Ajira Serikalini iwe miaka 10 tu, baada ya hapo watu wastaafishwe

Unapoteza muda na hii hoja. Unapaswa kutofautisha uendeshaji wa Serikali na kitu kama biashara ya hardware au kufyetua tofali. The more mtu akifanya kazi ndivyo anakua master wa hio kazi.
Zaidi sikuona mtu anasema anataka kwenda kuboresha nini ila imeelezwa kama ni mzunguko wa watu kuajiriwa Serikalini kwa ajili ya kupata fedha.
Kama unasema una elimu nzuri mbona usiombe hata huko private au ukajiajiri?
 
Yeyote anaetamka neno kujiajiri na yuko ofisini Kwa mtu au umma. Hajui Kesho yake la sivyo angefyata mkia. Maana ni ubinafsi ambapo shetani mwenyewe anakaa chonjo.
 
Unatumia kiungo Gani kufikiri kiongozi?
 
Tambua yakuwa hata mifumo ya elimu ipo kuchelewesha watu kukaa madarasani iki waajiriwee umri ukiwa umeenda.

Lakufanya serikali ianze kuajiri watu wenye masters na kuendelea
 
Uzuri wa mabadiliko ya vitu Kama hivi sio Kama kibaka kwamba yatakuja ghafla in the night, Ipo siku.
 
Exactly🤣
 
Huyo mwanzisha thread anaonyesha jinsi vijana wengi wa Tanzania walivyo hovyo kwa sababu elimu haijawasaidia. Na pia wanaongozwa na ubifsi mkubwa. Sasa hao watakaostaafu baada ya miaka 10 wataenda wapi? Kwanza hizo nafasi za ajira ziko ngapi? Badala ya ku push hii serikali zembe iliyojaa kila aina ya ufisadi na watu wanaokaa bure iwajibike wao wanafikiria jambo la kijinga kabisa.
 
Tatizo ni kuwa serikali ya CCM imeshindwa kuendesha nchi kwa sababu viongozi wake hawana hofu ya kushindwa uchaguzi. kishaona nchi ambayo kuanzia rais mpaka wabunge hawawaogopi wananchi na badala yake kila mtu anajitahidi kuwa chawa wa rais ambaye naye ni fisadi na mvivu basi jua kuwa mambo hayataenda.
 
Kabisa, hamna kitachoenda
 
pension funds haiwezi kuwa tatizo ufanye kazi kwa miaka mitatu mitano ishiri is the same thing hesabu ni ile ile tu kaka nishaliweka sawa hapo juu Mbona.
We dogo una ufinyu wa kufikiri
Unajua ni kwa nn serikali ilitunga sheria ya pension 2018 na fao la kujitoa
Kabla ya 2018 mtu aliyekuwa anafanya kaz private mkataba ukiisha anapewa hela zake zotee
Sasa hivi hupewi hadi ufikikishe miaka 60
Unavosema pension sio tatizo unafikir wewe ndiyo paymaster wa serikali unaweza kulipa wastaafu zaid ya 50,000 kila baada ya miaka kumi
Huoni tutakuwa na taifa la wastaafu vijana wengi sana ambao wangetakiwa wazalishe na kutoa huduma
 
tutafute njia bora zaidi za kuongeza nafasi za ajira
 
We ni empty vessel kweli.
Watu kama nyie ndy Eid Amin alikuwa anawatupa mto kagera.
 
Yani mimi ningekuwa nimesha staafu miaka mingi?

Acha kabisa Serikali mgeikuta ni mifupa mitupu, yani miaka kumi watu wangejuwa wanarudi nyumbani na mizigo ya pesa, Maana najua baada ya miaka 10 sina ajira, Naenda wapi?

Mfuko wa mafao hakuna kitu, mikopo ya chuo sijamaliza, Nyumba sina, watoto hawajalipiwa ada, mimi na mke wangu ahtujala ,bado misaada ya ndugu. Duh mge tuua kwa stress.

Acheni tuzekee kazini, tukifa nanyi mtakuja mzekee humu.
 
We ni empty vessel kweli.
Watu kama nyie ndy Eid Amin alikuwa anawatupa mto kagera.
Hujui kitu
Huyo idi amin wako alikimbia nchi shaur ya mawazo mgando kama yako
Tatizo lako huna ajira na sasa hivi kuna interview duuuh hatariiii lazima ulie
Njoo huku private tule maisha
Huku private ni utendaji wako na ubunifu wako hakuna usumbufu
 
Hujui kitu
Huyo idi amin wako alikimbia nchi shaur ya mawazo mgando kama yako
Tatizo lako huna ajira na sasa hivi kuna interview duuuh hatariiii lazima ulie
Njoo huku private tule maisha
Huku private ni utendaji wako na ubunifu wako hakuna usumbufu
Haya bana umeshinda mkuu. Endelea Kula maisha mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…