Ajiua kwa kujinyonga siku chache kabla ya harusi yake

Ajiua kwa kujinyonga siku chache kabla ya harusi yake

Labda nikutie moyo tu, nioneshe tajiri mmoja tu Africa mwenye umri kama wako ambaye utajiri wake sio wa kurithi.

Waliosema life start after 40 hawakuwa wajinga.

Sasa hapo mwanamke atakayekubali kuwa na mahusiano na wewe huyo ndio Mke wa kweli wa kuja kumuowa achana na wajinga wanaokwambia tafuta pesa.
Asante mkuu....upo sahihi sana

Changamoto ni kwmba sina kazi wala biashara ya kuingiza 100.......

Hapa nafikiria nikaombe wapi kazi yoyote.
 
Joseph Patrick Ngonyani mkazi wa Kijiji cha Makuyni kilichopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro amejiua kwa kujinyonga ikiwa zimebaki siku 29 afunge ndoa.

Uchunguzi wa chanzo cha kifo chake bado unaendelea.

Godlisten Malisa ameandika haya katika ukurasa wake wa Facebook kuhusu kifo cha Joseph Ngonyani (rafiki yake):
Mwezi August mwaka huu ulimvalisha pete mchumba wako na ukatuomba support marafiki zako kwa ajili ya ndoa yenu uliyopanga kuifunga mwezi December mwaka huu. Tulikutakia heri na kuahidi ushirikiano. Lakini leo nimeshtushwa na taarifa ya kifo chako cha ghafla. Nimeambiwa umejinyonga. What a shocking news.!

Rafiki na mdogo wangu #JosephNgonyani nini kimekusukuma kufanya uamuzi huu mgumu namna hii? Zilibaki siku chache tu kuelekea ndoa yako. Itakuaje sasa kwa mchumba wako? Je mipango yote mliyopanga ndio imeishia hapa? Kwanini hukutishirikisha ikiwa kuna jambo gumu uliloshindwa kulimudu? Daah. Just rest in peace bro. Nimeishiwa maneno.!

Wanaume tunapitia mengi sana. Baada ya kuweka taarifa ya dogo #JosephNgonyani kujinyonga, ndugu Mathew Mfinanga ameamua kushare sehemu ya mapito yake. Ni magumu sana, lakini jambo la muhimu tusiache kuongea. Kama unapitia changamoto ukaongea na watu 100 wasipokuelewa, basi kuna mmoja atakuelewa. Na Mungu atamtumia huyo mmoja kubadili story ya maisha yako.

Wanaume wengi hufikia hatua ya kujiua kwa kutokuongea, au kuona wakiongea watakua wamejidhalilisha. Please talk to save ur life. Taarifa ya taasisi ya afya ya akili nchini Marekani (National Institute of Mental Health) inaonesha kuwa 77% ya watu wote wanaojiua ni wanaume. Hizi takwimu zinatisha. Moja ya sababu ya wanaume "kukimbilia" kujiua ni kushindwa kuongea wanapopitia magumu.

Wanawake hawajiui kirahisi kwa sababu wanaongea sana. Katika kuongea kwao wanaweza kupuuzwa au kusaidika, lakini la muhimu wameongea. Kuongea kunapunguza mzigo, kunakupa nafasi ya kufikiria tena, kunakuwezesha kupata mawazo mapya, kunasaidia kujipanga upya. Kujiua ni ubinafsi. Ni kuacha mzigo mkubwa kwa wale waliokua wanakutegemea. Ni kuacha alama ya maumivu yasiyokoma kwa wanao, mke na ndugu zako. Kujiua sio suluhisho. Wanaume tuongee, tuongee, tuongee.!

Mchangiaji mmoja pia ametoa ushuhuda wake kuhusu alivyopitia hali ya sonona (See atached image) :
Unataka kusaidiwa wakati unapesa ulikua unawasaidia wenzako
 
Asante mkuu....upo sahihi sana

Changamoto ni kwmba sina kazi wala biashara ya kuingiza 100.......

Hapa nafikiria nikaombe wapi kazi yoyote.
Pole sana ndugu.
Tatizo ninaloliona kwako unachagua kazi. Fanya hata vibarua,mwanaume unakosaje hata Mia wakati hata ukiamua kuchota maji ya madumu na kuyauza unapata faida ya sh.100 kila dumu.
Umeshindwa hata kuwa dereva wa bodaboda au Bajaj au ukafanya day worker? You are not serious at all.
 
Wakumpa bodaboda au bajaji ni Nani?
Hujui Kama kupata boda boda au bajaji pia inahitaji connection ? Sasa Kama Hana connection hicho unachosema hakiwezekani kabisa.

Kuna kipindi nikiwa nimemaliza chuo Sina mbele Wala nyuma ,nikawa natamani hata saidia fundi kwa siku buku tano lakin nikawa nakosa ,unamfuata fundi ili muongozane anakwambia tayar nipo na watu wangu.
Unaenda viwandani nako unaishia getini wanachukuliwa wanaojulikana na masupervisors .
Hayo maji unayoyasema atachota baharini?
Vipi dumu za kuwekea hayo maji hujui yanapatikana kwa pesa ?
Na je hujawaza mkokoteni wa kubebea hayo maji ni mtaji unatakiwa hapo?

Ujue kuongea ni rahisi Sana hasa Kama hujawahi pitia hizi changamoto..
Watu wanapambana lakin inashindikana kabisa ,ndio hapo watu wanaamua kujiua maana anaona Kama dunia inamzomea na imemnyea.
Zaid hapa tutoe mbinu nyingi nyingi ili wenzetu waweze kujikwamua kwa kumwambia fanya iki na kile Ila sio kuwaona hawana mbinu au hawana akili mpaka wakakosa had kazi za kuwapatia hata 100.
 
Well said mkuu

Uishi Maisha marefu
 
Kila kitu kinapaswa kwenda kwa vipimo, mizani ikilemea upande mmoja ujue kuna tatizo mbele.
Ila mkuu tunaishi kwanza, kupendwa kunafuata, embu jiulize unaishi ili upende na kupendwa au unapenda au kupendwa ili uoshi?
 
Wakumpa bodaboda au bajaji ni Nani?
Hujui Kama kupata boda boda au bajaji pia inahitaji connection ? Sasa Kama Hana connection hicho unachosema hakiwezekani kabisa.

Kuna kipindi nikiwa nimemaliza chuo Sina mbele Wala nyuma ,nikawa natamani hata saidia fundi kwa siku buku tano lakin nikawa nakosa ,unamfuata fundi ili muongozane anakwambia tayar nipo na watu wangu.
Unaenda viwandani nako unaishia getini wanachukuliwa wanaojulikana na masupervisors .
Hayo maji unayoyasema atachota baharini?
Vipi dumu za kuwekea hayo maji hujui yanapatikana kwa pesa ?
Na je hujawaza mkokoteni wa kubebea hayo maji ni mtaji unatakiwa hapo?

Ujue kuongea ni rahisi Sana hasa Kama hujawahi pitia hizi changamoto..
Watu wanapambana lakin inashindikana kabisa ,ndio hapo watu wanaamua kujiua maana anaona Kama dunia inamzomea na imemnyea.
Zaid hapa tutoe mbinu nyingi nyingi ili wenzetu waweze kujikwamua kwa kumwambia fanya iki na kile Ila sio kuwaona hawana mbinu au hawana akili mpaka wakakosa had kazi za kuwapatia hata 100.
Mkuu ndio walimwengu tulivyo....
 
Wazee hili laifu sio poa hasa ukiwa mzaliwa wa kwanza...kwa kifupi mimi pia napita hardtime sana

Sina kazi (jobless)

Kodi yangu inaisha December (kichwa kinauma machozi yanatoka)

Umri umesogea miaka 26 mates wenzangu wengi wana maisha na darasani nilikuwa bora kuliko wao.nimeomba makazi ya majeshi yote mwaka jana mpka nimekataa tamaa

Kula yangu mzozo,unaumwa ila unapona kwa nguvu za Mungu...

Kushinda week mfukoni huna mia ni kawaida

Kwa kifupi depression is real ukiona unaaamka unakula unavaa mshukuru Mungu

Mungu anisaidie nivuke salama nakiri sometimes najifikiriaga sana kujipoteza(kujitoa uhai) sema namuonea huruma mama na madogo zangu.
Heb niambie dm kabila lako naelimu yako na upo mkoa gani naeza kusaidia mahali
 
Waafrika sisi au kuna waafrika kwenye bara lingine?.

"Mwanaume aongei sana asee.." hiyo ndiyo moja ya kauli inayotamkwa sana na binadamu wa kutoka Afrika na hata unapoongea kwa mmoja mmoja ili kupata hafueni basi ni kama umebeba kipaza sauti ukitangazia umma!.
 
Back
Top Bottom