Joseph Patrick Ngonyani mkazi wa Kijiji cha Makuyni kilichopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro amejiua kwa kujinyonga ikiwa zimebaki siku 29 afunge ndoa.
Uchunguzi wa chanzo cha kifo chake bado unaendelea.
Godlisten Malisa ameandika haya katika ukurasa wake wa Facebook kuhusu kifo cha Joseph Ngonyani (rafiki yake):
Mwezi August mwaka huu ulimvalisha pete mchumba wako na ukatuomba support marafiki zako kwa ajili ya ndoa yenu uliyopanga kuifunga mwezi December mwaka huu. Tulikutakia heri na kuahidi ushirikiano. Lakini leo nimeshtushwa na taarifa ya kifo chako cha ghafla. Nimeambiwa umejinyonga. What a shocking news.!
Rafiki na mdogo wangu #JosephNgonyani nini kimekusukuma kufanya uamuzi huu mgumu namna hii? Zilibaki siku chache tu kuelekea ndoa yako. Itakuaje sasa kwa mchumba wako? Je mipango yote mliyopanga ndio imeishia hapa? Kwanini hukutishirikisha ikiwa kuna jambo gumu uliloshindwa kulimudu? Daah. Just rest in peace bro. Nimeishiwa maneno.!
Wanaume tunapitia mengi sana. Baada ya kuweka taarifa ya dogo #JosephNgonyani kujinyonga, ndugu Mathew Mfinanga ameamua kushare sehemu ya mapito yake. Ni magumu sana, lakini jambo la muhimu tusiache kuongea. Kama unapitia changamoto ukaongea na watu 100 wasipokuelewa, basi kuna mmoja atakuelewa. Na Mungu atamtumia huyo mmoja kubadili story ya maisha yako.
Wanaume wengi hufikia hatua ya kujiua kwa kutokuongea, au kuona wakiongea watakua wamejidhalilisha. Please talk to save ur life. Taarifa ya taasisi ya afya ya akili nchini Marekani (National Institute of Mental Health) inaonesha kuwa 77% ya watu wote wanaojiua ni wanaume. Hizi takwimu zinatisha. Moja ya sababu ya wanaume "kukimbilia" kujiua ni kushindwa kuongea wanapopitia magumu.
Wanawake hawajiui kirahisi kwa sababu wanaongea sana. Katika kuongea kwao wanaweza kupuuzwa au kusaidika, lakini la muhimu wameongea. Kuongea kunapunguza mzigo, kunakupa nafasi ya kufikiria tena, kunakuwezesha kupata mawazo mapya, kunasaidia kujipanga upya. Kujiua ni ubinafsi. Ni kuacha mzigo mkubwa kwa wale waliokua wanakutegemea. Ni kuacha alama ya maumivu yasiyokoma kwa wanao, mke na ndugu zako. Kujiua sio suluhisho. Wanaume tuongee, tuongee, tuongee.!
Mchangiaji mmoja pia ametoa ushuhuda wake kuhusu alivyopitia hali ya sonona (See atached image) :