukuru tu huduma ya kujifungua ni bure
 
Una mimba ya karibia kujifungua unaanza safari ya basi dar bukoba😬😬😬😬😬😬😬. Tuna vichaa wengi sana mtaani.
Shotocan
Kila jambo lina sababu yake, wkt umemuita huyo mzazi kichaa, nilitamani ungepata nafasi kuonana naye na kumuuliza kisa na mkasa kilicho mpelekea Kusafiri ktk hali ile!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…