Ajira Serikalini iwe miaka 10 tu, baada ya hapo watu wastaafishwe

Ajira Serikalini iwe miaka 10 tu, baada ya hapo watu wastaafishwe

Mnajua kweli kuongea ,ukisema hakuna kinacho fanyika maana yake serikali imesimama ,au tafsiri yako ni ipi? Hali ingekuwa hivyo unavyo sema basi mchi hii isinge kuwa hapa ilipo, kikubwa ni nchi kuwa na utamaduni wa kuwajibisha viongozi wakubwa wa serikali na sio kulindana , huku chini watu wanafanya kazi bwana mdogo ndio maana nchi imefikia hapa ilipo, huwezi fananisha tanzania ya miaka 20 au 30 iliyo pita na ya sasa.
Sawa sikatai watu wamefanya kazi, hali iliopo sasa ni kwamba ufanisi sio ule uliokuwepo zama zile. Uzalendo hakuna hilo sijui utaliteteaje. Kazi inaenda na matokeo ila kwa hapa tulipofikia ni dhahiri kazi za mikataba zingeongeza tija. Uzembe unaofanyika serikalini huwezi kuukuta kwenye kampuni binafsi. Utajiuliza ni kwanini? Jibu liko wazi
 
Mnajua kweli kuongea ,ukisema hakuna kinacho fanyika maana yake serikali imesimama ,au tafsiri yako ni ipi? Hali ingekuwa hivyo unavyo sema basi mchi hii isinge kuwa hapa ilipo, kikubwa ni nchi kuwa na utamaduni wa kuwajibisha viongozi wakubwa wa serikali na sio kulindana , huku chini watu wanafanya kazi bwana mdogo ndio maana nchi imefikia hapa ilipo, huwezi fananisha tanzania ya miaka 20 au 30 iliyo pita na ya sasa.
Na kwa kuongezea tulitakiwa tuwe mbali mno ila sababu ya kukumbatiana na kuoneana aibu ndio tupo hapa tulipo. Wenzetu tulioanza nao safari wakajizatiti hatuwagusi kimaendeleo😂
 
Pension ya nini mtoto kaajiriwa na 23 akifika 28 anaachia ofisi hapo unalipwa penshen gani na bado umri mdogo? Kwani wanaopiga kazi kwenye NGO wanalipwaga pension wale baada ya contract ya miaka 5
Unamaanisha makato ya kwenda kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii yasiwepo na hiyo iwe moja kati ya condition za utaratibu huo wa ajira?
Vinginevyo tuondoe neno 'Kustaafishwa'.
Kwa utaratibu wa elimu yetu ni nadra sana kukuta mtoto anaanza kazi rasmi akiwa na 23 years.
 
Kuna kada nyingine sio za kuongelea tu eti kwa sababu baba yako hana ajira

Madaktari bingwa wanapatikana kwa njia ngumu sana sio rahisi kuwastaafisha kwa miaka 10 tu kijana

thats wastage of precious materials

Mtaalam wa mionzi mfano yuko mmoja tu katika hospitali flani, umstaafishe ili iweje?

waalimu wa Sayansi hawatoshi kabisa huko katika idara za Elimu msingi na sekondari, bado uwastaafishe, ili iweje?

SERIKALI INAPASWA KUPAMBANA NA HILI TATIZO LA AJIRA KWA NAMNA YA TOFAUTI, sio hivi ulivyoandika
Bado mleta maada ana hoja kukuzidi wewe mtaalamu wa x,, rays
 
Kwahio point yako ya kwamba wameshafanya kazi na kupata mitaji ni VOID ab INITIO wala ilikuwa haina maana kuiweka hapa sababu hata wewe unapingana nayo...

Kuhusu Sera sio kwamba aliyeajiriwa..., Kuhusu Sera ni kwamba tuliyemuajiri sisi ndio mabosi wake na anakula Kodi zetu hivyo ni kazi yake kutengeneza Sera wala sio Hisani..., Hao ndio kazi ya kutunga Sera..., wanacholipwa ndio wanatakiwa kukifanya..., Na hizo ndoto kwamba 100 percent ya watu wanaweza kujiajiri ndio nimekwambia ni Utopian Idea ambayo umekubaliana nayo paragraph ya kwanza naona tena unaileta hapa....
Tatizo lililopo ni la kimfumo, ata wewe ukipewa hiyo nafasi hutoweza kufanya chochote. Utapiga kelele kwa sababu uko nje ya mfumo, ila ukishaingia nawe unakuwa ni wale wale.
 
Hilo sio sawa, huwezi kuwatoa watu wenye uzoefu.
Ni bora wafanyakazi wote wa serikali wawe na mikataba ya miaka mitano mitano.
Kupata mkataba mpya wa kuendelea na mitano mingine itategenea na uadilifu, ufanisi, uchapa kazi, uzalendo na uzalishaji na matokeo chanya. Vinginevyo chukua mafao yako ukapambane mtaani.
Na wanapokufa hao wenye uzoefu huwa tunafanyaje?
 
sasa ndugu nikuulize,

Deni la bodi ya mikopo atalipa nani kama nikiajiriwa kwa miaka 10 tu?

Kwa kweli ukipewa kitengo cha kutunga sera za uchumi na Siasa utatenguliwa mapema sana
Na mimi mwenye miaka kibao tangu nile hela za heslib nan ananilipia hayo madeni yangu huko maana sijaajiliwa na sina huo mpango tena
 
Tatizo lililopo ni la kimfumo, ata wewe ukipewa hiyo nafasi hutoweza kufanya chochote. Utapiga kelele kwa sababu uko nje ya mfumo, ila ukishaingia nawe unakuwa ni wale wale.
Mtu mmoja hawezi kubadilisha System ila tunapoelekea kinachoendelea sasa hakitaendelea kesho.., Kuna mifumo mingi ilikuwepo Utumwa, Ukabaila na sasa hivi Ubepari ambao kutokana n teknolojia na hakuna uhitaji wa nguvu kazi na wenyewe utakufa kifo cha kawaida..., Uhitaji wa ajira zenye Ujira ni mkubwa kuliko Supply..., Na huwezi kusema kwamba huwezi kufanya cha kufanya wakati unachukua Kodi za watu na wewe kazi yako ni kuhakikisha welfare ya hawa watu....

Kwahio what is currently available is not fit for purpose....
 
Kiburi cha Check number hiki

Hizi ni siasa za waliojiriwa 😂 utaskia jiajirini.. Mara uzoefu sijui blaah blaah. Hivi Tanzania hii wafanyakazi wanaofanya kazi na kuwa audited na measures kama KPI ni % ngapi serikalini? Gavo Imekuwa ni sehemu ya watu kupumzikia maana hamna productivity yoyote zaidi ya kusaini mshahara tu😄 ukiachana na nafasi za udaktari na za ma technicians.
Yana mwisho.
 
Hapa lengo ni lipi kwamba ufanisi?, Wote tupate? Au nini?

Kama umechukulia kama njia ya kuongeza ufanisi kiutendaji ni kwambie hakuna positive impact utapata

Kama ni kusema wote tupate? Jibu ni jepesi,hakuna taifa lolote chini ya jua ambalo watu wake wako katika madaraja sawa.Wapo ambao watapata na wakukosa pia.

Sijui uliwaza nini, lakini hakuna uwiano sawa kati ya mda uliowekeza kwa huyo mtu na time uliyoweka mtu huyo kuproduce(Someone has to spend 17+ years in training and ask them to produce for 10 years only.Don't you see mismatch here?Will you profit from your investment?) Au mada yako ni kuongelea ubinafsi wa mtu nasio kwa malengo ya wengi
Kwani ukifanya kazi hiyo miaka kumi ukapata mtaji unashindwa kuendelea ku produce?
 
Mtu mmoja hawezi kubadilisha System ila tunapoelekea kinachoendelea sasa hakitaendelea kesho.., Kuna mifumo mingi ilikuwepo Utumwa, Ukabaila na sasa hivi Ubepari ambao kutokana n teknolojia na hakuna uhitaji wa nguvu kazi na wenyewe utakufa kifo cha kawaida..., Uhitaji wa ajira zenye Ujira ni mkubwa kuliko Supply..., Na huwezi kusema kwamba huwezi kufanya cha kufanya wakati unachukua Kodi za watu na wewe kazi yako ni kuhakikisha welfare ya hawa watu....

Kwahio what is currently available is not fit for purpose....
Kama mabadiliko yatachukua miaka 50 au 100 ijayo ambapo sisi hatuta kuwepo, kwa nini mabadiliko yafanyike?

Unatakiwa ujue, binadamu ni mbinafsi sana; na asipowekewa mifumo thabiti ataendelea kuwanyonya wengine.​
 
Hapana kwa kutumia rationality, kuna sectors zinafaa kuajiri watu kwa muda mrefu na sectors zingine zinapaswa kuajiri watu kwa muda mfup.

Hicho unachokisema kipo sahihi ila umeegemea katika upande wa watu wanaopaswa kupewa muda katika nafasi za kiutendaji,
Lakini pia tukitizama hao hao madaktari bingwa waliokuwa wachache muda wa miaka kumi ni mingi kazini wanaweza kufanya kazi then baada ya hapo wakawa wakufunzi katika vyuo vikuu vya madaktari hapa nchini na wakasaidia kuzalisha madaktari bingwa wengine wengi, Mbona ni swala linalowezekana kama serikali ikiamua.
Kwahiyo madaktari ningwa wote wae wakufunzi ili Hali huko vyuobi wakufunzi wapo, aise hii akili ya wapi mkuu
 
Kama mabadiliko yatachukua miaka 50 au 100 ijayo ambapo sisi hatuta kuwepo, kwa nini mabadiliko yafanyike?

Unatakiwa ujue, binadamu ni mbinafsi sana; na asipowekewa mifumo thabiti ataendelea kuwanyonya wengine.​
Miaka 50 mpaka 100 ? Hapa juzi tu Gen Z Kenya wamelianzisha..., na sasa hivi wamepoa ila hakuna kilichobadilika hivyo ni kwamba wameweka pause..., Na huku Bongo hawa ambao wapo kindergarten sasa hivi (na Gen Alpha) siku wakiingia mtaani unategemea nini kitatokea..., Ushaona hata mfano wa huyu mleta uzi badala ya kupeleka chuki kwa watunga Sera anapeleka chuki wa walalahoi na wabangaizaji wenzake (sababu hata wao wanachopata hakikidhi mahitaji)

Extreme Poverty anywhere is a threat to Society Everywhere....
 
Back
Top Bottom