Akili za umasikini: Bajeti ya Elimu $5B, lakini bajeti ya Kilimo in $500M

Akili za umasikini: Bajeti ya Elimu $5B, lakini bajeti ya Kilimo in $500M

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Ninaomba kuwasalimia wana jamii kwa jina la utukufu wa juu, pili ningependa kuwaomba tujadili kuhusu mgawanyo wa bajeti ya Kenya katika sekta za kilimo na Elimu.

Kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa la Kenya, zaidi ya 75% ya Wakenya huishi vijijini kwa kutegemea Kilimo, kilimo ndicho kinachotoa ajira nyingi zaidi kuliko sector yoyote ile, ni namba mbili kwa kuipatia Kenya fedha za kigeni, kilimo ndicho kinachotegemewa kwa kuzalisha malighafi za viwandani.

Kenya ni nchi yenye kukumbwa na njaa kila mwaka na watu wengi hufariki kutokana na njaa, Kenya ni nchi pekee hapa Afrika ambayo inategemea Chakula cha msaada kulisha watu wake isiyokuwa na vita vya ndani.

Kenya ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo kama ingetumia ardhi yake vizuri kwa kuwekeza katika miradi mikubwa mikubwa ya umwagiliaji kama ule wa Galana kulalu, ingeweza kuzalisha Chakula cha ziada hata kusafirisha nje ya nchi.

Hivi katika mazingira hayo ambapo uchumi wa nchi umeshikiliwa na Kilimo, kuwekeza $500M katika wizara ya Kilimo na kuwekeza $5B katika Elimu?. Ikumbukwe kwamba Elimu kimsingi ni miongoni mwa "recurrent expenditure", kwamba pesa nyingi hutumika kulipa mishahara ya walimu, wakati kwenye KILIMO asilimia kubwa huingia katika uwekezaji hivyo kuzalisha pesa nyingi zaidi ili kuendesha uchumi WA nchi na kupunguza gharama za maisha.

Naomba kuwasilisha.
 
Elimu tunawalipa walimu.
Kwani kilimo tunawalipa wakulima?Au tunawanununulia mbegu?.
Hahahaha,
1) Mikopo yenye riba nafuu, au isiyo na riba kwa wakulima
2) Kuwekwa miundombinu ya umwagiliaji maji, hasa katika sehemu zenye jangwa
3) Kuchimba Visima na mabwawa kwa ajili ya mifugo na KILIMO
4) Kuweka ruzuku kubwa katika mbolea, mbegu, dawa na zana zingine za ufugaji na KILIMO
5) Kununua mazao ya wakulima(hasa ya Chakula) pale ambapo bei ya mazao yao ipo chini ili kuwaepusha na hasara.
6) Kuhakikisha maghala ya Taifa yananunua na kuhifadhi Chakula cha kutosha muda wote.

Kama kweli Serikali ya Kenya inazingatia na kutoa kipaumbele uchumi na maisha ya wajenya wa hali ya chini, hiyo $5B ingepeleka kwenye KILIMO, zaidi ya wajenya 25M wangesaidika, wangeweza kuinua vipato vya familia zao na kuweza kugharimia Elimu ya watoto wao.

Kilimo kibaathiri sector zingine zote "directly" and within very short time.
 
We huwajui wakenya..hizo zote ni siasa
Watazinywa hizo hela wakulima haziwafikii.

Na Tanzania pia ukiwapa hela nyingi zinaishia seminar Kwa mabwana kilimo na wizarani.
Wanazinywa zote.

Siku zote ndo hivyo..kwenye maandishi mipango mizuuri Kwenye kutekeleza
Ni tofauti..
 
Baba wa taifa alisisitiza Elimu dhidi ya adui ujinga, umasikini na magonjwa.

Elimu, Elimu, Elimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujinga, maradhi na Umasikini, yote haya yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa haraka sana kama mtu au taifa litafanikiwa kupambana na umasikini, ndio sababu mtu aliyeelimika bado anaweza kuendekea kuwa masikini na kushambuliwa na maradhi, ila tajiri hawezi kukosa Elimu au kukosa afya bora, labda kama ameamua mwenyewe.
 
We huwajui wakenya..hizo zote ni siasa
Watazinywa hizo hela wakulima haziwafikii.

Na Tanzania pia ukiwapa hela nyingi zinaishia seminar Kwa mabwana kilimo na wizarani.
Wanazinywa zote...

Siku zote ndo hivyo..kwenye maandishi mipango mizuuri Kwenye kutekeleza
Ni tofauti..
Sio kipindi hiki cha Magufuli, kuliko ule pesa ya Serikali sasa hivi, ni bora umeze sumu.
 
Kwa hili nawaunga mkono wakenya, huwezi kuwa na kilimo bora kama huna elimu bora.

Wakenya hongereni.
Hahaha, huwezi kuwa na Elimu bora bila lishe bora. Huwezi kwenda kusoma ukiwa na njaa, viwanda havizalishi kwa kukosa Mali ghafi, familia hazina ajira, na uchumi WA nchi umelala.
 
Ujinga, maradhi na Umasikini, yote haya yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa haraka sana kama mtu au taifa litafanikiwa kupambana na umasikini, ndio sababu mtu aliyeelimika bado anaweza kuendekea kuwa masikini na kushambuliwa na maradhi, ila tajiri hawezi kukosa Elimu au kukosa afya bora, labda kama ameamua mwenyewe.
Yani unasema mtu aliyeelimika anaweza endelea kuwa masikini na kushambuliwa na maradhi?

Kuna kitu hakipo sawa kwako.

Kuna kupata elimu na kuelimika.

Bado serikali zinawajibu mkubwa sana katika kuelimisha jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kenya tunahitaji wasomi. (Highly skilled workers)
Vitunguu, mboga na hoho tutanunua Tanzania.
Kenya mnahitaji wasomi lakini hamuhitaji uhai watu wenu, vipi mnakubali kuona mamia ya raia wenu wanakufa kwa njaa kila mwaka lakini bado hamuwasaidii badala yake mnaongeza idadi ya wasomi wa vyuo vikuu wanaozurura na kukaa mchana kutwa pale Uhuru park.

Lazima idadi ya wasomi iendane na " Job creation ", bila kilimo na ufugaji" wapi mtatengeneza ajira za kuweza kuwaajiri hao wasomi mnaowazalisha kwa wingi?
 
Elimu tunawalipa walimu.
Kwani kilimo tunawalipa wakulima?Au tunawanununulia mbegu?
Mh. Lowassa kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 alikuwa ana kauli mbiu yake ilikuwa inasema kwamba kipaumbele chake cha kwanza ni ELIMU cha pili ni ELIMU, cha tatu ni ELIMU na cha nne ni ELIMU!
 
Back
Top Bottom