King klax
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 4,307
- 2,754
Wana Askofu na MchungajiHivi Moravian nao Wana Mapadri??.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wana Askofu na MchungajiHivi Moravian nao Wana Mapadri??.
Na mimi najua hivyo.Sasa mtoa Post ametoa wapi Padri wa Wamoraviani?.Wana Askofu na Mchungaji
Roho ya mkwawa..Mwanaume mmoja kutoka wilayani Ludewa amekatisha uhai wake kwa kujinyonga sababu ikiwa ni kutotajwa na padri katika misa ya Shukrani.
Bwana huyo na mke wake walikuwa wakitoa Shukrani katika Kanisa la Moravian kwa mtoto wao kupona lakini kwa sababu zisizofahamika Padri aliyeongoza misa hio alimtaja mama wa mtoto pekee na kumuacha yeye baba bila kutajwa hali iliyoleta sintofahamu.
............................
Habari Kamili;
MKAZI wa mtaa wa Kanisani B uliopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe anaefahamika kwa jina la Raban Razalo (48) amefariki kwa kujinyonga na waya kwa madai ya kutoridhishwa na kitendo cha Padri wa kanisa la Moravian kushindwa kumtaja jina wakati wa misa ya sadaka ya shukrani iliyofanywa na mkewe baada ya mtoto wao wa miaka 10 kupona majeraha ya kuvunjika mguu.
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issa amesema taarifa zilizobainiwa na jeshi hilo ni kwamba mtoto wa familia hiyo mwenye umri wa miaka 10 alivunjika mguu na kupelekea familia kuzunguka katika hospitali tofauti kupata matibu na kisha kupona jambo ambalo limemsukuma mama kwenda kanisani kutoa sadaka ya shukrani ambayo imekuwa chanzo cha kuondoa maisha ya baba wa familia.
“Walivyoenda kutoa sadaka ya shukrani,Padri wa kanisa hilo amemtaja mama wa mtoto peke yake, baba imemletea sintofahamu na matokeo yake baba ameamua kujinyonga kwa kutumia waya wa TTCL.
Kamanda Issa ametoa wito kwa viongozi wa dini kuangalia umuhimu wa familia kwa kuwa inaundwa na baba na mama.
“Viongoizi wa dini angalieni umuhimu wa familia,familia ni baba na mama,ukimtaja mmoja matokeo yake ndipo unapopata sintofahamu na maamuzi yasiyo kuwa na tija”amesema kamanda Issa.
Aidha ametoa rai kwa wanafamilia kutochukua maamuzi kwa jambo ambalo wamekwazika huku akisikitika kwa familia hiyo kumuuguza mtoto mpaka kupona na baadaye mzazi anafariki.
Chanzo: RFA
Mungu anakuona🤣Kila siku tunasema TTCL hawafai mnabisha ona sasa waya wa TTCL umeshaondoa mtu huko ludewa
Hio taarifa imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe,na yeye ndio kasema padri,kwahio aulizwe KamandaRFA mmepotosha,. Moravian hawana padri alafu kuhusu kujinyonga Kwa Huyo jamaa (Kwa asilimia kubwa alikuwa anaandamwa na pepo la kifo.apumzike Kwa amani
Sent using Jamii Forums mobile app
Padri ni neno la kilatini leny maana ya mchungaji kwa kiswahili.Hivi Moravian nao Wana Mapadri??.
HahahahaKila siku tunasema TTCL hawafai mnabisha ona sasa waya wa TTCL umeshaondoa mtu huko ludewa
Usirudie kuapa ndugu.Msala kwa TTCL.
Ila kmmkk me kujinyonga sio leo au kesho.
Maisha magumu ila aisee kiporo cha wali ma maharage kitamu.
Maajabu ya dunia mkuuHivi Moravian nao Wana Mapadri??.