Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Unaangalia mambo kwa mafungu.., jiulize kwanini tunasomesha watu kama Taifa ? Ili tuje tuwape pesa baadae au ili wakidhi haja fulani ? Kwahio tunasomesha waalimu madaktari n.k. au watendaji ili tu wapate pesa na sio kwamba kuna need fulani inayotakiwa ?Kwani huyo expert akifa dunia au nchi itasimama?
Pili unadhani kwanini umri wa pensheni, dunia nzima unaongezwa ?, Ni kwamba nguvu kazi inayochangia ni ndogo kuliko watu wanaopokea; Kwahio naweza kusema badala ya kuhangahika na kugawana kidogo kilichopo watu wenye busara wanawaza ni jinsi gani wanaweza kuongeza kilichopo...
Kwahio wanasayansi wakifa tulishangilia ? Ni kwamba watendaji wala usiwaone kama mzigo bali watu muhimu wa kutenda kitu husika kwahio kama mwalimu yupo na ana knowledge cha muhimu ni kuona ni jinsi gani mnatumia ujuzi wake kuhamishia wengine na sio jinsi gani utakatiza ujuzi wake..., In short perception yako ni myopic... Ni sawa sawa unasema sababu maji kwenye ndoo ni mazito, utoboe matundu ili yavuje na kukupunguzia ule uzito (badala ya kuangalia ni jinsi gani unaweza kusaidiana na wengine kubeba kwa pamoja).....Watu wanajipa umuhimu mno kwenye maisha... Walikuwepo mascientist mwenye akili na sasa hawapo na dunia inaendelea tu. Ajira ziwe za mikataba tu vijana nao wapate ajira.
In short cha maana ni kuangalia ni vipi tunaweza kuongeza ujira kwa watu ukizingatia hata huko Serikalini ni watu wachache sana wanakuwa absorbed..., Kwahio kuondoa tatizo ni kuhakikisha kila mwenye nguvu zake anapata ujira; Kama alivyosea Nyerere kwenye Mkutano wa TANU....
- CHAMA CHETU KINASEMA - mtu mwenye Afya ambaye tumeshindwa kumpa njia halali ya kujipatia riziki yake. Nawaomba ardhi - hakuna ardhi; hamnipi ardhi, Mnasema "Ardhi hakuna". Naomba kazi ya kibarua basi, Nipeni basi ya kibarua, "Hamnipi kazi ya kibarua. Mimi niko tayari kabisa kufanya kazi au ya kulima au ya kibarua chochote nipeni. Hamnipi Chama Chetu kinasema MTANILISHA.