Ajira Serikalini iwe miaka 10 tu, baada ya hapo watu wastaafishwe

Ajira Serikalini iwe miaka 10 tu, baada ya hapo watu wastaafishwe

sasa ndugu nikuulize,

Deni la bodi ya mikopo atalipa nani kama nikiajiriwa kwa miaka 10 tu?

Kwa kweli ukipewa kitengo cha kutunga sera za uchumi na Siasa utatenguliwa mapema sana
Ameshindwa kulifafanua vyema tu, ishu ni watu waajiriwe muda mfupi kama huleti matokeo huna ubunifu ndani ya miaka mitano unatupwa. Ukiwa mzuri unaongezwa mitano mingine ila maslahi yawe mazuri tu.
 
Hii kauli sitoiacha nitaplead sana tu na nitazisema waajiriwa wapewe mda specific wa kufanya kazi tupishane, we unataka kuhold possession kwa zaidi ya miaka 30+ kwani hiyo office ulijengewa wewe na familia yako?

If ni kwaajili ya public lets public be benefited kwa wote.

Kama ni uzoefu na utaalam ndy mana kuna interviews na selection ya wafanyakazi.

Kila mwenye criteria zinazohitajika kupata kazi apewe kazi kulingana na utaalam wake, tupishaneni kwenye hizo offices wote ni watanzania asee 🇹🇿
Hauoni hadi Baadhi ya Viongozi wa Kiimani nao wanang'ang'ania nafasi? Swala la msingi kutokana na kuongezeka kwa wimbi kubwa la uhaba wa ajira. Kutengenezwe mazingira wezeshi na rafiki kwa watu kujiajiri na kufurahia kujiajiri. Nina uhakika kukifanyika hivyo kutatokea mapinduzi ya watu kuacha kukimbilia ajira na kujiajiri.
 
Mtaongea yote mtajitetea ila inapaswa muachie vijana nao wapate ajira wazazi wanasubiri na wao waone matunda ya uzao wao nyie mnabana tu mnashikilia wenyewe tu, mnapeana viti wenyewe tu mnakuwa na mambo ya hierarchical systems kwenye public offices.

It’s your era to end up all of these oppressive deeds.

Wacha vijana tutafute njia bana.
Usitafute kichaka kisichokuwepo boss halafu acha ubinafsi, kufikiria ajira kwa upande wa kuitafuna nchi tu. Hapo ukipata hiyo nafasi kwa miaka 10 unadhani kuna la maana utafanya zaidi ya kuitafuna chap chap ili upishe mwingine naye atafune? pia si kila anayepinga hii hoja yupo serikalini au ni mwajiriwa.
 
Huyu jamaa akipata ajira haya mawazo atayafuta 😀😀
Anaweza asiyafute ila akaitumia miaka 10 kutafuna haswa sababu akili yake haiwazi uwajibikaji, inaamini katika kula keki. Ingewaza uwajibikaji angekuja na hoja ya kuhakikisha watumishi wa uma wanawajibika ipasavyo. Na hili ndo tatizo letu, kila aliye nje anawaza aliye ndani anatakiwa kupiga hela na aliye ndani anataka kumeet expectation za jamii inayomzunguka, matokeo yake mtumishi anakuwa mwizi mwizi tu.
 
Nadhani Serikali ndipo inaelekea huko kupitia PEPMIS na PIPMIS, kama mfumo huu utaendelea kuboreshwa na kusimamiwa vizuri, kwa mbaali naona baadhi ya Taasisi kufutwa au kuunganishwa lakini pia watu wengi watabadilishiwa nafasi hapo baadae. Labda uwepo kama formality tuu. Lakini kiuhalisia mifumo ya kidigitali inamulika utendaji wa mtu kwa uwazi sanaa.
 
Watu kama wewe mkipata ajira mkia mnauficha kama sio nyie, baada ya miaka 10 ukigongewa kuachia hiyo ajira utaanza kuleta maneno tofauti na unayoyasema.

WE TULIA MAISHA NI BAHAT, SIO KILA MTU AMEZALIWA ILI ALE KEKI YA NCHI
 
Back
Top Bottom