KERO Ajira zirudi TAMISEMI tu, huku AJIRA PORTAL ni kupotezeana muda tu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Pole, ndo shida ya kusomea mitihani badala ya uelewa.
Mfumo wa elimu yetu upo hivyo. Usimlaumu mtihitimu Bali ilaumu serikali dharimu ya Ma CCM iliyojaa watu wenye roho mbaya na wanaojali maslahi Yao na familia zao. Serikali ya roho mbaya, unamkalisha mtu kitaa Kwa miaka kumi unakuja kumfanyia mtihani unaofanana na yule aliyemaliza mwaka mmoja uliopita. Maamuzi ya namna hii hufanywa na watu wenye roho mbaya tu na mashetani pekee na wala si binadamu wenye utu na mwenye kumuogopa Mungu. Shame on you Ma CCM
 
Key of differentiated jomba hujui kweli sisi walimu hatari tupu nimemaliza 2015 lakini siwezi shindwa hizo
Inaonekana wewe ni miongoni mwa wanufaika wa mfumo mbovu wa CCM.
 
Hamuwezi kuajiriwa wote ndugu yangu, We kubali tu.
Nani kakwambia anataka waajiriwe wote?? Maneno haya tunayasikia kutoka Kwa watu waliolifikisha taifa hili hapa tulipo na hawataki kuamini kama wao ndio wamechangia kutufikisha hapa tulipo. Kama wewe unategemea ajira ya kuteuliwa Kwa sababu Babu/bibi/baba/mama/mjomba au shangazi anajuana au alikuwa kada mtiifu wa CCM ambao ndio wametufikisha hapa, Kaa tu pembeni Hauna ulazima wowote wa Kuweka comment yako hapa.
 
Ndo maana nimeanza na kumpa pole.
 
Hapana, mikando ni lazima, hatutaki walimu vilaza mashuleni
 
Ni wapi serikali ilikwambia ukimaliza chuo wanakuajiri?? Nenda shule za private zimejaa nchi nzima.
 
Hii Geography ya wapi tena jamani...Kwamba ndio mambo yamebadilika ivi?
 
Kulialia hakutakusaidia.

Ukifanya application ya kazi PSRS anza kula msuri hakuna njia ya mkato Jamaa utalia sana humu.

Hakuna wa kukuletea sahani ya chakula mezani pambana uipate.
 
Serikalini huwa hakuna interviews Bali ni kufanya mitihani na anapata maksi nyingi ndo mshindi na ndio maana hakuna ku-shortlist wanachofanya ni kuita kundi lote au kubwa mtajijua.
 
Nenda kapambane na usaili jombaa.

Hakuna njia ya mkato ya kuapata kazi watu wamepambana sana na usaili zaidi ya miaka mitano ndio wanatoboa.

Walimu usaili mmoja mnaanza kulialia kazeni buti wasomi ni wengi hakuna ajira za burebure.
Walimu na afya walizoea kupewa kazi bila interviews, sasa kimewakuta na uzuri huwezi kukosa cha kujibu japo sio straight lakini kwa maneno mengine ya kuokoteza okoteza, vinginevyo mtu awe mweupe sana na hapo jopo ndo litakapoona huyu si wa kumpa dhamana ya wanafunzi
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ Ww tena πŸ˜‚πŸ˜‚

Kwahy ulitaka uambiwe maswali yatatokea wapi πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sasa shule ungeenda kufundisha nn
 
Huko tamisemi ndio utawapangia maswali ya kukuuliza? Jiandae kabla ya paper
 
Jiunge na chadema ili upate haki yako πŸ˜‚
 
Nimeshafanya mitihani yao mitatu nyingine nilifika oral but sikuitwa na vitu wanavyouliza ni kukomoana , Baada ya hapo nikaachana na hiyo biashara ya utumishi. Nimefanya interview na mashirika mawili ya kimataifa tena panel ya watu tisa na interview za online na kupata moja ya shirika ambalo nafanya hadi now . Nasisitiza pale utumishi amna interview ni ujinga ujinga tu kuna watu nawafahamu mmoja yuko jimbo la kassimu alipata 49 below 50 leo yuko kazini . Hapo utaelewa namaanisha nn na sio kwamba maisha utayapata kupitia utumishi kuna fursa kila mahali za kumtosha kila mtu , kuna organization itaona potentially yako hivyo milango ya fursa bado ni mingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…