Akili ya BMW kwenye Magari

Iweke garage mkuu,chukua pikipiki
 
Asante sana Mkuu
 
Iliungua balbu ya taa ya mbele tukazunguka Dar nzima ikapatikana kwa 120,000/=
 
BMW X3 toleo la kwanza za dizeli zote ni Xdrive.

Kama yako ilikuwa inavuta nyuma tu, then kuna shida mahali.
 
BMW X3 toleo la kwanza za dizeli zote ni Xdrive.

Kama yako ilikuwa inavuta nyuma tu, then kuna shida mahali.
Inawezekana. Maana hata reviews nilikuwa nikizitazama naona hichi ulichoandika. Nilishaiuza, ni miaka imepita.
 
Zinakwama Land cruiser maporini huko anazungumzia Bima watu wengine bhana kwa hiyo anataka kuaminisha jamii kuwa hizi gari za starehe kama server ya TRA inavyotambua iende kwenye matope huko isikwame wakati pana muda hata Land rover unafikiri upite au ugeuze maana anaweza kupita popote ni Nissani chura..na Nissan nyingi zipo sawa kwenye tope..
 
Bado hakuna mantiki kwenye comment yako
 
Hoja yake huyo jamaa ni nyepesi mno na haina mashiko
 
Gear box ya DSG hata BMW, wanatumia sana, angalia kwenye min coper, na baadhi ya BMW na hizi ndio zinafanya kumuumiza kichwa mjapani
 
BMW ni gari nzuri lkn kila siku lazima itakuwa inafeli mahali. Lazima itasumbua. Kuna madudu mengi sana ambayo inabidi urekebishe na ufuatilitie muda wote, haswa kama ni model ya zamani. Ni gari ambayo vifaa vinafeli kwa kasi, kimoja baada ya kingine.
 

Pia usisahau, BMW ndio gari ya kwanza kutengeneza V8 engine ambayo ina twin turbo ambazo zipo kwenye lile bonde la pale katikati. Wanaita Hot Vee V8 engines.

Yaani wakati kampuni zingine zikitengeneza v8 engines pale kati wanaweka intake manfold. Halafu turbo wanaziweka huko pembeni na kupelekea engine kuchukua sehemu kubwa.

BMW wakaja na Hot Vee engine ambayo ni N63 ambayo kwa mara ya kwanza waliiweka kwenye X6.

Hii Hot Vee layout ina advantages mbili.

1. Inapunguza sana turbo lag, kwa sababu turbo zipo karibu na exhaust manfold.

2. Inafanya engine kuchukua sehemu ndogo. Tofauti na turbo zikikaa huko pembeni.

Hiyo point namba 1 ya turbo lag ni mojawapo ya sababu kwanini BMW X5 m competition na BMW X6 M competition zinanyanyasa sana huko barabarani hasa F series na G series. Mliozifatilia hizi gari nadhani mnaujua moto wake.

Ingawa hiyo N63 engine yale matoleo ya mwanzo ilileta shida sana probably walishindwa kucontrol joto kubwa hasa ukizingatia engine ni direct injection plus twin turbos.

Ila matoleo ya mbele yake walifix hizo failures na sasa ni moja kati ya best high end perfomance engines za BMW.

Audi, Mercedes, Porche wameshaadapt aina hiyo ya engine.

Toyota ndio wanafile patent sasa hivi nao walete chuma kama hicho.

For real these BMW guys wana akili ya peke yao.
 
Wajerumani wako more advanced kwenye industry ya magari mara nyingi huwa naangilia kwenye channel ya NATIONAL GEOGRAPHIC na DISCOVERY FAMILY jinsi wajerumani wanavyofanya tafiti na kufanya design za magari hakika hawa jamaa ni noma
 
B58 & S58 engines zina balaa si kidogo.
 
BMW ilianza kama kampuni ya kutengeneza engines kabla ya kuanza kutengeneza magari.. Kwahiyo likija swala la engines hapo ndio penyewe..!

Engines za BMW zina character ya tofauti.. Zinahitaji uzipush.. BMW sio gari ya kuendesha kama Toyota kwenye 2500rpms.. BMW engine inakuwa alive kuanzia 4000rpms mpaka redline bila kukata puff..
Head design yao ni hatari.. flow ya hewa kwenye engines zao ni unmatched..!

Engines za performance kwa Toyota kama 3sgte..3M kwenye Toyota 2000GT..1LR kwenye Lexus LFA.. Imebidi ashirikiane na Yamaha.. Kupata head nzuri..!ndio maana ukiendesha 3gste unapata kusmile jinsi engine inavyobehave.. Inapumua vizuri.. Character ya BMW..

Mwisho kabisa.. Toyota Supra ambayo ni legendary/icon kwa Toyota imekubali kuwa powered na mashine ya Bavaria..wamenyoosha mikono hapo..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…