Akili ni nywele: Wakati Wizara ya Ardhi Bongo wanahangaika na clinic za ardhi, Kenya wameanza kubomoa na kuyajenga upya maeneo yaliyojengwa vibaya

Akili ni nywele: Wakati Wizara ya Ardhi Bongo wanahangaika na clinic za ardhi, Kenya wameanza kubomoa na kuyajenga upya maeneo yaliyojengwa vibaya

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Kila siku nasema kuwa akili ni nywele.

Ukiwa na akili timamu, utajua tatizo ulilonalo ni lipi na utaweka na kutekeleza mipango sahihi ya kulitatua hilo tatizo.

Wenzetu Kenya waligundua wana tatizo la mipango miji, kwa maeneo mengi kujengwa vibaya bila mpangilio na kufanya wananchi wengi kuishi kwenye maeneo ambayo hayana hadhi na staha kwa binadamu wa kawaida.

Hivyo wamekuja na mpango wa kubomoa maeneo hayo na kuyajenga upya. Saivi Kibera imeanza kuvinjwa na kujengwa upya. Mukuru imeanza kujengwa flats nzuri kwa ajili ya makazi ya wananchi wa kawaida.

Kwa upande mwingine huku kwetu bongo kama kawaida yetu, Tuna tatizo la makazi holela na ujenzi usio na mpangilio ila Wizara ya Ardhi wako na cliniki za ardhi. Eti kutatua migogoro ya ardhi ambayo kiuhalisia imesababishwa na wao kutotimiza wajibu wao wa kuifanya nchi yetu kupangwa na kujengwa vizuri. Mbaya zaidi wamelala tu huku kila siku maeneo ambayo hayajajengwa vizuri kwa mpangilio yanazidi kuongezeka nchini.

Kila siku nitasema. Akili ni nywele na bila kuwaondoa CCM tutazidi kuwa vituko hadi kiama.
Screenshot_20241217_081420_Facebook.jpg
FB_IMG_1734412856599.jpg
Screenshot_20241217_081336_Facebook.jpg

FB_IMG_1734414982619.jpg
Screenshot_20241217_090052_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom